Mkurugenzi apinga uamuzi wa madiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi apinga uamuzi wa madiwani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro limepitisha uamuzi wa kuwalipia ada wanafunzi 8,528 wa shule za sekondari za kata katika manispaa hiyo.

  Uamuzi huo uliopitishwa juzi na baraza hilo linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), umepingwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Bernadette Kinabo.

  Kinabo amelitaka Baraza la Madiwani kutekeleza sera za maendeleo za Serikali iliyopo madarakani katika miradi ya elimu akisema badala ya halmashauri hiyo kuwasomesha wanafunzi hao, ni bora fedha hizo zikaelekezwa kwenye utekelezaji wa sera za Serikali kwa kujenga maabara na maktaba katika shule zinazotarajiwa kuanzishwa kidato cha tano na sita mwaka huu.

  Katika kikao maalumu cha kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2011/12 kilichofanyika juzi mjini Moshi, Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhari Michael alisema kila mwanafunzi anahitajika kulipiwa ada ya Sh 20,000 kwa mwaka mmoja hali ambayo itafanya jumla ya Sh milioni 170 kutumika kwa ajili hiyo.

  Michael ambaye ni Diwani wa Kata ya Bomambuzi (Chadema), alisema licha ya kuwajibika kulipa ada, wazazi wengi wanakabiliwa na changamoto ya kuchelewesha kulipa michango ya zaidi ya Sh 240,000 kwa ajili ya chakula, mishahara, walinzi na wapishi.

  Alisema wamefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh milioni 351 kutoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato ya halmashauri hiyo na kwamba sehemu ya fedha hizo zitatumika kuwalipia ada wanafunzi wote.

  Alisema, zitatumika pia kuongeza vyoo katika baadhi ya shule za sekondari zinazokabiliwa na upungufu wa vyoo.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri katika kupinga uamuzi huo, alisema, “Halmashauri inakabiliwa na upungufu wa milioni 136/- katika bajeti yake ya elimu ya sekondari.

  Ni bora Baraza hili likaelekeza matumizi ya fedha hizo katika kutekeleza sera ya elimu ikiwa ndio sera ya Serikali iliyopo madarakani ”.

  Kinabo alisema, wakati Serikali inawalipia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, kwa wanafunzi ambao wazazi wao wana uwezo , ni bora wakabeba jukumu wenyewe kuwasomesha.
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Serikali iliyo madarakani ndiyo hiyo iliyoamua kuwalipia karo hao watoto, serikali ipi huyo mkurugenzi anayoisema?

  Huu ni ushahidi tosha kuwa viongozi watendaji wa local governments wawe wanawajibika kwa madiwani waliochaguliwa. Kuwa na serikali za majimbo sio kuletewa kina Kinabo waliowekwa kutetea ufisadi.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Big up sana madiwani wa chadema kumbe hata hapa bongo tunaweza kujenga nchi yenye kuwapa wenyenchi huduma muhimu kama ilivyokuwa Libya ya Gadafi. Tatizo la hawa makada wa ccm na viongozi wao ni maamuma wasioambilika! Namwomba Mungu aniache niwe hai hadi niione siku wenyenchi tutakapoi-dissolve CCM kama kilivyofanyiwa kile chama cha Mubaraka wa Misri au kile cha Ben Ali wa Tunisia!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Anataka wajenge vyoo na maabara ili apate 10% toka kwa mkandarasi,si kwamba ana uchungu na wananchi.si mnakumbuka bagamoyo vyoo vilijengwa kwa bilions of money!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  moto ameusoma huyo choko kinabo na akuna rangi asiyoiona mbaya zaidi kuna vichwa vya malawyer umo ndani ndio amechanganyikiwa anajuta kuwa mkurugenzi aombe aendele loliondo akale buku 3 za magari ajui moshi kumechafuka aibiwi mtu watu wanataka pesa ifanye kazi
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaaaaaaaa kweli inabidi hawa wazee wasome alama za nyakati na wabadilike unajua serikali ndio inayotakiwa kujenga shule na vyoo na sio halmashauri wala wazazi hiyo pesa itatoka tu kwa ada watakewasitake!
   
 7. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Jana niliona kipindi Star TV kikieleza mgongano wa kimawazo kati ya madiwani wa CHADEMA na CCM pamoja na mkurugenzi wa hii halmashauri. Sakata lenyewe ni juu ya kutaifishwa kwa jengo la Halmashauri linalotumiwa na CCM, kilichonisikitisha ni jinsi ambavyo huyu mama anaonekana kutokuwa na nia ya dhati kuwa na ushirikiano na Meya pamoja na madiwani wa CHADEMA kwa madai ya kwamba hawajui sheria wanahitaji kujifunza zaidi. Nilimsikia mwenyekiti wa madiwani wa CCM akiwabeza madiwani wa CHADEMA kwamba wengi wao ni hawana elimu ya kutosha akidai wengine wameishia darasa la saba. Wananchi wamewaamini hao madiwani wasiokuwa na elimu, waache wawatumikie wananchi. Mkurugenzi hataki suala hilo kujadiliwa katika baraza, lakini madiwani wanataka lijadiliwe japokuwa lipo mahakamani. Wanadai ni vyema wakatambua mwanasheria wa halmashauri atakwenda kuzungumza nini mahakamani.
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hatoki mtu hapo kwani CHADEMA wengi ni malawyer wacha wapoteze muda wao mahakamani!labda mahakama nayo isitende haki!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Point of order,

  Madiwani wanachaguliwa na wanachi na wanaongoza wananchi ambao wamewachagua.

  Mkurugenzi anateuliwa na raisi kufanya kazi za kiutendaji katika manispaa, miji, nk

  Inakuwaje Mkurugenzi ambaye hawakilishi wananchi anaamua kutengua uamuzi wa madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi?

  Matumizi ya manispaa yanatokana na kodi inayolipwa na wananchi kwa njia moja au nyingine na hailipwi na mkurugenzi, inakuwaje mtu mwingine aje kuwapangia matumizi ya hela zao kinyume cha matakwa yao kama yanavyowakilishwa na wawakilishi wao?

  Je katika hali kama hiyo wananchi wanaweza kufanya nini kutetea maslahi yao?
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hili mkurugenzi inaelekea ameamua tu au kujipendekeza kwa mwajiri wake ambaye ni serikali ya CCM, au anataka kuonyesha ukereketwa wake kwa chama hicho. Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba kulipia wanafunzi karo hakujapingana kwa hali yeyote ile na ilani ya CCM, na hata hivyo baraza la madiwani ndilo lenye kauli ya mwisho kwenye masuala ya kisera.
   
Loading...