Unajua internet ni (web) kama ile nyumba ya buibui au barabara
Kwahiyo kutoka kwangu signal inaweza ikapita kwenye mkonga then satellite then mkonga then satellite then ndio inafika kwako.., inategemea na traffic jams (mfano wa magari kwenye barabara, Kufika Pugu kuna njia zaidi ya moja) kwahiyo hizi zote zitakuwa interconnected kama barabara zilivyo connected zote.., uzuri kwa sasa badala ya signal kutoka marekani kuja africa kutumia satellite peke yake, sasa kutakuwa na huu mkonga
Hata hiyo modem yako ya Zain/Zantel/Tigo..., signal inaweza ikatoka kwako kwa njia ya satellite mpaka huko kwa hao Zain/Zantel/Tigo (Gateway) ambapo hapo kutakuwa kuna barabara nyingi (Mikonga na Satellite) kupeleka signal yako inapokwenda.
Pia kumbuka hata ukituma Picha ili ifike kwangu hiyo picha inavunjwa vunjwa kwenye pcs ndogo ndogo alafu hizo pcs (pkts) zinatumwa kwa njia tofauti alafu zikifika kwangu browser yangu inazikusanya zote na kuziunganisha ili nipate full picha.., kwahiyo huenda pua ya picha ilipitia njia ya mkonga then satellite wakati sikio lilipita kwenye satellite peke yake.