Mkurugenzi mkazi UNDP aleta heri Same

Mkurugenzi mkazi UNDP aleta heri Same

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
MKURUGENZI MKAZI UNDP ALETA HERI SAME

[emoji172]Mkurugenzi mkazi wa UNDP Bi Natalie BOUCLY atembelea Wilaya ya Same kwa siku mbili.
Akagua miradi iliyofadhiliwa na UNDP kupitia shirika la SIPRO na TFS.
[emoji172]Akabidhi majengo 4 yaliyojengwa kupitia mradi wa Kuboresha usimamizi wa Misitu ya Mazingira Asilia na kukuza utalii kwa ufadhili wa UNDP kwa TFS. Majengo yamejumuisha ofisi ya msitu wa Chome na ofisi 3 (ranger outposts) kwa ajili ya usimamizi wa msitu katika kata ya Chome, Bwambo na Bombo.
Mradi huo pia umejenga majengo kama hayo ktk misitu sita nchini ambayo ni Minziro, Uzdungwa, Mt Rungwe, Magamba, na Mkingu. Jumla ofisi 6 na Ranger posts 15.
Miradi 8 iliyofanywa na SIPRO ya kilimo, mifugo, mazingira, barabara.
[emoji172]Atembelea mradi wa ujenzi wa Daraja Heikapombe kata ya Makanya Na mradi wa jengo la kijiji cha Mhero kata ya Chome.
[emoji172]Aahidi kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Same kulinda na kuhifadhi msitu wa Chome pamoja na raslimali zake.
[emoji172]Afurahishwa sana na mpango mkakati wa Wilaya wa kuhifadhi mazingira pamoja na kuimarisha Utalii.
Aahidi kushirikiana na Wilaya kutekeleza mikakati hiyo, kwani yote itasaidia kuwa na uhakika wa usalama wa hifadhi ya Chome/ Shengena.
[emoji172]Afurahishwa na mpango wa kupanda kilele cha Shengena, aahidi kushiriki siku hiyo.
Aahidi kuwakutanisha viongozi wa Wilaya na balozi zinazojihusisha na mazingira na utalii.
[emoji172]Naye Mtendaji Mkuu wa TFS Prof. Dos Santos Silayo aliyeambatana naye aahidi kuendelea kuimarisha utalii katika hifadhi ya Chome kama ilivyo kipaumbele cha serikali katika hifadhi zote za misitu nchini.
[emoji172]DC Same Mh. Rosemary Senyamule, atoa shukrani kwa UNDP na kuwaahidi usimamizi makini wa fedha zote zinazotolewa.
Awakumbusha TFS kuongeza tija kwa miradi inayotolewa kwa wananchi wa vijiji 27 vinavyozunguka msitu wa TFS kama mbadala sahihi na kuongeza utayari wa wananchi kulinda msitu huo.
" Nategemea tukiimarisha utalii kwenye eneo la Shengena, tutawashirikisha wananchi wengi wawe sehemu ya utalii huo. Wakiona tija ya utalii, wataulinda msitu wetu ambao ni kama moyo wa Wilaya ya Same" . Alisema DC Huyo.

Ziara ya viongozi hao ilifanyika Tar. 20 na 21 Aug. 2018. Ambapo pia walikuwepo wawakilishi toka wizara ya Fedha na TAMISEMI .

" Same is not the same"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vip tuliambiwa tutakuwa donor vip mbona misaada inazidi kumwagika au zile zilikuwa ni raha za punyeto?
 
Back
Top Bottom