Mkulima aenda kuchukua fomu za urais, ashindwa kulipa milioni, atoweka

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,836
7,492
11418907_386572794861723_2362812716647963344_n.jpg
Mkulima darasa la saba Eldoforce Bilohe amekua kituko baada ya kukaribishwa CCM makao makuu DODOMA na kisha kushindwa kukamilisha zoezi kwa kukosa fedha.

Amepata ushabiki mkubwa kutoka kwa wananchi na waandishi. Kaingia kwa miguu na kaondoka kwa miguu kuelekea benki hata hivyo amechelewa kurudi.

Chanzo: AZAM TWO

Bonyeza HAPA kumsikiliza wakati akiongea na waandishi wa habari
 

Attachments

  • JamiiForums Mgombea.mp3
    801.1 KB · Views: 4,463
Mkulima kahojiwa kasema hana elimu ila anauzoefu kwenye chama waandishi wamemzingira kuliko wachukua fomu wote ukiacha lowasa alivaa t-shirt chovu ya ccm na anaonekana hana uchumi kapauka sana na anaonekana mzee kwa shida si kwa kuzaliwa zamani
 
Aliyemwambia hiki Chama chetu ni cha wakulima walala hoi ni nani? Chama cha hadhi yake kilishakufa na Mwl. NYERERE ati. Kimebakia Chama cha wenye nazo wafanyabiashara na mafisadi. NO mkulima wala Mfanyakazi
 
Maajabu yanaendelea ndani ya CCM.Ukistaajabu ya mafisadi kupewa fomu utaona ya mwananchi wa Mjimtala Kigoma Bwn.Idfonce Dihole alifika Dodoma kuchukua fomu ya kugombea.Huku akiwa na maji mkononi aliingia ofisi za CCM kwa mbwembwe na kuchukua fomu kuomba ridhaa
 
Mgombea urais ndg Edfonce kutoka Kigoma ambaye ni mhitimu wa darasa la saba amechukua fomu ya kugombea. urais. Ninavyofahamu ni kuwa mgombea urais anapaswa kuwa na elimu ya chuo kikuu. Sasa imekuwaje huyo ameruhusiwa kuchukua fomu?
 
Maajabu yanaendelea ndani ya CCM.Ukistaajabu ya mafisadi kupewa fomu utaona ya mwananchi wa Mjimtala Kigoma Bwn.Idfonce Dihole alifika Dodoma kuchukua fomu ya kugombea.Huku akiwa na maji mkononi aliingia ofisi za CCM kwa mbwembwe na kuchukua fomu kuomba ridhaa


Alilipia fomu?
 
Huu ni mtego mkubwa kwa chama tawala,wakimkatalia itaonekana kweli CCM ina wenyewe (elite group/few select) ambao wanawatumia tu supporters wao (wengi wana elimu duni) for their political interests lakini hawawaoni kama ni wenzao ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom