Mkumbushe mwanao kabla ya 2024

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,412
*
x.jpeg

1. Mkumbushe mwanao kuwa WIVU utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake.

2. Mkumbushe Mwanao kuwa Msaada sio Haki yake asipopewa Asinung'unike atafute Chake.

3. Mkumbushe Mwanao kuwa Tumeona mazuri kwa watu waliokuwa wakiitwa wabaya na Tumeona mabaya kwa watu waliokuwa wakiitwa wazuri kwahiyo Aishi na kila mtu kwa akili.

4. Mkumbushe Mwanao kuwa a-Date na Mtu ambae atampush kutimiza malengo yake Kwa Umri wake sio wa kushangilia kupostiwa Mitandaoni au kuwekwa Profile Picture whatsapp, Facebook na insta.

5. Mkumbushe Mwanao kuwa Tunakosa Usingizi ili wanaotutegemea wapate kulala Vizuri.

6. Mkumbushe Mwanao kuwa Akiwa baba hata akiumwa hatotamani watoto wajue maana tumaini lao pekee ni yeye.

7. Mkumbushe Mwanao kuwa Kilicho bora kwake hakiwezi kuwa bora kwa watu wengine.

8. Mkumbushe Mwanao kuwa alipoamka leo kuna Mwenzake amevuta Pumzi ya Mwisho, inabidi amshukuru Mungu kwa hii zawadi ya Siku Nyingine.

9. Mkumbushe Mwanao kuwa Njia yake ikishanyooka asithubutu kuwanyooshea vidole ambao Njia zao bado zina KONA.

10. Mkumbushe Mwanao kuwa Mtu atakae mpatia Bega wakati analia basi Asimsahau wakati amenyamaza.

11. Mkumbushe Mwanao kuwa Wengine hatuna Mtu wa kumtegemea au Ndugu wa kumlilia Shida, Ukimtoa MUNGU Tunaamini sana kwenye Nguvu, Juhudi na Maarifa Yetu. ZAIDI Aishi Vizuri na Watu ila asijipe umuhimu kwenye maisha ya WATU
#Shukuru Mungu kwa kila Pumzi.
 
Back
Top Bottom