Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Hapa naweza kusema ni kama imetoka oda fulani kwa watumishi wote wa Umma.
Na kuwaza kwa ndani kabisa inawezekana ikawekwa lokoo watakapiga kura na wasio piga kura halafu wasiopiga kura kitawalamba!
=================
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amewahamasisha watumishi wa umma kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
"Nawaomba wenzangu watumishi wa umma tujitokeze kwa wingi siku ya Oktoba 29 kwenda kupiga kura huu ni wajibu wetu wa kikatiba na njia ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya nchi yetu," alisema Mkomi.
Akizungumza katika kikao cha tatu cha Baraza la Nane la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili, Mkomi alisema licha ya kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, ana mapenzi na ustawi wa taifa, hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura, hasa watumishi wa umma, kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia.