Mkumbushe mwanao kuwa...

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Endelea kumwambia mwanao kuwa ile kauli isemayo 'tone moja la ubaya huchafua bahari ya wema' ni ya ukweli na pekee aiamini asilimia 100. Akikuuliza kwanini?

Mwambie amtazame vizuri Golikipa katika mchezo wa mpira wa miguu, bila kujali ataokoa hatari ngapi, bila kujali atacheza kwa juhudi kiasi gani ila mwishoni mashabiki watamlaumu kwa goli moja alilofungwa.

Asipokuelewa usimshangae, yawezekana akili yake bado haijapevuka hivyo mfafanulie kuwa, ana uwezo wa kutenda mema kwa moyo wake wote mbele ya wanadamu, lakini siku akija kukosea kitu kimoja basi watasahau yote aliyowahi kuwatendea hapo awali.

Tafadhali usisahau kumwambia kuwa, aache majivuno na kujiona fahari katika mgongo wa dunia hii, maana bila kujali Mungu kaumbaje viumbe wake, ila kila kiumbe kina kikomo chake. Eeh! Ndio maana tunazaliwa tuna miguu miwili, lakini hatuwezi kukwea miti miwili kwa wakati mmoja.

Najua hii hatoilewa vizuri, wala usiwe na shaka. Mueleze tu taratibu kuwa, Mungu katuumba na uwezo wa tofauti kwa kila kiumbe ila lazima kuwe na kikomo chetu, na ndio maana hata kinyonga ana rangi ya kumfanya ahimili kila mazingira, lakini siku msitu ukiwaka moto kinyonga lazima ataungua maana hana rangi ya kumfanya ahimili moto.

Akiwa bado anawaza hilo, we endelea kumhusia kuwa, awe na shukrani na roho ya kuridhika kwa kila kidogo apatacho. Yaani hata kama ana kiu yenye kuhitaji lita nzima ya maji, ila kila apatapo tone moja ni lazima ashukuru maana wapo tayari waliokufa kwa kiu.

Mwambie mwanao kuwa asipende kubishana na wanadamu kwa kila kitu, kwani maisha si mtihani wa mashindano. Msihi tu, saa nyingine kuna faida kubwa kwenye kujishusha kuliko kujaribu kushindana kwa kila kitu. Akikuuliza kivipi? Muache na hii kauli kuwa; "Nyani aokotapo jiwe akamrushia, kisha na yeye akaliokota kumrudishia wote wanaonekana manyani."

Ahsante kwa kusoma, naitwa Amani Dimile

#amanidimile
#misemo_ya_hekima
#fikrazadimile

To be continued...
 
Hapo utakuwa umemfanya mwanao kuwa 'mnyonge'.

Dunia ya aina hiyo imeshapita, ni lazima mtoto awe 'aggressive' ili aweze kwenda na ulimwengu wa sasa.
Akikimbizana na kuwaridhisha walimwengu atakuwa anapaka upepo rangi.
 
A very high wisdom, nimeicopy na kuitunza hii. Asante sana🙏
 
Hiyo point yako ya mwisho imenifariji kidogo juzi kuna dada mmoja ni wakala wa m pesa nilienda kutoa pesa akasema muamala hajauona na hali ya kuwa mimi huku pesa imetoka na meseji inaonekana yaani toka juzi nilikuwa napanga mikakati ya kumfanyia kitu kibaya
 
Hiyo point yako ya mwisho imenifariji kidogo juzi kuna dada mmoja ni wakala wa m pesa nilienda kutoa pesa akasema muamala hajauona na hali ya kuwa mimi huku pesa imetoka na meseji inaonekana yaani toka juzi nilikuwa napanga mikakati ya kumfanyia kitu kibaya
Dunia ni njema lakin haina mwema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom