Mkurugenzi gaming board atabadilishwa lini?

Mkurugenzi gaming board atabadilishwa lini?

hotstoryg

Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
18
Reaction score
13
Kwa kweli tangia board ya michezo ya bahati nasibu inaanzishwa, Mkurugenzi ni huyo huyo Abbas Tarimba! Je, ni kweli ndio mtu pekee kati ya Watanzania wote ndio anaweza kusimamia Gaming Board?

Je, unyonyaji mkubwa unaofanywa na wamiliki wa casino kwa Watanzania kwa kutowapa mikataba wafanyakazi kwa zaidi ya miaka miwili kazini ni sawa? (mfano ni PRINCESS CASINO).

Je, wafanyakazi wa Kizungu wanaokuja kufanya kazi ambazo Watanzania wenzetu wanaweza na wao kulipwa pesa nyingi tofauti na wazawa ni sawa? (mfano ni LEGRAND CASINO).

Je, ni kwa nini ukaguzi wa machine zinazotumika huwa haufanywi kulinganisha na Casino za nchi nyingine ambazo huwa zinafanyiwa ukaguzi mara kwa mara?

Tunamuomba rais mteule aangali upande huu kwani ni kodi nyingi sana zinapotea na Watanzania wengi sana wananyanyasika sana kwa hawa waajiri wa Kizungu wanaomiliki hizi casino.
 
Duh huyo Tarimba kweli amekaa hapo,nimemsikia tangu 1996 mpaka sasa kuwa ni Mkurugenzi wa Gaming Board.
 
Back
Top Bottom