Mkulu kwa hili ni msanii

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
RAIS Jakaya Kikwete ameeleza kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa mashirika ya reli kwa njia ya ubia katika Afrika Mashariki na kutaka uangaliwe kwa kina.

Akifungua jana kongamano la kujadili Mpango Kabambe wa Reli katika Jumuiya ya Mashariki, Rais aliwataka washiriki wa kongamano hilo kujadili hali hiyo kwa uwazi.

“Naelewa sisi sote tumepitia katika hali ngumu kwenye usimamizi wa reli zetu chini ya mfumo uliopo… ninakuombeni kwa dhati, ujasiri na uwazi, mlijadili suala hili kwa kina,” alisema Rais.

Aliwataka kuchambua uwezo na udhaifu wa pande mbili za ubia kwa maana ya Serikali kwa upande mmoja na wawekezaji kwa upande mwingine ili kuona jinsi zilivyochangia kusababisha matatizo yaliyopo.

“Mtakuwa mmefanya jambo lenye tija na haki kwa serikali na watu wa eneo letu hili, kama mtakuja na mikakati na mapendekezo ya kufufua na kuimarisha ubia huu.

“Ninadhani kama suluhisho imara na endelevu halitapatikana mapema, hata mikakati ya maendeleo kwa ajili ya reli zetu itakuwa ni kazi bure,” aliongeza. Alisema anataka kuona mtandao wa reli unakuwa katika hali nzuri hasa katika muktadha huu ambao nchi wanachama wa Afrika Mashariki zimeamua kuwa na soko la pamoja.

“Tunahitaji kuimarisha mawasiliano na kuunganisha reli zetu ili kujenga fursa muafaka na ufanisi katika kushirikiana kwenye matumizi ya vifaa na zana, kuvuna raslimali na kulitumia soko la pamoja. Muda hautusubiri katika hili,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo, Rais alisema ukosefu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika sekta ya reli ni eneo lingine linalotia shaka na kwamba muda umefika kwa Serikali za eneo hili kutumia sekta hiyo kikamilifu katika uwekezaji.

“Mahitaji ya uwekezaji mtaji katika kuimarisha reli katika Afrika Mashariki ni takriban dola bilioni 20 za Marekani … kiasi hiki cha fedha hakiwezi kupatikana kutoka serikali zetu pekee … sekta binafsi ina uwezo wa kuziba pengo kama utawekwa utaratibu mzuri wa malipo,” alisema.

Alishauri kuwapo mpango mahsusi wa kuimarisha taasisi za kifedha za Afrika Mashariki akitolea mfano wa Masoko ya Mitaji na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) kama vyombo vitakavyosaidia kuhamasisha uchangiaji wa maendeleo ya reli Afrika Mashariki.

“Naelewa siku chache zijazo, Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki watajadili mpango wa sera ya kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Afrika Mashariki wenye lengo la kuanzisha miradi ya maendele.
Source: Habarileo

Maoni Yangu: amekuwa rais muda wote rites wakiwatesa wafanyakazi na anazo habari zote za mkataba. sasa hii habari anamdanganya nani. Tutasikia mengi hadi october.
 
alisema hatma ya trl ni alhamisi.
je hiyo speech yake ndiyo imetangaza hatma ya TRL?
Baba mtu mzima tena rais anapodanganya unadhani atapata ushindi halali kweli??
najua TISS watashiriki mchezo mchafu wa ccm kubakia madarakani....
 
Back
Top Bottom