SoC02 Mkopo Elimu ya Juu

Stories of Change - 2022 Competition

Almas22

New Member
Aug 24, 2022
1
0
Kila mwaka takriban wanafunzi laki mbili na nusu (250,000) hujiunga na chuo kikuu katika vyuo mbali mbali kwa ngazi tofauti tofauti.

Baadhi ya Wanafunzi wanaojiunga na chuo hupata heshima ya kupata kutoka kwa Serikali kupitia bodi ya mkopo (HESLB) ili kujikimu kimaisha. Kila mwaka idadi ya wanafunzi huongezeka japo pesa fedha za kuwakidhi zinakua hazitoshi na hili sio jambo jipya.

Mfano mwaka wa masomo 2017/ 2018 serikali iliidhinisha shilingi bilioni 427 kwa ajili ya wanafunzi 122,000 ilihali mwaka wa masomo 2016/ 2017 Serikali iliidhinisha shilingi bilioni 483 kwa wanafunzi 120,000. Hivyo tunaona kuwa wanafunzi wameongezeka na pesa ikapungua. Takwimu hizi ni kutokana na habari iliyowekwa katika tovuti ya bbc.com/ swahili news.

Katika ugawaji wa pesa hizi hutolewa kwa asilimia , wapo wanaopata 100% , wengine hupata 99%, wengine hupata 80% ila pia wapo wanaopata 3% hadi asilimia moja. Anaepata asilimia moja yeye huwa na uhakika wa kupata fedha ya kujikimu (boom) ila ada hujilipia yeye mwenyewe.

Na ada ya chuo kikuu cha Serikali kwa ngazi ya shahada ni 1200000 hivyo mwanafunzi anayetoka katika familia duni kabisa ambae amepata mkopo 1% na anapokea fedha ya kujikimu tu shilingi 500,000 hatoweza kujikimu na kulipa ada kwa shilingi 500,000 inayokuja kila baada ya miezi miwili, matokeo yake wengi hawaji vyuoni walipochaguliwa na hata wakifanikiwa kufika basi asilimia kubwa hawamalizi masomo yao kutokana na maisha kuwa magumu na ugumu wa kulipa ada kwa ujumla. Hivyo lengo la kutoa mkopo ili kuwasaidia linakuwa halijafanikiwa kwa asilimia zote.

Ushauri wangu kwa Serikali ya Tanzania hususan mamlaka husika ni kua; Kwanini Serikali isijikite zaidi katika kuwalipia ada zaidi wanufaika wote wa mkopo ili wawe na uhakika zaidi wa kupata elimu na wao wanufaika wabaki na jukumu la kujikimu kimaisha.

Pia hii ingepunguza usumbufu wanaopata wanafunzi kwa kuhama vyuo hasa kutoka vyuo vya binafsi kwenda vya serikali , kama watalipiwa ada bas wanafunzi hawa watakwa na uwezo wa kusoma chuo chochote bila kubagua kwamba hiki binafsi au hiki ni cha Serikali.

Pia kuna kundi la wanafunzi ambao wao hufika chuoni na kujisajiri na punde baada ya kuanza masomo wao huacha chuo na kuwa anakuja kuchukua fedha za kujikimu bila kusoma na kwa wakati huo huo anakua analipiwa ada. Endapo angekua analipiwa ada tu kwa asilimia kubwa sana angetimiza jukumu lake la kusoma na hatokuwa na sababu ya kuacha masomo yake. Kwa kiasi kikubwa swala hili lingepunguza hilo swala na kwa njia moja au nyingine wangelimaliza kabisa kwa ujumla

Swala hili la kuwalipia ada wanufaika wote wa mkopo lingesaidia katika kurejesha nidhamu ya fedha miongoni kwa wanafunzi kwasababu kumeibuka wanafunzi wanaoishi maisha ya anasa kama ulevi, matumizi mabaya ya fedha kutokana na kuwa na uhakika wa kupata fedha za kujikimu za uhakika endapo wanufaika hawa watakua wanalipiwa ada basi fedha zao za kujikimu wangetumia kwa nidhamu. Lile neno ambalo wanafunzi wamekuwa wakilitumia la "fedha za shetani" halitokuwepo tena.

Kwa njia moja au nyingine hili jambo litarudisha imani za Watanzania kwa bodi ya mikopo na wanafunzi hasa wanufaika kwa ujumla

Jambo hili pia litaongeza uwajibikaji uwajibikaji wa mzazi kwa mtoto wake kwa sababu wazazi wamekuwa na tabia ya kuwaacha wanafunzi pale wanapotambua kuwa wameweza kupata mkopo. Endapo hilo litafanyika basi wazazi wataendelea kuwajibika vizuri kwa watoto wao kwa kipindi chote watakachokua masomoni na atawajibika kwa chochote kikubwa au kidogo atakachokua anapata.

Ni kheri mtu ahangaike kutafuta shilingi laki moja ya kula na kujikimu kwa Mwezi kuliko kuhangaika kulipa shilingi milioni moja na laki mbili ya ada kwa mwaka mzima.

Hii kwa njia moja itaongeza motisha na hali ya kusoma kwakuwa mtu atasoma akitambua kuwa ada yote imelipwa na jukumu lililobaki ni yeye kujikimu binafsi, wanafunzi wengi zaidi watafanikiwa kupata ujuzi na watalazimika kutafuta ajira na hapo Serikali itapata urahisi wa kufatilia madeni yao, itapunguza idadi wa wanaoacha chuo kwa sababu ya kukosa ada (university dropouts).

Pia itapunguza kwa kiasi kikubwa wale wanafunzi ambao hawasomi na lengo lao hua ni kufanya ela ya mkopo kama mitaji ya biashara na badae wao hugeuka wadaiwa sugu.

Hata kwa hali ya kawaida mtu hupata amani hasa mwanafunzi anapotambua ada yake imelipwa na jukumu lake ni kusoma na pia itaondoa matabaka baina ya wanufaika kua huyu amepata asilimia 100% na mwingine ana asilimia 1%.

Ushauri huu ni kwa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania hasa kwa mamlaka husika ambayo ni bodi ya mikopo( HESLB). Pia nichukue nafasi hii kuipongeza mamlaka hii kwa jitihada zake zote ambazo imefanya na hakika inastahili hongera. Nafahamu ushauri huu utahitaji muda katika utekelezaji wake na haya ni mawazo yangu binafsi nikiwa nimesoma chuo japo sikua mnufaika wa mkopo ila kwa kiasi kikubwa na kwa umakini nimeweza kuchunguza hili na kubaini kuwa kuna mabadiliko yanahitajika katika huu mchakato wote. Kutokana pia na uchumi na hali ya nchi yetu ni ngumu kuwalipia ada na pesa za kujikimu wanufaika wote kwa usawa hivyo endapo watalipiwa wote ada zoezi hili lingekuwa na manufaa makubwa sana.

ALMAS JOHN MDAKI
 
Wanufaika wapya wa Mkopo zaidi ya elfu 20 HESLB 2022/2023 | Majina ya Waliopata Mkopo
Habari njema kwa waombaji wote wa mkopo wa HESLB, Allocation ya mkopo bechi ya kwanza sasa inapatikana mtandaoni kuangalia allocation ya mkopo Tembelea Tovuti ya HESLB ya Maombi ya Mikopo na Mfumo wa Usimamizi https://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/Olas

Nifanye nini nikikosa mkopo kwenye bechi ya kwanza HESLB?
Kuwa mvumilivu na subiri kwa sababu bodi ya mkopo inatoa majina ya waombaji wa mkopo waliopata mkopo kwa Bechi. Bechi za majina ya waliopata mkopo ni nyingi wakati mwingine hufikia tano au sita

Je nikisubiri hadi bechi zote za majina zikatoka na ikiwa sioni jina langu, nifanye nini?
Bodi ya mikopo hufungua dirisha kwa waombaji kukata rufaa kwa hivyo ikiwa unajiona kuwa una hoja, unaweza kukata rufaa
Je, nifanye nini ikiwa sipati mkopo baada ya kukata rufaa?
  • Lipa ada ya masomo na chakula cha kujifadhili na gharama za malazi.
Naweza kuomba mkopo huku nikiendelea na masomo?

  • Ndio mwaka ujao bodi itafungua dirisha jipya la maombi
Maswali baadhi ambayo naweza kukupa msaada angalau wa majibu kuendena na uelewa wangu
Je, iwapo nilikatisha(disco) masomo nifanye nini ili niweze kupata mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) Soma hapa

Je, ni lazima nifuate taratibu gani ili nilipwe mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB)?

Ili bodi ifanye malipo, mnufaika lazima afuate taratibu hizi

1. Mfadhiliwa lazima ajiandikishe kikamilifu katika taasisi ya elimu ya Juu, vinginevyo itamfanya akose sifa ya kupokea fedha hizo.

2. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) lazima ipokee maelezo ya ziada ya wanufaika. Jukumu la kutuma taarifa hizo ni la taasisi ambayo wamekubali Wanufaika na kuwasajili kikamilifu.

Nyongeza:

iwapo mnufaika wa mkopo atajiandikisha katika taasisi ya elimu ya juu ambayo ni tofauti na ile ambayo TCU ilipeleka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), mnufaika hatapokea fedha za mkopo hadi aombe kupangiwa upya au Kuhamishiwa mkopo.

Ikiwa mnufaika atabadilisha programu yake aliyoichagua awali, kiasi cha mkopo wake hakitabadilika hadi aombe kutengewa tena.

Mwisho, bodi ya mikopo Huendelea kufuatilia maendeleo ya mnufaika katika Vyuo vya Elimu ya Juu mara kwa mara ili kufanya uamuzi wa malipo.

Recomended Posts

 
Back
Top Bottom