Mkurugenzi mstaafu wa ujasusi Uingereza: Iran amemzidi Marekani kwenye hii vita

Mkurugenzi mstaafu wa ujasusi Uingereza: Iran amemzidi Marekani kwenye hii vita

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,438
Reaction score
69,163
Mwaka 1907 Balozi wa Uingereza nchini Ujerumani Eyre Crowe aliaandaa andiko zito "The Crowe Memorandum" na kulituma London. Mle ndani alisema kwamba Ujerumani inakusanya chuma na mainjiania kwa siri, jambo ambalo linaashilia kwamba wanategengeza silaha na kujiandaa kijeshi.

Mwaka 1907, Uingereza kama taifa, lilikuwa kubwa kama Marekani ya leo. Jeshi lake ndilo lilikuwa na jeshi bora kabisa la majini kuliko taifa lolote lile duniani. Eyre Crowe aliposema kwamba Ujerumani anajiandaa kupambana na Uingereza wengi ndani ya Uingereza walimpuuza na kumdharau sana kwasababu hata kama Ujerumani alikuwa na nguvu asingeweza kupambana na Uingereza.

Rule Britannia, The British Rules the Waves, The Empire The Sun Never Sets na A Charge of the Light Brigade ndizo Propaganda zilizotawala karne za 18, 19 na 20 kuhusu Muingereza. Miaka saba baadaye mwaka 1917, kwenye VITA YA KWANZA YA DUNIA, alochokisema Crowe kilitimia. Ujerumani hakuangahika kutengeneza manowari kubwa za kijeshi (Dreadnoughts) bali alibuni nyambizi (U-Boats) za kisasa na kufanikiwa kuanzisha "Sub-Marine Warfare" kitu ambacho kilikuwa kigeni duniani.

Meli za Uingereza, za Kijeshi na Kibiashara zilizamishwa kwenye bahari ya Atlantiki, Ujerumani alikuwa anaenda kushinda vita, mpaka pale Uingereza alivyosaidiwa na Marekani mwaka 1917. Uingereza alishinda vita lakini safari ya kuporomoka kwa Uchimi ndipo ilipoanza. Sasa hapa nasema nini: IN WAR, the biggest mistake is underestimating your enemy. Najua wengi mtakasirika lakini ukweli ni kwamba Marekani na Israeli walikosea mahesabu yao kama ambavyo walifanya kule Cuba 1962 na Vietnam mwaka 1965.

Hili liliwaponza wengi katika historia ya dunia: Crassus, Pompey, Darius III, Alexander the Great, Napoleon, Hitler na wengine wengi.
==============================================================================

Huyu hapa ni Mkurugenzi mstaafu wa shirika kongwe la Ujasusi duniani, MI6, Sir Alex Young. Amekuwa na uzoefu mkubwa wa kupambana na Iran kwa muda mrefu akiwa mwanajeshi na jasusi wa Uingereza. Anasema dhahiri kwamba Iran walijipanga vizuri kabla ya vita na wameonesha uwezo mkubwa. Ametumia kauli "THE UPPER HAND" kwamba Iran has better advantage than America.

Hapa alikuwa anahojiwa na The Economist. Silazimishi mtu kuamini ninachokisema, sikiliza, chambua kivyako na fanya maamuzi ya unachotaka kuamini.

Ila jambo ambalo huwezi kulipinga ni kwamba WW3 imeshaanza na itachukua muda sana kukubaliana na huu ukweli. WW1 haikuwa WW1 mpaka ilivyofika mwaka 1916 hivi ndiyo ikawa kubwa. WW2 haikuwa WW2 mpaka mwaka 1941 hivi ndiyo wataku kufahamu kwamba wamechelewa. Hii yetu itakuwa ndefu mno na mpaka kuja kusanua mchezo tutakuwa tumechelewa mno:

View: https://www.youtube.com/shorts/ZuKZHERb8_Q?feature=share
 
Times of Israel.jpeg

Upande mwingine Bwana Benjamin Netanyahu analalamika kwamba MOSSAD imemuangusha baada ya kushindwa kutimiza ilichomuahidi kabla ya vita kuanza. Walisema wangesababisha vurugu nchi ikachafuka na utawala ukaanguka, lakini hilo jambo halijatokea bado. Israeli wana nguvu sana, tena sana lakini hapa walizichanga karata zao vibaya mno na yamewakuta.

View attachment 3562275

Hii kitu niliwaambia wadau kwenye uzi ule wa vita wakabeza. Inasadikiwa hii vita ilitakiwa kudumu kwa masaa 48 tu. Baada ya kuuwawa Ayatollah walitarajia yatokee maandamano kama ya Arab spring na utawala wa kiayattolah uangushwe kupitia Cells zao huko Iran. Matokeo yakaja kinyume. Tuombe wamalize kwa amani hii kitu isijeikasambaa duniani kote.
 
Hakuna mtu anependa au kushabikia vita na mauaji ya raia waso na hatia.

Lakini "I am sorry to say", Donald Trump kaamua kuivamia Iran mazima na itakuwa vita itayolazimisha vita ya tatu ya Dunia.

Sote tuombe isitokee hivyo.
 
Tunachoangalia ni facts sio nani kasema

Huwezi niambia Iran wana intelejensia kubwa wakati waziri wao wa Intelejensia kabamizwa pamoja na waziri wa ulinzi na wakuu kibao wa baraza la usalama wa taifa.

Mwenye intelejensia kali tunaona anachofanya, kaweza kumlipua kiongozi mkubwa kwa sekunde 40 tu, kaweza kuingilia mawasiliano na kutrack viongozi, n.k.
 
Huyo akisema wamsikiliza uzuri kwani ana madini ya kutosha.
Israeli alianza kushindwa vita dhidi ya Iran mwaka 2023.

Israeli siku zote iliweza kujitanabaisha kama taifa ambalo linaonewa na kuchukiwa na watu wenye hila dhidi yake. Jambo hili lilifanya taifa la Israeli kuungwa mkono na watu wengi duniani. Binafsi hata mimi Anti-Semitism huwa nadhani ni ukichaa wa akili tu. Lakini walichofanya Gaza kina Netanyahu kimefanya dunia nzima, hata mataifa mengine kusita kumsaidia kwenye hii vita kwa Intelijensia, Diplomasia na Propaganda. Netanyahu na Trump wako peke yao.

Ukiona hadi The New York Times na The Economist wanapinga vita dhidi ya Marekani na Israeli kwa kiwango hiki, basi fahamu fika kuna kitu hakipo sawa kabisa kwenye kambi ya Magharibi. Naamini NATO kuna muda watamuunga mkono Marekani na Israeli lakini itakuwa baadaye sana ambapo nao wenyewe yamewakuta tayari.
 
imemuangusha baada ya kushindwa kutimiza ilichomuahidi kabla ya vita kuanza.
Iran Toka Mwaka jana Hadi sasa imekamata double agents, agents, sympathizers wa Mossad na Israel zaidi ya 700!!! Kwa hiyo, missions za kuleta vurugu ndani ya Iran zimekufa ukizingatia Israel na US waliua watoto wa Iran waliokuwa Shuleni. Nyongeza US na Israel wakamuua Ayatollah na wakajigamba kuwa wamemua. Hili limewaleta Karibu zaidi na kuwa Wamoja wairan.
 
Hii kitu niliwaambia wadau kwenye uzi ule wa vita wakabeza. Inasadikiwa hii vita ilitakiwa kudumu kwa masaa 48 tu. Baada ya kuuwawa Ayatollah walitarajia yatokee maandamano kama ya Arab spring na utawala wa kiayattolah uangushwe kupitia Cells zao huko Iran. Matokeo yakaja kinyume. Tuombe wamalize kwa amani hii kitu isijeikasambaa duniani kote.
Kita nikitaka kufanya maendeleo vita inakuja , naombea vita iishe mapema mzizo usiwe mkubwa na kuenea .
 
Israeli alianza kushindwa vita dhidi ya Iran mwaka 2023.

Israeli siku zote iliweza kujitanabaisha kama taifa ambalo linaonewa na kuchukiwa na watu wenye hila dhidi yake. Jambo hili lilifanya taifa la Israeli kuungwa mkono na watu wengi duniani. Binafsi hata mimi Anti-Semitism huwa nadhani ni ukichaa wa akili tu. Lakini walichofanya Gaza kina Netanyahu kimefanya dunia nzima, hata mataifa mengine kusita kumsaidia kwenye hii vita kwa Intelijensia, Diplomasia na Propaganda. Netanyahu na Trump wako peke yao.

Ukiona hadi The New York Times na The Economist wanapinga vita dhidi ya Marekani na Israeli kwa kiwango hiki, basi fahamu fika kuna kitu hakipo sawa kabisa kwenye kambi ya Magharibi. Naamini NATO kuna muda watamuunga mkono Marekani na Israeli lakini itakuwa baadaye sana ambapo nao wenyewe yamewakuta tayari.
Yes hii ni about Marekani kutawala Dunia na kumzuia China ambae amekuwa (hadi sasa) akifaidi mafuta machafu ya pale kisiwa cha Kharg na Mareani akitaka kisiwa hicho kwa namna yoyote ile.

Si umesikia zile dola bilioni 200 ziloombwana Pentagon?

NATO kwa siri wote wapo wamesogeza meli zao eneo hilo, huku kwa sie public wacheza na Runinga tu na disinformation.

Hichi walokifanya sasa Trump na Marekani wamehisiwa kuwa wamefanya "manipulation" kwenye soko la mafuta duniani (tusisahau Trump ni mfanyabiashara) na wote reps na Dems wote kwenye hili ni wamoja.
 
Iran Toka Mwaka jana Hadi sasa imekamata double agents, agents, sympathizers wa Mossad na Israel zaidi ya 700!!! Kwa hiyo, missions za kuleta vurugu ndani ya Iran zimekufa ukizingatia Israel na US waliua watoto wa Iran waliokuwa Shuleni. Nyongeza US na Israel wakamuua Ayatollah na wakajigamba kuwa wamemua. Hili limewaleta Karibu zaidi na kuwa Wamoja wairan.
Na kwa nyongeza Iran kwa sasa hakuna Internet (WAN) bali kuna intranet (local LAN), hivyo raia wameruhusiwa kutumia intranet ndani ya Iran na mawasiliano yapo kama kawaida isipokuwa hawana mawasiliano na nje ya Iran.

Pili, baada ya yale mauaji ya mwanzo ya raia na waandamanaji raia wameingia woga mkuu hivyo kushindwa kufanya kampeni yoyote ile ya kuandamana.

Tatu, vile vikosi vya ki-Kurd kule kaskazini vilipewa msaada na CIA ili walianzishe nao wote walishughulikiwa na vikosi vya Iran (Proxies) kulekule kabla hata hawajaanza mambo yao.

Ndo maana waona hali iliyopo kwa sasa.
 
Tunachoangalia ni facts sio nani kasema

Huwezi niambia Iran wana intelejensia kubwa wakati waziri wao wa Intelejensia kabamizwa pamoja na waziri wa ulinzi na wakuu kibao wa baraza la usalama wa taifa.

Mwenye intelejensia kali tunaona anachofanya, kaweza kumlipua kiongozi mkubwa kwa sekunde 40 tu, kaweza kuingilia mawasiliano na kutrack viongozi, n.k.
Unahisi hao wazee wa miaka 86 hata wanajua AI na GPS coordinates ni nini? Kama unaamini vita vinapiganwa na hao wanasiasa then Iran Hana kitu, ila uhalisia haupo hivyo.

Handala Kundi la Iran la hii vita wanadukua Israel kama hawana Akili vizuri, mpaka ukiona Netanyahu anabandika Gundi kwenye simu anaelewa wanachofanya, mpaka ukiona Taa za barabarani zinatolewa Israel wao wanaelewa wanachofanya.

Juzi Dimona kumepigwa hakujalia Ving'ora wala missile Ku intercept Handala wame claim udukuzi huo wamefanya wao.

Angalia hata picha za Satellite base za Marekani zilivyopigwa, ni mpuuzi pekee atasema hawa watu walikua hawana intelligence.
images (1) (11).jpeg

Unaona Radar hizo zimekuwa precisely attacked, MTU yupo Iran pengine maisha yake yote hata nje ya Iran haijawahi kutoka, anabonyeza Tu kitufe missile inaenda exactly kupiga sehemu Fulani tena kisehemu kidogo Tu kama dishi la Mita kadhaa kinateketezwa. Unahisi hii sio intelligence?
 
View attachment 3562275
Upande mwingine Bwana Benjamin Netanyahu analalamika kwamba MOSSAD imemuangusha baada ya kushindwa kutimiza ilichomuahidi kabla ya vita kuanza. Walisema wangesababisha vurugu nchi ikachafuka na utawala ukaanguka, lakini hilo jambo halijatokea bado. Israeli wana nguvu sana, tena sana lakini hapa walizichanga karata zao vibaya mno na yamewakuta.

Nyau awapeleke hao MOSSAD wakaandane kwa niaba ya wananchi wa Iran, ili wakichafue.. Huyu jamaa na Trump wamekuwa kama wehu
 
Na kwa nyongeza Iran kwa sasa hakuna Internet (WAN) bali kuna intranet (local LAN), hivyo raia wameruhusiw kutumia intrant ndani ya Iran na mawasiliano yapo kama kawaida isipokuwa hawana mawasiliano na nje ya Iran.

Pili, baada ya yale mauaji ya mwanzo ya raia na waandamanaji raia wameingia uwoga mkuu hivyo kushindwa kufanya kampeni yoyote ile ya kuandamana.

Tatu, vile vikosi vya ki-Kurd kule kaskazini vilipewa msaada na CIA ili walianzishe nao wote walishughulikiwa na vikosi vya Iran (Proxies) kulekule kabla hata hawajaanza mambo yao.

Ndo maana waona hali iliyopo kwa sasa.
Kuongezea mkuu Wakurdi wa Iran wamekataa, wamesema wao sio mercenary, wamesalitiwa na USA before na hawatakubali now.

Waliopigwa ni Wakurdi wa Iraq ambao wengi wanaishi kambi za USA.
 
Unahisi hao wazee wa miaka 86 hata wanajua AI na GPS coordinates ni nini? Kama unaamini vita vinapiganwa na hao wanasiasa then Iran Hana kitu, ila uhalisia haupo hivyo.

Handala Kundi la Iran la hii vita wanadukua Israel kama hawana Akili vizuri, mpaka ukiona Netanyahu anabandika Gundi kwenye simu anaelewa wanachofanya, mpaka ukiona Taa za barabarani zinatolewa Israel wao wanaelewa wanachofanya.

Juzi Dimona kumepigwa hakujalia Ving'ora wala missile Ku intercept Handala wame claim udukuzi huo wamefanya wao.

Angalia hata picha za Satellite base za Marekani zilivyopigwa, ni mpuuzi pekee atasema hawa watu walikua hawana intelligence.
View attachment 3562288
Unaona Radar hizo zimekuwa precisely attacked, MTU yupo Iran pengine maisha yake yote hata nje ya Iran haijawahi kutoka, anabonyeza Tu kitufe missile inaenda exactly kupiga sehemu Fulani tena kisehemu kidogo Tu kama dishi la Mita kadhaa kinateketezwa. Unahisi hii sio intelligence?
Makombora karibu 92% ya Iran yanazuiwa na mifumo kama Iron Dome, lakini Iran yenyewe haiwezi kuzuia hata shambulio moja, unaona tofauti au bado?

Hao Handala hawafikii popote mbele ya Israel waliomdukua Ayatollah akiwa anatumia kitochi na wakambamiza ndani ya sekunde 40 tu.

Hilo eneo lililopigwa ni miongoni mwa machache ambayo makombora yaliweza kupenya. Sasa linganisha na Israel, akiamua kulenga target yoyote ndani ya Iran, kuna kizuizi ?

Iran anarusha makombora kwa wingi, Israel anaingia mpaka Tehran na kupiga anapotaka, anamfuata adui sebuleni kwake kabisa sio kumshambulia kwa mbali.

Na hadi leo Iran wanahangaika kupata intel ya kulipiza kisasi kwa viongozi wakubwa wa Israel, wakati Israel anafanya operation ndani ya sekunde chache na anarudia mara kwa mara. Iran walichoweza ni kutumia AI kutengeneza video kuwafariji watu kama wewe eti wamemuua Neta

Hiyo ndiyo intelligence, si kelele, ni matokeo.
 
Back
Top Bottom