Mkuu m2me wakati tunachukua mkopo kuna mkataba huwa tunasign ila wengi wetu hatusomi kilichoandikwa embu jaribu kuchukua ule mkataba usome kipengele hadi kipengele inawezekana ukapata majibu ya maswali uliyouliza.
Shida zinatufanya tusisisitizie kusoma. Na zile terms and conditions ni nyingi mno na jamaa wanafanya kusudi kuziweka kwa small fonts uone uvivu na shida kuzisoma.
Hivi ile bima inayolipiwa katika makato ya mkopo inasimamia nini hasa?
zili nakala zinatakiwa kuwa tatu ambopo ukishasaini wewe pamoja na mwajiri moja unatakiwa upewe wewe nakala moja pmj na mwajiri wako moja kama hujapewa fuatilia ni muhimu sana kuwa na nakala yako.Nashukuru mkuu, ngoja niitafute ILA nakumbuka baada ya kuisaini ilirudishwa bank kwa ajili taratibu nyingine za kupatiwa mikopo na wala hatukurudishiwa mimi pamoja wafanyakazi wenzangu ambao tulichukua mkopo kwa wakati huo. Tulichopatiwa ni karatasi inayoonesha jinsi makato yatakavyokuwa yakifanyika. Yote kwa yote, nakumbuka hakuna kipengele kilichokuwa kikigusa hayo maswali yangu hapo juu.
Nashukuru mkuu, ngoja niitafute ILA nakumbuka baada ya kuisaini ilirudishwa bank kwa ajili taratibu nyingine za kupatiwa mikopo na wala hatukurudishiwa mimi pamoja wafanyakazi wenzangu ambao tulichukua mkopo kwa wakati huo. Tulichopatiwa ni karatasi inayoonesha jinsi makato yatakavyokuwa yakifanyika. Yote kwa yote, nakumbuka hakuna kipengele kilichokuwa kikigusa hayo maswali yangu hapo juu.
Ilitakiwa na wewe pia ubaki na nakala.......anyway kuna mambo kadhaa.... kwanza kwa uzoefu nilionao kama ni mkopo ambao haukuhusisha hati ya shamba or something like that unaweza kusepa na uwe tayari tu kupigiwa simu ila hawawezi kukufanya chochote zaidi ya kukutoa kwenye gazeti after some months or years hivyo usiogope kabisa.....
Pili kwa upande wa stanbic wana policy zao za kusubmit luku number ao namba ya dawasco kama ulisabmit wanakufatilia nyumbani kwako unless kama umepanga na unategemea kuhama hapo unapokaa ni vyema ila, utakuwa umemwachia landloard msala....... Hilo la kwanza nina jamaa yangu kashapiga bank tatu walipomtafuta kwenye simu hawakuweza kumpata na ni tokea 2010, so kama ni jasiri chukua option number 1.
Mkuu
Nimepitia kipengele cha nane cha mkataba huo kinaonyesha kuwa pande husika hazina budi kuwasiliana kwa maandishi ikiwa kutatokea jambo lolote, hivyo tunaomba utujuze kama kipengele hicho kimetekelezwa?.
Huo ni Mchango wangu, lakini nategemea wajuzi zaidi watakuja kutoa ufafanuzi juu ya suala hili kwa manufa ya wakopaji wengine wa sasa na wajao.