Mkurugenzi asomewa shtaka la mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi asomewa shtaka la mauaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ehud, Apr 19, 2011.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi wa Hoteli ya Kitalii ya South Beach ya jijini Dar es Salaam, Salim Nathoo maarufu kwa jina la Chipata (53), amepandishwa kizimbani akikabiliwa na kesi ya mauaji ya kumchoma moto kijana aliyeingia kwenye hoteli yake bila kibali.

  Nathoo, mkazi wa Mikocheni A alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Temeke, Khasim Mkwawa, jana akiwa pamoja na mshitakiwa mwenzake John Mwangiombo (32), kujibu tuhuma za mauaji.

  Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi Dastan Kombe aliiambia Mahakama hiyo kuwa Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 6.30 usiku eneo la Mjimwema Kigamboni, washitakiwa walishirikiana kumpiga na kumchoma moto Lila Hussen (34) na kumsababishia kifo.

  Hata hivyo, Hakimu Mkwawa aliwataka washtakiwa wote kutojibu shtaka hilo kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu kwa kutajwa tena.

  Hata hivyo, ndugu wa marehemu Lila hawakufika mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wanashughulikia utaratibu wa mazishi wa ndugu yao.

  Inadaiwa alichomwa moto na washtakiwa baada ya kuingia hotelini hapo kwa ajili ya kuwatafuta wageni wake, ambapo washtakiwa hao walimwagia mafuta na kumvisha tairi na baadaye kumuwasha kwa kibiriti.

  Hata hivyo, marehemu kabla ya kifo chake alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  Akithibitisha kifo hicho, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Devid Misime, alisema Lila alifariki usiku wa kuamkia juzi hospitalini hapo baada ya juhudi za madaktari kuokoa maisha yake kushindikana.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  akaozee jela 53+35=88yrs
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Chipata hana shauri la kujibu.
   
 4. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 341
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  RIP Lila
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Hivi ukiangalia mtiririko wa tukio majibu kamili hayaji kichwani
  Marehemu Lila aliingiaje kama hakulipa
  katika umati wa watu mle ndani waligunduaje hana band mkononi?
  Alipokamatwa na kuamriwa achomwe moto ni nani alietoa amri hiyo?
  Petrol ilinunuliwa saa ngapi?
  NANI ALIYETEKELEZA KITENDI CHA KUWASHA KIBERITI NA KUMCHOMA BINADAMU MWENZIE?
  HIVI KUITWA BOUNCER KUNA QUALIFICATION GANI? Au ndo yale mambo ya tegeta?
   
 6. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  GAMA

  Kwa nini comments zako kuhusu mauaji ya huyu mlala hoi mtanzania ni za kishetani? Au una mkono wako katika mauaji haya? Ulishabikia kuchomwa moto na leo uanaandika upuuzi tena. Ni haki yako kutoa maoni lakini sio kuchangia ujinga kwenye jukwaa la wenye akili. Samahani kama nimekuudhi ila nadhani ni stahili yako.

  Kama huna la kuchangia, soma uondoke. Usilete mzaha kwenye masuala nyeti hasa uhai wa mtu.   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  kma akawaida polisi wamekurupuka ..huyu mhindi hana kesi ya kujibu mtaona
   
 8. M

  Mwera JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbw* huyo wakihindi nahuyo mtumwa wake wote wakipatikana nahatia wanastahili kunyongwa mpk kufa kwa mujibu wa sheria za tanzania,hakuna kifungo hapo nikitanzi tu kwamujibu washeria,alieua kwa upanga nae atauawa kwa upanga.
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu Tanzania kila kitu kama hakiathiri masilahi ya watawala kinaachwa kiende naturally, hakuna measures za kuprotect Public. Katika nchi zinazojali usalama wa raia(Public safety) kila eneo linakuwa na sheria za kuhakikisha usalama wa raia first. Mfano hiyo kazi ya Ubaunsa bongo wenzetu wanaita Door Supervisors ambao hupewa leseni na wizara husika baada ya kuhudhuria masomo ya kujua sheria mipaka ya kazi na jinsi ya kukabiliana na watu wenye different levels of intoxications, wanapewa mtihani na ukifaulu unapewa leseni ya miaka mitatu kwa kulipa ada, mtu yeyote anayefanya kazi bila kibali faini yake mpaka milioni tatu na mwebye hoteli/bar anafungiwa leseni na faini juu.

  Unakuta kazi baunsa si kupiga watu bali ni kuelekeza na kuwasiliana police muda wowote kunapokuwa na tafrani, sisi kwetu baunsa kazi yake ni kutoa kibano matokeo yake ndiyo haya ya kujiona wapo kwe jungle, struggle fo existence survival for the fittest.
   
 10. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  inasikitisha sana , kweli hawa jamaa wakaozee jela.
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena...nadhani suala la mabouncer liangaliwe upya sio mtu ili mradi ana kifua kikubwa na kichwani box basi anaachiwa kufanya atakavyo,naamini pamoja na amri ya huyo mdosi lakini mabouncer wangekuwa fit upstairs na kufahamu sheria na wajibu wao wasingetekeleza unyama ule
  sanasana wangetumia misuli yao kumdhibiti boss wao mdosi aliyepanic
   
 12. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  at list roho yangu imetulia!!!

  nilitoa machozi baada ya kusoma habari ya Lila na alivyochomwa kikatili kwa kuvishwa tairi na kuwashwa moto

  nawachukia wahindi sana, niliwahi kufanya kazi nao wananyanyasa sanaaa!!!

  Akaozee jela!!!

  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
   
Loading...