Mkurugenzi Pangani asimamishwa

Mkurugenzi Pangani asimamishwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
IMG_9238.jpg
 
Pole kwa Mkurugenzi.

Halmashauri kuna majungu sana. Kutafutana kwingi.
 
Lakini hawa wakueugenzi wana mambo. Kwanini hakutaka kulipa deni la supplier.
Huwezi kujua sababu kwa sababu DED hatujamsikia.

Ila majukumu ya hawa wakurugenzi ni mengi sana na yenye kuwagusa wananchi moja kwa moja.

Huenda alikabiliwa na bill nyingi ikambidi acheleweshe, na huenda supplier naye ana mizizi kwa wakubwa huko wenye nguvu.
 
Wakurugenzi sio wakuhurumia ni wapuuzi sana kazi kula hela tu!
Wakurugenzi wa Halmashauri jumla yao ni 185.

Huwezi kuniambia kwamba wote ni walaji wa hela.

Ninavyofahamu wana majukumu mengi na wanafanya kazi katika mazingira tofauti ya kisiasa na kiutendaji. Anaweza akawa sawa kiutendaji ila kisiasa wakamkataa.

Ukurugenzi ni kazi ambayo muhusika anatakiwa amridhishe aliyemteua, wananchi anaowatumikia na wanasiasa ambao ni wenye maamuzi na Halmashauri.

Huwezi kukuta Mkurugenzi anamfurahisha kila mtu.
 
Hiyo ni salamu tosha kila anachofanya Makonda kina baraka za mwenyekiti mwenyewe nyuma yake, sasa jichanganye.
 
Huwezi kujua sababu kwa sababu DED hatujamsikia.

Ila majukumu ya hawa wakurugenzi ni mengi sana na yenye kuwagusa wananchi moja kwa moja.

Huenda alikabiliwa na bill nyingi ikambidi acheleweshe, na huenda supplier naye ana mizizi kwa wakubwa huko wenye nguvu.
Nilimsikia anasema walitaka tiles za 60*60 supplier katoa 40*40 ndo maana malipo yamechelewa mwaka mzima.
Mpaka kitu cha ujenzi kinaagizwa it means fungu lipo. Na kama supplier kaleta kitu tofauti na quotation ilitakiwa wakatae order sio unatumia halafu kulipa mwaka unapita eti karatasi....
 
Hii nchi sometimes iende tu kimakonda makonda
 
Wakurugenzi wa Halmashauri jumla yao ni 185.

Huwezi kuniambia kwamba wote ni walaji wa hela.

Ninavyofahamu wana majukumu mengi na wanafanya kazi katika mazingira tofauti ya kisiasa na kiutendaji. Anaweza akawa sawa kiutendaji ila kisiasa wakamkataa.

Ukurugenzi ni kazi ambayo muhusika anatakiwa amridhishe aliyemteua, wananchi anaowatumikia na wanasiasa ambao ni wenye maamuzi na Halmashauri.

Huwezi kukuta Mkurugenzi anamfurahisha kila mtu.
Huyo Mkurigenzi hatekelezi miradi hela ameshapokea! Halipi wazabuni kwa kisingizio tu!
Huyo ni mpuuzi aondoke tu!
 
Nilimsikia anasema walitaka tiles za 60*60 supplier katoa 40*40 ndo maana malipo yamechelewa mwaka mzima.
Mpaka kitu cha ujenzi kinaagizwa it means fungu lipo. Na kama supplier kaleta kitu tofauti na quotation ilitakiwa wakatae order sio unatumia halafu kulipa mwaka unapita eti karatasi....
Katika Halmashauri lolote linaweza kutokea.

Inawezekana kulikuwa na majadiliano mengine lakini supppier kaamua kuchukua hatua za kisiasa kumkomesha!
 
Huyo Mkurigenzi hatekelezi miradi hela ameshapokea! Halipi wazabuni kwa kisingizio tu!
Huyo ni mpuuzi aondoke tu!
I agree ukimsikiliza Hana hoja . Swali lilikua unadaiwa hudaiwi...kama unadaiwa na fungu lipo unachelewesha malipo Kwa mwaka mzima kisa technicality
 
Katika Halmashauri lolote linaweza kutokea.

Inawezekana kulikuwa na majadiliano mengine lakini supppier kaamua kuchukua hatua za kisiasa kumkomesha!
Maybe ila wanalalamikiwa sana kuchelewesha miradi ili Hali utakuta mzigo ushaingia kutoka serikali kuu. Sijui lengo ni nini hasa
 
Hawa ndo wanafanya miradi isianze wanachukua hela wanachelewesha malipo na kuzalisha riba na kutesa wananchi!
I agree ukimsikiliza Hana hoja . Swali lilikua unadaiwa hudaiwi...kama unadaiwa na fungu lipo unachelewesha malipo Kwa mwaka mzima kisa technicality
 
Kwahiyo ametumbuliwa sababu kachelewesha malipo Kwa Supplier?

Basi wakurugenzi wote watumbuliwe Kwa sababu hakuna Halmashauri ambayo haidaiwi na hawa suppliers.
 
Wote Nyinyi ni watafuta sababu tu!
Mkurugenzi kama hajapokea hela hakuna shida lakini sio kutesa wazabuni huku hela ipo zaidi ya miaka 2!
 
Back
Top Bottom