Mto_Ngono
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 686
- 589
Nilipokumbuka ile hadithi ya kibanga kampiga mkoloni nikajiuliza kwa nini hakummaliza kabisa. Yapo mambo mengi katuletea au kuyafanya ambayo ukiyaangalia kwa nje ni mazuri kumbe yana ubaya sana hasa katika kutudhoofisha kimwili na kiakili. Nadhani tunamkumbuka sana mkoloni hadi kuona anafaa kuweka katika vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwavuta watu karibu.
Suala moja tu ambalo najiuliza ni kwa nini katika project kubwa za ujenzi (haswa mall n.k) mabango mengi yanayoonesha picha ya jengo litakapokamilika hupambwa na wazungu!! picha katika mabango hayo huonesha watu kuingia na kutoka lakini watu hao wengi huwa ni rangi ya mkoloni. Hatuwezi kuweka watu kufanana na rangi zetu au hatujui thamani yetu na ya rangi yetu hadi tuwaweke wao ndani ya taifa letu!!
Please, wachora ramani badilikeni basi angalau tuone rangi zetu pale sio wakoloni tu. Wakoloni wabaya sana.