Mkulima na Punda

Mkulima na Punda

Red Scorpion

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,736
Reaction score
4,255
Mkulima mmoja alikuwa na Punda aliyedumu nae kwa miaka mingi sana akimsaidia shughuli za kilimo na uchukuzi. Alikaa naye toka akiwa mtoto mpaka punda akawa mzee kabisa.

Siku moja wakiwa wanatoka shambani, kwa bahati mbaya yule punda alitumbukia kwenye kisima kirefu sana ambacho kwa wakati ule kilikuwa kimekauka. Yule Mkulima akawaza sana atafanyaje kumtoa yule punda na baada ya kutafakari sana akasema kwanza hata hivyo huyu punda ameshazeeka ni hasara kuingia gharama za kumtoa. Akaona vema tu amzike humo humo.

Akaenda kuita majirani, wakaja na sepetu wakaanza kumwagia udongo, mchaka na Matakataka ili kumfukia. Mwanzoni tu ni kama punda alijua kitachoendelea, akapaza sauti na kulia kwa sauti kali ajabu. Sauti ya malalamiko. Hawakujali waliendelea kufukia kwa kutupia kila aina ya taka taka.

Baadae kidogo kwa mshangao wa wengi ghafla punda alinyamaza kimya kabisa sauti ikapotea. Baada ya kutupia taka kadhaa, mkulima yule akaamua kuchungulia shimoni. Alishtushwa mno na alichokiona kila taka na mchanga ulipokuwa ukiangukia mgongoni mwa punda, alikuwa akifanya kitu cha kushangaza.

Udongo ulipomwangukia, alijitingisha ukamwagika na akaukanyaga akainuka juu kidogo. Kila ulipokuja aliendelea kufanya hivyo hivyo, hatimaye baada ya muda mkulima na majirani walishangaa kuona amefika juu kabisa ya ukingo wa kisima na akatoka kwa furaha kabisaa.

# FUNZO
Kuna wakati maisha yatakurushia matakataka ya kila aina. Acha kulia na kupiga kelele, Jitingishe, Yafanye ngazi. Kila jaribu linalotupata ni ngazi ya kupandia.

Kamwe hatuwezi toka kwenye visima virefu kwa kulia peke yake. Bali kwa kupambana kuchomoka kwa Juhudi na Maarifa. Wacha waone uko kimya baada ya Makombora waliokurushia. Yadake, yapange, yafanye ngazi ya kupandia.

Changamoto yeyote unayopitia sasa, ni shimo na michanga. Binadamu ni zaidi ya punda. Acha kulia, Jikung`ute, Yakanyage, Nyanyuka juu, Toka Shimoni..Kanyaga
Twende Mbele.

IMG-20171102-WA0081.jpg
 
Somo zuri sana mkuu,Ni hadithi sema ni funzo la kweli.Wakati mwingine ukiona unaelemewa sana we usichoke yawezekana ndiyo nafuu inakuja.
 
Back
Top Bottom