Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Missenyi shtuka haraka

PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
335
496
Inawezekana hujui kinachoendelea kwenye idara ya Ardhi na hasa kwenye uuzaji wa viwanja unaoedelea sasa.Inaelekea ama kwa kujua au kutojua umewaamini sana watumishi wa idara ya ardhi Ila usiposhituka utapambana na migogolo mingi ambayo ingeweza kuzuilika kama mchakato wa uuzaji wa viwanja ungesimamiwa kwa weledi, uaminifu na uadilifu.

Mchakato wa uuzaji wa viwanja hivyo umegubikwa na viashiria vya ukiukwaji wa taratibu na kutengeneza mianya ya rushwa na kupelekea kusababisha migogolo isiyokuwa ya lazima hapo baadae.

Mkurugenzi shutuka, Watanzania siyo wajinga Baba.
 
Back
Top Bottom