Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,176
- 1,939
Habari wakuu
Ni matumaini yangu sote tu wazima wa afya, ila moyo wangu umejawa na masikitiko kutokana na yale yanayoendelea nchini hasa katika sakata la "nyeti".
Sipendi kuwa mwamuzi wa kusema vitendo hivi vipo au havipo kwa sababu ninaamini ulimwengu huu una mambo mengi ambayo mengine yapo mbali na ufahamu wangu, ila kilichonisikiitisha ni jinsi gani jamii yetu ya Kitanzania inaonesha watu walio wengi kutokuwa na ufahamu wa taratibu za kisheria hata zile ambazo ni za msingi kabisa.
Kuna jitihada zinahitajika sana katika kujenga jamii yenye kutambua kuwa kuna sheria na zinahitaji kufuatwa. Hebu fikiria kuwa kwenye jamii ambayo haijui kwamba mkimkamata mtu ambaye ametenda uhalifu mnatakiwa kufanya nini, badala yake ni kuchukua sheria mkononi.
Lakini mimi nimewaza sana kwanini jamii hii yetu ya Watanzania tuliosifika kwa uungwana tumefikia hapa. Ninachokiona mimi ni kwamba kuna sehemu tumepasahau na kutupilia mbali hasa kwenye mafunzo ya ngazi ya familia. Wenzangu "Millenials" wanakumbuka jinsi mafunzo yalivyokuwa katika ngazi za familia.
Ukitazama wengi katika hao wanaochukua sheria mkononi ni vijana walio katika kundi la generation z lakini ni product ya Millenials. Millenials hakuna cha kukwepa hapa tumeshindwa kurithisha tulicholithishwa.
Jambo jingine nililoliona ni kwamba sasa watu kuishi pasipo kujua mipaka ya kisheria. Imekuwa ni "rule of the jungle, the fittest will survive". Kwanini hii inatokea? Ni kwa savabu tumeanza kujenga jamii ambayo haijui uwepo wa sheria. Mfano mdogo, kama mwananchi ameachwa ajifanyie anavyotaka yeye kama vile kupanga biashara hata barabarani na sehemu za waenda kwa miguu na hajaoneshwa kwamba hapa umevunja sheria, unategemea atakuwa "sensitive" na hizo sheria?
Kama mwananchi anamuona kiongozi wake anavunja sheria na hakuna matokeo yoyote, yeye atakuwa na sense ya hizo sheria? Tujisahihishe wote kama jamii, tumeanza kukengeuka na kwenda vibaya kabla matokeo hayajawa mabaya zaidi.
Jambo la mwisho nililoliona ni tatuzo la kisaikolojia "mob Psychology". Mnakumbuka wale tuliosoma enzi hizo shule za boarding za serikali? Migomo ya kula maharage ilisababisha hadi kuchomwa shule? It was mob psychology, kwa mtu mmoja mmoja asingeweza kufanya hivyo. Kwa mazingira ya sasa ya utafutaji kuna vijiwe vya watu wengi kama vile bodaboda na kadhalika, sasa mob psychology inatawala.
Kuishinda hii inahitaji elimu mtambuka kwa makundi yanayokaa pamoja kwa muda mrefu. Lakini sasa hapa pia ninawaza tutaishinda je saikolojia hii ambayo pia inaweza kupatika kwa kiasi kikubwa katika makundi mitandaoni?
"My take" sisi kama jamii tujitafakari, tunakoelekea siyo kuzuri kabisa.
Soma pia

- Mtu anayedaiwa akigusa nyeti zako zinapotea azua taharuki Tunduma
- Kimara: Polisi walingilia kati kumuokoa aliyepigwa na Wananchi kwa kudaiwa kupoteza nyeti za mtu Mwanaume mmoja
- Muliro: Aliyedai kuchukuliwa Nyeti Kimara ni muongo
- SACP Augustino Senga: Wanaodai Nyeti zao zimepotea Tunduma Madaktari wamethibitisha zipo
- Chalamila: Tangu nisikie ukishikwa bega nyeti zinapotea nimekuwa makini, sina mali nyingine