MKUKUTA Phase I: Maoni yako

Jambo la kwanza mimi nasema sisi siyo masikini wa mali umasikini wetu ni wa akili. Wakubwa wanatuambia sisi ni masikini na sisi tunakubali na tunaimba wimbo huo. Jambo la kufanya ni kukataa umasikini, kwa sababu rasilimali tunazo na tuanze kutumia akili zetu kufikiri ni namna gani tutajikwamua kutoka kwenye umasikini wetu kwa kutumia rasilimali tulizonazo. Tatizo letu ni kuwa tuna mipango mingi sana lakini utekelezaji hakuna au ni kidogo sana. Kazi yetu kubwa ni kulalamika na kulaumu serikali,ndugu na kila mtu tunayeweza kumlaumu tunashindwa kuchukua majukumu yetu au kujilaumu wenyewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yetu.

Tunalotakiwa kulikazania ni Uwezeshaji kiuchumi na kuwapa watu wetu maarifa yaani elimu ya juu college au Chuo kikuu siyo ile ya kufuta ujinga. Pia tufundishe Ujasiriamali vijana wetu wawe waajiri badala ya kuwa waajiriwa. Ikiwezekana tuwe na mfuko wa elimu/na uwezeshaji kutoa ruzuku siyo mikopo kuwasomesha watoto wetu wote. Pesa zinaweza kupatikana kwa kuchangisha harambee, kushirikisha wadau Serikali, wananchi, wafanyabiashara, nchi rafiki, NGOs nk. Usiseme pesa hakuna Mbona yakitokea maafa huwa wanachangia? tusisubiri maafa. Nimekazania elimu kwa sababu mifano hai inaonyesha nchi zilizotoa kipaumbele kwa elimu kama India, China Japan n.k. zimepiga hatua. Mfuko huo pia unaweza kutumika kwa uwezeshaji kutoa ruzuku kwa watu wote wanaopenda kuwa wajasiriamali. Watu hawa wanaweza kupewa maarifa ya ujasiriamali ili wabuni miradi na kuwa Waajiri badala ya kuwa waajiriwa.

Tukiendelea kuchezea elimu tutajenga taifa la wajinga na kazi yetu itakuwa ni kuwabebea wawekezaji mikoba yao. Hili wazo la kuanzisha mfuko wa uwezeshaji ninalo kichwani hata kama watu wote watakataa kulifanya mimi najipanga kulifanya hapo baadaye mambo yangu yakininyookea.
CHARLES NAZI
 
nyie hakuna lolote mnalolifanya,huo umaskini utaondolewa kwa maoni?????????????Mfumo bomu? hata mkiandika maproposal mazuri bila kubadilisha mfumu hakuna kitu, nyie endeleeni kupiga domo ili walau mwisho wa mwezi mpate cha kuweka kinjwani, hakuna kingine, mkapa aalimleta yule prof SATO mbona hakuna mabadiliko????msaidieni mkulima wa papmba, korosho, kahawa, katani, matunda, mvuvi,kuongeza samani kwa mazao yao then mhakikishie soko la uhakika, mbona tutataendelea tu? bila ya kulizan amaswali
 
Back
Top Bottom