Mkosokoto kwenye korodani ya kushoto

Mkosokoto kwenye korodani ya kushoto

Atukuzwe Mungu

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2018
Posts
210
Reaction score
280
Korodani yangu upande wa kushoto ina kama kamba zimejisokota, nimeenda hospital kufanya ultrasound Dokta akasema nina varicocele, matibabu ya kufanyiwa operation ili kutoa huo msokoto.

Hali hii imekuwa ikinipa usumbufu kama vile kuhisi joto kali kwenye korodani, miguu kusumbua kama nitasimama muda mrefu eg 20min.

Natafuta ushauri kuhusu changamoto ya Varicocele. Kama kuna mtu anajua daktari mzuri wa mfumo wa uzazi wa wanaume (Urologist) au ana uzoefu na jinsi matibabu yake yanavyokwenda, naomba anisaidie maelekezo.
 
Hapana, Sina maumivu makali ila usumbufu tu wakati wa kutembea kwani nikiwa natembea korodani ya upande wa kushoto kama vile imeelemewa na uzito wa huo msokoto na kulazimisha kuingia mapajani wakati natembea. Pia nahisi joto kali sana sehemu ya korodani.
Tofauti na upasuaji unaweza fanyiwa embolization , ila pia ukifanyiwa operation haiathiri uwezo wako wa tendo ila inaboresha tofauti na ukibaki na tatizo, ila kuna mda pia wa kupona ili uweze kurudi Kawaida.
 
Tofauti na upasuaji unaweza fanyiwa embolization , ila pia ukifanyiwa operation haiathiri uwezo wako wa tendo ila inaboresha tofauti na ukibaki na tatizo, ila kuna mda pia wa kupona ili uweze kurudi Kawaida.
Oooh!! Asante sana mkuu, hiyo tiba kwa hapa Moshi Kilimanjaro napata hospital gani mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom