Kuna Jamaa ana mpenzi wake, wanakaa tofauti lakini wapo karibu sana. Jamaa anafunguo za nyumba ya mpenzi wake kwa hiyo asipomkuta hufungua na kukaa akimsubiria halikadharika na demu hivyohivyo. Sasa kasheshe imejitokeza kumbe jamaa alichukua kadi ya gari ya demu bila kumwambia kaenda kuchukulia mkopo yapata mwaka sasa. Na jamaa hali mbaya sasa ameshindwa kumalizia deni, watoa mikopo wamekuja juu wanataka gari tu. Hapo demu ndio amejua kumbe kadi yake ilitumika kukopa huo mkopo nae kaja juu ile mbaya na hamtaki tena huyo jamaa.
katika hali hiyo wa JF mnashauri nini?
Hakukopa Benki alikopa kwa watu binafsi
tabu ya kudate ma-opportunist ndio hiyo.
Mmmh, benk gani inayokubali collateral bila consent ya mwenye jina?? Labda kama alifoji kiapo cha huyu dada.
Anyway, wanasheria wapo awatumie.
ni story ya kweli , huyo demu ana jina la kilugha, kama Bumi, Gwantwa huwezi kujua kama demu au mwanaume. alitumia jina la demu kama jina lakeStory ya kutunga hiyo tena ya kusadikika, unawezaje kutumia kadi au hata hati ya mtu mwingine kuombea mkopo na Kampuni gani itafanya ujinga kutoa huo mkopo.Huyo msichana hana cha kuogopa adunde na gari lake mtaani na siku akija kukamatwa na hao ambao huyo kaka alikopa awaulize ni lini yeye kama yeye aliwahi kuomba mkopo period
Kongosho na BADILI TABIA, hakukopa bank. Loan sharks wa mitaani hawana hiyana, unaweza kuweka rehani hata sufuria na blender! Yaani hiyo kitu kama imelogewa aisee, watu wanatapeliwa magari hivi hivi mjini.
kama ndo hiyo nadhani msaada wa kisheria unahusika hapo.......
watachukuaje dhamana ambayo mhusika hajasign?
ila kama hela anazo akomboe tu gari lake........
walaahiiiiiii mwanaume wa namna hiyo unaweza kumchinj aisee.....
halafu abadili vitasa vya nyumba yake.....