Mkoloni alituweka katika mgawanyiko wa makundi nasi tumejiweka katika matabaka

nkulikwa

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
721
813
Wakati wa ukoloni tuliweka katika makundi ya Watu weusi, weupe na waasia; baada ya kuanza kupigania uhuru kukawa na kundi lingine la wanaopinga serikali! Sheria mbali mbali zikaundwa kuwaweka ndani wapigania uhuru baadaye tukapata uhuru wa bendera, lakini hatukuondoa tabia za kikoloni. Tunawachukia wakoloni na kulaani kututawala lakini kitabia tunafanana nao!
Kwa mfano viti vya bunge ni vya wabunge wote, nini kinatufanya kuvigawa katika makundi, ati hapa watakaa wabunge wa Chama tawala na huku wapinzani. Ni tabia za kubaguana, ni kula nyama ya mtu. Wabunge walifaa wakae pamoja kwa kuchanganyika Maana wote ni wabunge na wote ni Watanzania! Nchi tunayopenda umoja na mshikamano. Matokeo ya kukaa katika vikundi tofauti ni kuendeleza uchama badala ya kujadili mambo ya nchi kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom