Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Niko hapa morogoro ktk moja ya hotel zinazosifika. Ninachokiona bado rais Magufuli hajapata watu wanaostahili kumsaidia ktk uongozi. Kuna watu hawa wanaojiita ni wakurugenzi, mainjinia wa maji. Watu hawa wanatia aibu takribani miji yote isipokuwa Tanga.
Hapa morogoro hakuna maji. Kisingizio cha mkurugenzi wa MORUWASA eti maji hayatoshi kwa wakazi wa mji huu lakini ajabu ni kwamba kuna magari yanasomba maji toka huko huko MORUWASA na kuyaleta mahotelini na majumbani. Hali hii haikubaliki na ni aibu kuendelea kuwa na wakurugenzi wa aina hii. yasemekana magari haya ni miradi yao waajiliwa wa MORUWASA!
Nasikitika sana kuona suti ninayovaa na kujiita mgeni ndani ya hotel, naishia kuoga maji ya ndoo na vikopo. Kule kwangu Dar, tunaoga maji ya chumvi yaliyochimbwa na mahoteli, labda huko idadi ni kubwa, iweje kamji kama haka nako ni tatizo?