simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,785
- 9,719
mkuu Invisible siwaamini sana hawa TAKUKURU CCM! acha tusubiri!
Hii kweli wenyewe wanahitaji kuchunguzwa sababu za kushindwa kukamata mafisadi wa EPA.Takukuru is Toothless hata miba ya Samaki hawawezi kuivunja wataweza hiyo Mifupa ya Ng'ombe.
Takukuru wenyewe wala Rushwa hawana lolote hapo ni Changa la macho wa Watanzania
mkuu Invisible, kichwa cha habari kingesomeka "takukuru kuwasafisha Mkulo, Maige na Ngeleja"
habari ingenoga!!!!!!!
Nasubiri kwa hamu kuona mwisho wa hiyo sinema mpya in town kwa hisani ya CCM. Uliwahi kuona wapi mtuhumiwa wa wizi kwa mali za umma akiandikiwa tena hundi eti kwa kimombo cha GRATUITY?
PCCB hawana strength zaidi ya CAG. Inamaana CAG asingebaini madudu hela za walipa kodi si zilishaibwa na hao jamaa? Inawezekana kabisa hao wezi wanakula mchongo na PCCB.NOOOOO kama kweli majarada yapo kwa Hosea watafikishwa mahakaman,na pia inategemea na uzito na ushahidi wa tuhuma dhidi yao.PCCB is strong enough,subirin mtaona
Takukuru ni Washing Machine ya Mafisadi na Hapo hamna Kesi yoyote na hakuna mtu atakayepelekwa Mahakamani au Gerezani zaidi ya Takukuru kula Kodi zetu kwa uchunguzi wa kijinga na mwsiho watakuja na conclusion ya kusema hakuna wizi uliofanyika zaidi ya kelele za Wapinzani na hatufanyikazi kwa kusukumwa na Wapinzani. Dr. Hosea pia ni Janga la Taifa kama Kikwete. Help us GOD tutoke hapa tulipo
Ericus Kimasha,Watanzania hasa vijana, kwa ufahamu wangu na udadisi juu ya Politics, Power Strugle and Economy naomba nisimame kuhesabiwa miongoni mwa watakao dumu daima upande wa utetezi kwa Ezekiel Maige.
Mzimu mkubwa unaomwandama huyu Mtanzania si nyumba aliyonunua $0.7M cash au njia aliyotumia kupata hiyo pesa bali ujasiri wake kuvuluga syndicate ya waporaji wa maliasili zetu waliodumu kwenye sekta tangu miaka ya mwanzo wa 1960.
Na kubwa la pili ni malengo makubwa na dhamira ya dhati iliyokuwa ikijidhihirisha katika mafanikio yaliyokuwa yameanza kupatikana katika sekta ya Maliasili na Utalii. Maize asingeweza kuyafanya haya bila kuyagusa na kuyabatilisha maslahi makubwa na ya toka enzi ya wakubwa wa nchi hii. Wakubwa hao wengi wako nje ya serikali na hata nje ya nchi. Wananguvu za kubadilisha uongo kuwa ukweli na kinyume chake vilevile. Mwiko aliouvunja Maize ndo Ngeleja alidhani kwa kuuenzi nao watamuenzi kumbe haikuwa hivyo. Ngeleja hajavuluga maslahi ya mkubwa yeyote ila pale wao walipokula yeye kakomba mboga hadi kulamba mwiko.
Rai yangu kwa vijana wasimeze habari kama zinavyowekwa kwenye vyombo vya habari. Na katika yanayoitwa kashfa kuu kupitia kamati za Bunge msichukulie wajumbe kama Malaika na kudhani kila wanalotaarifu ndo ukweli. Hata marefa wana timu zao! Ukitaka kunielewa rejea mswada wa kuondoa kodi kwenye mafuta ya taa uone jinsi Bunge na Kamati zinavyotumika ki-udalali hata katika masuala nyeti.
Nikipata muda nitajitahidi nifumbue mafumbo zaidi labda vijana wenzangu mtanielewa. Hapa mimi si mjumbe wa Maige bali ni muathirika wa ukweli uliopindishwa. Kwa jinsi hii taifa litaendelea kuwakosa watu wenye maamuzi yenye manufaa kwa wananchi. Mbaya zaidi sijazisikia sauti za Wazawa ambao kwa hakika kabisa walipewa vitalu kwa mara ya kwanza toka Tanganyika huru. Simameni jamani, jitokezeni muuweke ukweli huu wazi na Watanzania wasiojua waelewe pumba na mchele.
Ni dhambi kubwa kumuacha Maige kujitetea mwenyewe kwa jambo alilolifanya kwa nia safi kuwanufaisha ninyi Wazawa.
Watanzania hasa vijana, kwa ufahamu wangu na udadisi juu ya Politics, Power Strugle and Economy naomba nisimame kuhesabiwa miongoni mwa watakao dumu daima upande wa utetezi kwa Ezekiel Maige.
Mzimu mkubwa unaomwandama huyu Mtanzania si nyumba aliyonunua $0.7M cash au njia aliyotumia kupata hiyo pesa bali ujasiri wake kuvuluga syndicate ya waporaji wa maliasili zetu waliodumu kwenye sekta tangu miaka ya mwanzo wa 1960.
Na kubwa la pili ni malengo makubwa na dhamira ya dhati iliyokuwa ikijidhihirisha katika mafanikio yaliyokuwa yameanza kupatikana katika sekta ya Maliasili na Utalii. Maize asingeweza kuyafanya haya bila kuyagusa na kuyabatilisha maslahi makubwa na ya toka enzi ya wakubwa wa nchi hii. Wakubwa hao wengi wako nje ya serikali na hata nje ya nchi. Wananguvu za kubadilisha uongo kuwa ukweli na kinyume chake vilevile. Mwiko aliouvunja Maize ndo Ngeleja alidhani kwa kuuenzi nao watamuenzi kumbe haikuwa hivyo. Ngeleja hajavuluga maslahi ya mkubwa yeyote ila pale wao walipokula yeye kakomba mboga hadi kulamba mwiko.
Rai yangu kwa vijana wasimeze habari kama zinavyowekwa kwenye vyombo vya habari. Na katika yanayoitwa kashfa kuu kupitia kamati za Bunge msichukulie wajumbe kama Malaika na kudhani kila wanalotaarifu ndo ukweli. Hata marefa wana timu zao! Ukitaka kunielewa rejea mswada wa kuondoa kodi kwenye mafuta ya taa uone jinsi Bunge na Kamati zinavyotumika ki-udalali hata katika masuala nyeti.
Nikipata muda nitajitahidi nifumbue mafumbo zaidi labda vijana wenzangu mtanielewa. Hapa mimi si mjumbe wa Maige bali ni muathirika wa ukweli uliopindishwa. Kwa jinsi hii taifa litaendelea kuwakosa watu wenye maamuzi yenye manufaa kwa wananchi. Mbaya zaidi sijazisikia sauti za Wazawa ambao kwa hakika kabisa walipewa vitalu kwa mara ya kwanza toka Tanganyika huru. Simameni jamani, jitokezeni muuweke ukweli huu wazi na Watanzania wasiojua waelewe pumba na mchele.
Ni dhambi kubwa kumuacha Maige kujitetea mwenyewe kwa jambo alilolifanya kwa nia safi kuwanufaisha ninyi Wazawa.
Elli,Eti, haiwezekani wakatolewa hadharani kwa wananchi wenye hasira kali wakamaliza game? mbona vibaka wa simu na kuku huwa wanakutana na wananchi wenye hasira kali? hawa vipi hawaingii kwene category hii? laiti wezi wa kuku nao na wale wa simu wangekuwa wanachunguzwa na Takokuru haki ingepatikana bila ya ncha ya upanga
Hivi hawa mawaziri na huwa wana kinga wawapo madarakani?
Inakuwaje nyendo zao hazichunguzwi kipindi wapo madarakani? Sababu hii taarifa zinaonyesha haya mambo hawakuyafanya baada ya kuondoka wizarani bali ni sehemu ya maisha yao walipokuwa pale.
Nashindwa kuelewa hii nchi ipo salama kwa kiwango gani... Hawa PCCB wanapswa wajiulize wanamsaidiaje rais na nchi.
Utata mwingine ni kitendo cha rais kutoa speech inayotafsirika kama vile anawalilia mawaziri wake kwa kusema wanaponzwa na watendaji wao na kuahidi safari hii ku deal na hao watendaji.
Nazidi kujiuliza kama hawa ndiyo rais alikuwa anawalilia au tumpe nafasi atuonyeshe wengine!