Mkulo awashambulia TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo awashambulia TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makerubi, Jun 28, 2011.

 1. m

  makerubi Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Fedha, Mustafa Mkulo, amelishambulia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa kuendelea kuchukua fedha za Serikali zitokanazo na kodi ya wananchi kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya mitambo ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) bila dalili yoyote ya kurudisha fedha hizo.

  Hata hivyo, shirika hilo limesema tayari Serikali imetoa fedha za kununulia mafuta ya mitambo hiyo ya IPTL na hadi juzi jioni, mitambo hiyo ilifikia uzalishaji wa megawati 30 kutoka 10 baada ya mafuta hayo kuanza kutumika.

  Akizungumza na HABARILEO kwa njia ya simu jana kuhusu fedha za kununulia mafuta hayo, Mkulo alisema, hafahamu chochote kuhusu mchakato wa kutolewa fedha hizo kwa kuwa yupo Dodoma.

  Amesema, jambo la msingi linalotakiwa ni kwa Tanesco kuhojiwa kwanza namna ambavyo imetumia Sh bilioni 17 ambazo hadi sasa imepewa na Serikali kwa ajili ya kununulia mafuta ya mitambo hiyo na kiasi cha fedha walizoingiza.

  “Mimi naomba mnisaidie, kwani Tanesco ni shirika linalofanya biashara au la nini? Serikali imekuwa ikilipa fedha ambazo ni za walipa kodi kwa ajili ya hiyo mitambo lakini hawaelezi zimetumika vipi na kama zitarudishwa au la,” alisema Mkulo.

  Alisema fedha zinazotumika kununulia mafuta hayo ni za walipa kodi, hivyo haiwezi kuingia akilini fedha zao kutolewa kwa Tanesco bila kurudishwa wakati shirika hilo linajiendesha kibiashara, hali ambayo aliiita kuwa ni sawa na kuwabebesha mzigo wananchi.

  “Je wameshaulizwa namna walivyotumia fedha hizo kuzalisha umeme? Kiasi gani wameuza? Fedha walizouzia umeme ziko wapi na kwa nini hazitumiki kununulia mafuta mpaka Serikali itoe tena fedha?” alihoji na kuongeza kuwa si jambo jema kuwaongeza mzigo wananchi kwa kunufaisha wengine.

  Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, alisema utaratibu unaotumika kuchukua fedha za Serikali kununulia mafuta, ni kwa njia ya ankara ya kudai malipo kutoka IPTL kwenda serikalini.

  Amesema, baada ya hapo, kila mwisho wa mwezi IPTL huwajibika kupeleka ripoti Wizara ya Nishati na Madini ya jinsi mafuta yalivyotumika.

  Kuhusu kurudisha hizo za fedha za mafuta ya IPTL serikalini, Mhando aliweka wazi kuwa suala hilo halitawezekana kutokana na ukweli kuwa shirika linajiendesha kwa hasara na linatumia gharama kubwa katika uendeshaji na kuingiza fedha kidogo.

  “Kwa mfano tu, IPTL wao wanazalisha na kuuza umeme kwa senti 32 za Marekani kwa uniti moja, wakati sisi tunazalisha na kuuza kwa senti nane za Marekani, kwa kweli tunajiendesha kwa hasara, hatuwezi kulipa hizo fedha,” alisema.

  Akizungumzia kuwashwa kwa mitambo hiyo ikiwa ni kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme katika bwawa la Mtera na hivyo kusaidia kupunguza makali ya mgawo wa umeme, alisema tayari fedha zimetolewa na Serikali kwa Wizara ya Nishati na Madini na mafuta yameanza kupakuliwa.

  Alisema, kuwashwa kwa mitambo hiyo na kupewa mafuta kutasaidia kupunguza makali ya mgawo wa umeme nchini na megawati hizo zitakuwa zikipanda kulingana na mafuta na idadi ya mitambo itakayowashwa.

  “Serikali ilitoa fedha tangu juzi kwa Wizara ya Nishati na Madini ambayo ndio wasimamizi kwa ajili ya kuagiza mafuta ya mtambo wa IPTL, na kwa taarifa nilizonazo tayari mafuta yameanza kupakuliwa na kupelekwa kwenye mitambo,” alisema Mhando.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  serikali imejishindwa..wote tuhamie jimbo la kilindi tukale good tym
   
 3. j

  jategi Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nafikiri ni wakati mwafaka sasa kwa tanesco kufanya kazi zake kwa kuzingatia weledi na kuacha siasa na wasiruhusu kuingiliwa na wanasiasa katika kutekeleza mipango yao ya kuzalisha na kusambaza umeme. Kama Tanesco wanaamini kwamba IPTL wanawauzia umeme kwa bei kubwa sana basi waacha kununua umeme wa IPTL wazalishe wa kwao au wanunua kwa wazalishaji wengine ambao wanauza kwa bei nafuu. Aingii akili, hasa akili ya kibiasha kwa mtu kununu unit moja kwa senti 35 alafu yeye anauza hiyo unit moja kwa senti nane, tujiulize hiyo senti 22 ataipata wapi na faida gani mtu huyo anapat kwenye biashara ya namna hiyo? Nakubaliana na Ndugu mkulo kimsingi, kwamba kama shirika linafanya biashara na limeshapewa start up capital inabidi litoe taarifa ya matumizi ya mtaji huo na baada ya muda shirika lijiendesha lenyewe kwa faida na kupeleka gawiwo serikali, sasa katika hali hii ya kununua umeme kwa senti35 alafu inauuza kwa senti nane, Tanesco wanamfaidisha nani, watuweke wazi tufahamu, maana inaweza kuwa tunawalaumu bure hawa ndugu zetu wa tanesco kumbe kuna mtu anafaidi kodi zetu. Jambo la pili ni mipango endelevu ya uzalishaji umeme, sijawaona tanesco kama watu wenye nia ya dhati kuongeza uzalishalisha wa umeme nchi hii, maana vyanzo ni vingi ila hawavitumii wala kuwa na mia ya kweli kuvitumia. Rai yangu kwa tenesco ni kwamba wabadilike, kwa haraka ili kuondoa haibu hii ya kugawa giza kwa wananchi na kudidimiza uchumi wetu
   
 4. s

  saggy Senior Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanini IPTL wanunuliwe Mafuta halafu tena wauze Umeme kwa Tanesco Jamani?Hivi Wabunge wetu mpo jamani?mbona mnanyamaza mpaka Waziri anawafumbua macho na hamtaki kumuunga mkono kutetea Mabillion ya walipa kodi yanayopotea jamani?
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Jaman me nashangaa kama ubunifu wa suluhu ya matatizo ya umeme umeshindikan jaribun hata kuangalia nchi jiran wenzetu wanafanyaje katika secta hiyo nahis itatusaidia maana kuumiza vichwa imeshindikana. by the way hiz resource ambazo tunazo mbona hazitusaidii je ni kwaajili ya kunufaisha wagen?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,644
  Likes Received: 82,365
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa kuhusu hili. Pesa itoke hazina kuwanunulia mafuta IPTL ili waendeshe mitambo yao. Kwani wao si wanalipwa na TANESCO sasa inakuwaje washindwe kununua mafuta wenyewe mpaka wapate pesa toka hazina? Je hizi pesa toka hazina wanazilipa? au ndio ufisadi kama kazi?
   
 7. s

  saggy Senior Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli,mimi mpaka naona machozi yananilenga!kweli ,kweli jamani,kweli wamama Wajawazito wanakufa kila siku,Hospitali hazina madawa,watu wanashinda kula mlo mmoja kwa siku huku Watetezi wetu Wabunge wamenyamaza wakati wanajua IPTL wananunuliwa mafuta na Serikali ili wazalishe umeme ambao tene unauzwa kwa Tansesco? Kwanini tunanyamazia jambo hili,mpaka Waziri anasema kwa Huruma na tunanyamaza jamani?

  Kwanza tunataka Waziri mwenye dhamana atuambie kwamba ni Shillingi ngapi IPTL wamepewa angalau tu kwa Mwaka huu unaoshia Juni 2011!
   
 8. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Toka lini Serikali ikalipa bili za umeme?
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Watu wengine wanajadili mambo bila kuwa na uweledi nayo. The root causes ya matatizo haya yote ni Wanasiasa na SERIKALI yetu walio-SIGN mkataba na IPTL. Mkataba wa SERIKALI na IPTL unasema kwamba serikali kwanza itailipa TANESCO Tsh 5 bilion kwa mwezi hata kama inazalisha au haizalishi umeme. Pia Serikali itainunulia mafuta IPTL ya kuendeshea mitambo yake. Na mwisho IPTL itaiuzia TANESCO unit 1 kwa $ 35 wakati TANESCO wao wanatuuzia watanzania unit moja kwa $ 8.

  Hao ndiyo maamuzi ya wanasiasa wetu walio sign mkataba na IPTL. Kuwalaumu TANESCO ni ujinga wakati tunafahamu waliongia mkataba na IPTL ni serikali sio TANESCO. Kwakuwa sisi Watanzania tumekataa kuwaadabisha wanasiasa wetu in a ballot box, simply kwasababu ya ushabiki wa kivyama ngoja tuonje joto ya jiwe. TANESCO kamwe haiwezi kujiendesha kibiashara kama inaingiliwa na wanasiasa na hasa hao wala rushwa wa serikali ya CCM.
   
 10. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi nchi hii ingekuwa bado inatawaliwa na Wazungu pamoja na kukosa mvua tunekuwa tuna tatizo la Umeme? Nauliza.
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu Mkulo ana wapumbaza wajinga tu. Sio werevu kama mimi. Kama kweli anataka aumbuke aoneshe mkataba SERIKALI iliyo-sign na IPTL. Hayo yote anayolalamikia yako kwenye mkataba. Ni serikali hii ya CCM iliyo sign mkataba huo mbovu kwasababu ya rushwa. JK akiwa waziri wa nishati na madini.

  Serikali ilishajibaragua kwenda mahakamani ICC ikaishiwa kubwagwa chini. Tutaendelea kunyonywa na IPTL kwa kipindi cha miaka 20 kutokana na serikali ilivyo-sign mkataba. The root causes ya matatizo haya yote ni viongozi wala rushwa wa serikali ya CCM. Watanzania mtalia hadi machozi ya damu lakini bila kuindoa hii cancer (read CCM). Matatizo yetu hayatapungua bali yatazidi kuongezeka. Mwaka 1997 mgao wa umeme ulikuwa 12 hours, leo mwaka 2011 mgao wa umeme ni 72 hours, believe me kufikia 2015 mgao wa umeme uta last for 128 hours ie 7 days, the writing is already on the wal.
   
 12. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Tatizo kila mgao wa umeme unapokuwepo ni dili kwa kundi fulani la watu hasa hao waliosaini hiyo mikataba feki,
  mafuta yakinunuliwa kuna watu wana percent zao,mitambo ya IPTL ikiwashwa kuna kamisheni kibao.
  Mi nawashauri watanzania wote kutoka kila kona ya nchi,mwenye debe haya,mwenye ndoo haya,mwenye pipa hayaa,na hata mwenye kidumu cha lita tano au hata mwenye mkojo tu tujitokeze wote tuende Mtera na KIDATU tukamwagie huko hayo maji ili mitambo ifanye kazi then tuone watakula wapi.Ni mtizamo wangu tu.
   
 13. E

  Evergreen Senior Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo ndiyo hata mm nashindwa kuelewa,Unampa hela azalishe Umeme,halafu akizalisha anakuuzia kwa bei mbaya!! Hapa bado siielewi,kwanza kwa nn IPTL wapewe hela?
   
 14. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Simple tusingekuwa na tatizo la umeme. Kwani quality ya social Services 1961 ukilinganisha na leo hii...quality then was goodLike people who have seen the inside of a classroom some hopeless MPs keep talking about increased numbers of infrastructures as a measure of development... Hivi pop ya TZ ni static? Unaposema shule zimeongeze so what? Hivi kazi serikali ni nini? Jamani hawa wabunge posho kazi kweli kweli...Wonders shall never end.
   
 15. s

  saggy Senior Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana Bobuk,Unit moja haiwezi kuuzwa Kwa $35 Bwana! Ni $0.35 na na $0.8 kwa taarifa yako.Huenda Hesabu zinakupiga chenga kidogo!

  Ahsante Bwana Bobuk kwa maelezo yako mazuri,ni kweli kwamba kuna watu waandika mada humu bila kuwa na weredi nayo.Hata mimi sikuwa nafahamu vizuri na maelezo yako yamenisaidia kufahamu vizuri the Story.
   
 16. s

  saggy Senior Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi ni nani ali Sign mkataba wa IPTL jamani,naomba nisaidiwe na wanajamii wenzangu!
   
Loading...