Za10,
Kuna jamaa yangu wa Ghana ambaye nilikuwa naye kama week moja iliyopita alinishangaa wakati namweleza kuhusu upotevu wa zaidi ya $1bn katika dili za kifisadi kupitia viongozi wa dola na wapambe wao. Alinambia kuwa wakati wa Jerry Rawlings waliunda kikosi cha kupambana na rushwa ambacho hadi sasa kinafanya kazi nzuri. Ukiacha tatizo la muundo wake kwamba wakuu wake ni maofisa wakuu wa jeshi na polisi, jamaa alisema hiyo anti-corruption unit inatisha sana. Alinambia kuwa baada ya uchaguzi kuna baadhi ya kesi za rushwa ambazo rais mpya ameagiza zishughulikiwe haraka. Matokea yake watu wanataka kufa kwa pressure na tayari waziri mmoja wa zamani kakamatwa uwanja wa ndege akitaka kuingia mitini. Jamaa anasema kuwa Anti-corruption kama yetu iliyochini ya rais haiwezi kamwe kufanya kitu. Hata kwao wanayo ya dizaini hiyo ambayo wananchi hawajui hata inachokifanya. Kwa ufupi PCCB yetu ni sehemu ya drama ya uongozi wa hovyo na ufisadi! Nadhani tunahitaji jeshi kidogo ili tupige kwata. Hata nidhamu ya wanafunzi wa Mgulani na Makongo siyo sawa na Kinondoni Muslim!!
Za10,
Katika hilo la misaada na masharti yake, kweli kwa muda mrefu huo ndio ulikuwa mwelekeo na hata Bilaterals pamoja na multilaterals ukiondoa mashirika ya Umoja wa mataifa waliweka masharti ikiwa ni pamoja na kuwa na utawala bora na kuheshimu haki za binadamu.Hapa karibuni nadhani miaka mitatu sasa, katika kuboresha ufanisi wa misaada, wadau wa maendeleo ( donors) na serikali walijadili na hatimaye kukubaliana na serikali kuwa misaada yote sasa ipitie mkondo wa bajeti ya serikali ( GBS - General budget support).Kwa maana hiyo basi pesa ya wafadhili ukiondoa USAID ambao Sera zao haziruhusu modality hii wanatumbukiza misaada yao katika bajeti na hawatoi tena misaada through projects ( project support ni kwa kiwango kidogo sana).Sijui kama kuna tathmini imefanywa kuona kama kuna ufanisi katika utaratibu huu.Angalau project support ulikuwa unaweza kufanya evaluation ya project na kuona kama yale malengo yamefanikiwa ukilinganisha na kiwango cha pesa iliyotumika.Sijui hili unalionaje.
WoS:
Hili ni suala gumu kwa sababu watawala wetu bado wanafanya tathimini za maendeleo kutokana na wao kukamilisha miradi.
Kwa sababu nia nzima ya kuwepo kwa misaada ni kuondoa umasikini. Hivyo tuanze kwa kuangalia vigezo vya kumwita mtu masikini. Na kwa kutumia vigezo hivyo basi tunaweza kusema kuwa misaada hiyo imesaidia au imetuacha pale ilipotukuta.
Na kigezo kingine ni lazima wale wanaosaidiwa waweze ku-sustain walichosaidiwa. Na kama wanashindwa basi hakuna tofauti kati ya Aid and Relief.
Kwa mfano huyu jamaa chini ameelezea umasikini ni nini. Lakini tunaweza kuwa na vigezo vyetu na baada ya muda fulani tuangalie kama tumevifikia.
David Gordon's paper, "Indicators of Poverty & Hunger", for the United Nations, defines absolute poverty as the absence of any two of the following eight basic needs:
- Food: Body Mass Index must be above 16.
- Safe drinking water: Water must not come from solely rivers and ponds, and must be available nearby (less than 15 minutes' walk each way).
- Sanitation facilities: Toilets or latrines must be accessible in or near the home.
- Health: Treatment must be received for serious illnesses and pregnancy.
- Shelter: Homes must have fewer than four people living in each room. Floors must not be made of dirt, mud, or clay.
- Education: Everyone must attend school or otherwise learn to read.
- Information: Everyone must have access to newspapers, radios, televisions, computers, or telephones at home.
- Access to services: This item is undefined by Gordon, but normally is used to indicate the complete panoply of education, health, legal, social, and financial (credit) services.
Labda vigezo vya Tanzania tunaweza kuongeza kuwa amani na mshikamano ni utajiri wetu na tumefanikiwa katika hilo!( sic!)
Nimesoma katika Guiness Book of Records 2009 kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watu wasiokuwa na raha ( most unhappy people)! Nimeshangaa kweli maana we have always been known as watu walio na tabasamu wakati wote... kila kitu ni shwari HAKUNA TABU - NO PROBLEM!
WoS, naona mambo yanaenda yakiongezeka. Kumbe tumeingia hata kwenye GBR!!
Kuna ukweli fulani lakini. Kuna mzungu mmoja alinambia kuwa Watanzania ni hatari sana kufanya nao kazi kuliko Wakenya na Waganda; kwa sababu hata wakichukia wanajifanya mambo ni poa. Akasema TZ itabaki nyuma tu kwa sababu watu wana-protest passively ukilinganisha na Wakenya wanaowasha moto papo kwa papo!
Mkuu..
Duh umenifanyanimecheka;-) maana umenikumbusha village na the way I know maisha niliyokulia..kwa mwendo huu ...tuko mbali mno...maana MAJORITY hawatimizi hivyo vigezo...Aise .if this is the way they define..development..we are no where..no where kabisa..Kwa sababu hata tukitafuta vigezo vyetu..ni vipi...maana kuishi kwenye sakafu ya udongo is already the minimum of the minimum..otherwise sijui..labda wachumi watusaidie..
Labda vigezo vya Tanzania tunaweza kuongeza kuwa amani na mshikamano ni utajiri wetu na tumefanikiwa katika hilo!( sic!)
Nimesoma katika Guiness Book of Records 2009 kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watu wasiokuwa na raha ( most unhappy people)! Nimeshangaa kweli maana we have always been known as watu walio na tabasamu wakati wote... kila kitu ni shwari HAKUNA TABU - NO PROBLEM!
Wakati Tanzania ilishika mkia katika kinyang'anyiro hicho cha watu wenye raha katika nchi 98 zilizoshindanishwa, Denmark iliibuka mshindi wa kwanza, kwa kuwa na watu wenye raha!
I like your comments comrade!
You could be right.Nadhani some of the global commitments zinafanywa na viongozi wetu kama namna ya ku conform ili kunufaika na misaada na siyo kufanya kweli! Ukiangalia kiasi cha ufadhili nchi yetu inachopata kama namna ya kutekeleza hayo malengo ya milenia na pia kutengezea MKUKUTA na michakato yake, utaona kuna wanaofaidika na hiyo michakato.Kila kukicha ni seminar kuhusu MKUKUTA, MDGS - mara warsha za wadau maana hiyo michakato ni highly consultative na participatory.Mwisho wa siku matokeo ni vigumu kuyapata hasa kwa wale walengwa - wananchi waishio chini ya hiyo $1 kwa siku.Anayepokea posho za warsha si mwanakijiji wala mlalahoi wa mjini bali ni technocrats wa mijini wenye mishahara yao, wenye vibiashara vyao wanavyofanya baada ya saa kazi n.k. Ukiupunguza umaskini by half hata warsha na seminar zitapungua.Ukiufuta umaskini kabisa basi tena utakuwa umefanya baadhi ya watu ( donors, consultants etc) kukosa kazi.
Pole sana ndugu yangu.
Uliamini kabisa kuwa MKUKUTA na MKURABITA vitakuteremshia gharama za maisha?
Kimsingi MKURABITA, kama ungetekelezwa kimantiki... ni sera bora sana kuliko ndugu zetu kupoteza ardhi na thamani nyingine bila msaada wa kitaalam... Kuhusu MKUKUTA, hakuna kitu PERIOD!!!
hata waliopewa majukumu hawakutranslate mkakati kikakimilifu...as always it is the capacity to execute roles and responsibilities that has been a challenge kwa watanzania