Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Lembeli aliacha kazi TANAPA akakimbilia ufisadini na sasa unamrudi tartiibu. Doctor the Presida come 1/11/2010
Mwenzake Dk Mlingwa yamemfika. Alikuwa Mkurugenzi wa TAWIRI,akakimbilia siasa, miaka mitano katemwa (Shinyanga mjini). Sasa hivi sijui yuko wapi?
Mambo ya siasa bwana, we acha tu!
Alisema watu ni masikini sana wilaya hiyo pamoja na kwamba wanakalia eneo la migodi miwili mikubwa ya dhahabu – Bulyanhulu na Buzwagi. Alishangaa kwa nini kila mgodi katika hiyo inachangia sh milioni 200 tu kila mwaka kwa hakmashauri ingawa kila mmoja unapishana katika uzalishaji.
Alisema tofali moja (gold bullion) la tofali la dhahabu lingeweza kusomesha watoto wa wilaya hiyo bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.
Alimshambulia JK kwa kutoa ahadi za uongo zisizokuwa na mantiki. Alisema JK anapotoa ahadi kwamba atatengeneza barabara anadanganya tu, kwani kazi ya serikali ni kutengeneza barabara kwa sababu ndiyo inakusanya kodi. Alishangaa kuona kwamba JK anaifanya hiyo kuwa ahadi ya kampeni. Slaa alisema hivyo huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.
Asante kwa taarifa nimeambiwa pia leo anaunguruma shinyanga mjini Mbele ya MWASISI wa CHadema Bob Nyanga Makani.
Mwenzake Dk Mlingwa yamemfika. Alikuwa Mkurugenzi wa TAWIRI,akakimbilia siasa, miaka mitano katemwa (Shinyanga mjini). Sasa hivi sijui yuko wapi?
Mambo ya siasa bwana, we acha tu!
Heshima kwako Nyumbu,
Mkuu Mlingwa ni rafiki yangu wa karibu sana tangu akiwa mkurugenzi TAWIRI.Kwasasa Mlingwa yuko Njiro[Msolla] nyumbani kwake anasoma magazeti tangu asubuhi mpaka jioni mambo yake si mabaya sana ana Landrover moja anaitumia kwa shughuli za utalii si unajua tena Arusha watalii wengi kipindi hiki.
Mlingwa anategemea kujiunga Sokoine University kama mwalimu mwakani uongo mbaya elimu yake nzuri hawezi kulala njaa lakini inataka moyo from deputy minister hadi mwalimu !,siasa wakati mwingine inaweza kukuangusha vibaya hadi mbwa unaowafuga wakakudharau.
1st post updated with photos from Kahama/Nzega