Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo, alisema.
Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.
Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.
Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!? aliongeza.
Hiyo RED: Kwani Bw. Mkullo ana faida gani hasa kwa Tz? Ni mfujaji na fisadi kama aliyemteua tu. Nionavyo mimi hofu aliyonayo si hasa kuhusu Uwaziri bali ni kutokana na madudu mengine tu ambayo yanamwandama.