Mangi merry
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 221
- 41
Mara kadha nimekuwa nikijiuliza, kwanini Watu wa Maeneo yaliyokaliwa na mkoloni mwarabu hasa wale waliofuata utamaduni wa mkoloni mwarabu huwa hawafanyi vizuri kielimu!? Kisha nikapata majawabu kadhaa ambayo haikuwa rahisi kujua kama kweli yalikuwa sahihi au lah, majawabu hayo ni kama yafuatayo:
(i) mkoloni huyu hakutoa fulsa za kielimu kwa watu aliowatawala.
(ii) lifestyle ya huyu mkoloni inakinzana na elimu inayotolewa nchini hivyo watu wanaoiga lifestyle yake wanafeli mitihani.
(iii) uongozi uliofuata baada ya mkoloni mwarabu haukutoa fulsa za kielimu maeneo aliyoyakalia.
Tathmini yangu alikolezwa na habari niliyoisoma katika gazeti la Mwananchi kama inavyoonekana hapo chini.
KUTOKANA na mfumo wa elimu
ulivyo, mitihani hasa ile ya taifa,
ndicho kipimo kikubwa cha
kiwango na maendeleo ya elimu
nchini.
Ingawa baadhi ya wadau wa elimu
wamekuwa wakishauri mitihani
isiwe kipimo pekee cha elimu, bado
mfumo tulionao unatutaka
kuwapima wanafunzi kupitia
nyenzo ya mitihani pekee.
Kwa kipimo hicho, ni wazi kuwa
mikoa iliyo Pwani na Kusini mwa
nchi hii, ina tatizo la msingi katika
utoaji wake wa elimu.
Sote ni mashahidi kuwa, katika
mitihani wa kidato cha nne
uliofanyika mwaka 2011, shule nane
kati ya 10 zilizovuta mkia kitaifa,
zilitoka katika mikoa ya Pwani nat
Tanga
Kwa mujibu wa matokeo hayo, shule
hizo zilizokuwa na watahiniwa
zaidi ya 40, zilikuwa Bwembwera,
Pande Darajani, Mfundia, Zirai,
Tongoni (Tanga), Maneromango na
Kibuta (Pwani).
Kama hiyo haitoshi, matokeo ya
mtihani wa kidato cha pili
uliofanyika nchi nzima mwaka jana,
unaonyesha kuwa shule zilizofanya
vibaya zaidi kitaifa zinatoka ukanda
wa Kusini.
Shule hizo ni Kinjumbi, Miguruwe,
Njinjo, Mbembaleo, Marambo,
Mihambwe, Jinduma, Kiroma,
Luagala Napacho na Litipu.
Aidha, matokeo ya mtihani wa
kidato cha nne yalitoka wiki iliyopita
yanaonyesha namna shule za mikoa
hiyo zilivyofanya vibaya.
Kwa mujibu wa matokeo hayo,
orodha ya shule kumi za mwisho
inajumuisha shule nane zinazotoka
mikoa hiyo.
Shule hizo zenye watahiniwa zaidi
ya arobaini ni Mibuyuni (Lindi),
Ndame (Unguja), Namndimkongo
(Pwani), Chitekete (Mtwara),
Kwamndolwa (Tanga), Kikale
(Pwani), Mkumba na Tongoni
(Tanga).
Kwa mtu mdadisi wa mambo,
lazima ajiulize kwa nini shule
zinazotoka katika ukanda mmoja
ziwe nyingi katika kundi hilo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Philip Mulugo, anadhani
hali hiyo inasababishwa na uhaba
wa walimu jambo linalomfanya
asema kuwa mwaka huu Serikali
itapeleka walimu katika eneo hilo.
(i) mkoloni huyu hakutoa fulsa za kielimu kwa watu aliowatawala.
(ii) lifestyle ya huyu mkoloni inakinzana na elimu inayotolewa nchini hivyo watu wanaoiga lifestyle yake wanafeli mitihani.
(iii) uongozi uliofuata baada ya mkoloni mwarabu haukutoa fulsa za kielimu maeneo aliyoyakalia.
Tathmini yangu alikolezwa na habari niliyoisoma katika gazeti la Mwananchi kama inavyoonekana hapo chini.
KUTOKANA na mfumo wa elimu
ulivyo, mitihani hasa ile ya taifa,
ndicho kipimo kikubwa cha
kiwango na maendeleo ya elimu
nchini.
Ingawa baadhi ya wadau wa elimu
wamekuwa wakishauri mitihani
isiwe kipimo pekee cha elimu, bado
mfumo tulionao unatutaka
kuwapima wanafunzi kupitia
nyenzo ya mitihani pekee.
Kwa kipimo hicho, ni wazi kuwa
mikoa iliyo Pwani na Kusini mwa
nchi hii, ina tatizo la msingi katika
utoaji wake wa elimu.
Sote ni mashahidi kuwa, katika
mitihani wa kidato cha nne
uliofanyika mwaka 2011, shule nane
kati ya 10 zilizovuta mkia kitaifa,
zilitoka katika mikoa ya Pwani nat
Tanga
Kwa mujibu wa matokeo hayo, shule
hizo zilizokuwa na watahiniwa
zaidi ya 40, zilikuwa Bwembwera,
Pande Darajani, Mfundia, Zirai,
Tongoni (Tanga), Maneromango na
Kibuta (Pwani).
Kama hiyo haitoshi, matokeo ya
mtihani wa kidato cha pili
uliofanyika nchi nzima mwaka jana,
unaonyesha kuwa shule zilizofanya
vibaya zaidi kitaifa zinatoka ukanda
wa Kusini.
Shule hizo ni Kinjumbi, Miguruwe,
Njinjo, Mbembaleo, Marambo,
Mihambwe, Jinduma, Kiroma,
Luagala Napacho na Litipu.
Aidha, matokeo ya mtihani wa
kidato cha nne yalitoka wiki iliyopita
yanaonyesha namna shule za mikoa
hiyo zilivyofanya vibaya.
Kwa mujibu wa matokeo hayo,
orodha ya shule kumi za mwisho
inajumuisha shule nane zinazotoka
mikoa hiyo.
Shule hizo zenye watahiniwa zaidi
ya arobaini ni Mibuyuni (Lindi),
Ndame (Unguja), Namndimkongo
(Pwani), Chitekete (Mtwara),
Kwamndolwa (Tanga), Kikale
(Pwani), Mkumba na Tongoni
(Tanga).
Kwa mtu mdadisi wa mambo,
lazima ajiulize kwa nini shule
zinazotoka katika ukanda mmoja
ziwe nyingi katika kundi hilo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Philip Mulugo, anadhani
hali hiyo inasababishwa na uhaba
wa walimu jambo linalomfanya
asema kuwa mwaka huu Serikali
itapeleka walimu katika eneo hilo.