Mkude gangwe!

Mkude gangwe kavuliwa mpaka chupi bado anasubiri ushahidi kamili. Dudu aingie ndani.
 
Mkude gangwe alijikwaa mlimani akiwa kabeba tenga la maboga boga 1 lika vingirika basi akafurahi ile mbaya,... kumbe mnaweza kutembea wenyewe akamwaga tenga zima akabaki na tenga tupu , ... tangulieni sokoni ntawakuta
 
Mkude gangwe,baada ya hakimu kusoma kesi,aligundua mkude hana hatia,akwambia,"kuanzia sasa mkude uko huru kurudi uraiani,hauna hatia",mkude akakataa kurudi uraiani ili kumkomoa hakimu!
 
Jaaaah! Mkude kweli gangwe kapanda Abood kwenda Dar kalipa nauli tu lakini ndani TV kaangalia buree hata hawajamtoza
 
Mkude gangwe,kafika mlangoni kwake,kapiga hodi robo saa nzima bila mkewe kufungua,baada ya mkewe kufungua mlango,kakataa kuingia ndani,kalala pale pale nje ya nyumba hukua akinyeshewa na mvua!
 
Mkude gangwe,kalima, kavuna mahindi gunia 10,kisha akaalika majirani,akatumia gunia 8 katika sherehe ya kujipongeza kwa mavuno mazuri!
 
Hahahahahaha lol! Mkude gangwe mtoto wake anaumwa akaamua kumpeleka hospitali. Ilipofika zamu ya Mkude gangwe kumuona Dr akamwambia daktari, "Mwanangu anaumwa hapati choo lakini anaharisha sana" Mkude kweli gangwe.
 
Mkude gangwe alijikwaa mlimani akiwa kabeba tenga la maboga boga 1 lika vingirika basi akafurahi ile mbaya,... kumbe mnaweza kutembea wenyewe akamwaga tenga zima akabaki na tenga tupu , ... tangulieni sokoni ntawakuta
ahaaa,.mkude basi mkali..!!
 
Mkude Gangwe, alienda hospitali kung'oa jino moja linalouma, akaishia kung'olewa yote kwa sababu daktari kamwambia bei ya kung'oa jino moja ni shilingi elfu tano na hata uking'oa yote bei ni hiyo hiyo.

Alipofika nyumbani huku akiwa kibogoyo kabisa akamsifia Mamakoba kuwa kamkomoa daktari.
 
Mkude Gangwe, alienda hospitali kung'oa jino moja linalouma, akaishia kung'olewa yote kwa sababu daktari kamwambia bei ya kung'oa jino moja ni shilingi elfu tano na hata uking'oa yote bei ni hiyo hiyo. Alipofika nyumbani huku akiwa kibogoyo kabisa akamsifia Mamakoba kuwa kamkomoa daktari.
Ayaaaah,mkude kaharibu kabyser!
 
Mkude gangwe,kagoma kumpeleka mwanae kidato cha kwanza kuwakomoa walimu waliojipendekeza kumfaulisha!
 
Mkude kweli Gangwe hela aliyoipata aliporudi kupigana vita ya nduli kule Uganda aliinywia yote ila rafiki yake koplo Mtemvu yeye hela yake alijengea nyumba.
Mkude alisikika pale kwa mama Joisi akinyaka ulabu akiwa na Dudu
Mkude " sijapata kuona mtu mjinga kama koplo Mtemvu, wewe hela ukaijengee nyumba kwani utaishi maisha, eti hio akili ya mtu kweli?"
Dudu "Mhh hapaana iyo sio akili ni matoope"
Mkude "Mimi hela yangu mtoto wa kihuni nakata maji, wee mama Joisi leta nusu kkama tulivyoo"
 
Mkude kapangisha nyumba yake ya Kiloka kwa,bondwa,koba,bang'ala na semoze ye mwenyewe analala sebuleni ha ha haaaaaaaa
 
Back
Top Bottom