Mkojo hurutubisha ngozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkojo hurutubisha ngozi

Discussion in 'JF Doctor' started by Rutashubanyuma, Apr 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Mkojo hurutubisha ngozi
  [​IMG]

  Haji Kalili ​

  [​IMG] ZIPO hadithi nyingi za kale zinazoelezea matumizi ya mkojo wa binadamu na baadhi ya wanyama kwamba ni tiba mbadala.
  Wapo watu waliokuwa wakitumia tiba mbadala hiyo kupata nafuu au kupona kabisa maradhi tofauti yaliyokuwa yakiwasumbua.
  Hadithi iliyopokewa na Imamu Bukhari, mmoja wa wasaidizi wa Mtume, inaeleza kwamba baadhi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kwamba unywaji wa mkojo wa ngamia ni dawa.
  Katika hadithi nyingine ya Bukhari, Volume 7, kitabu cha 71, Ukurasa nambari 590: “ Anasimulia Anas: Hali ya hewa ya Medina enzi ya Mtume Muhammad (SAW), ilikuwa haiwakubali baadhi ya watu, kwa hiyo Mtume aliwaamuru kufuata muongozo alioutoa wa kunywa maziwa na mkojo wa ngamia kama tiba.
  Walimtii na kuanza kunywa maziwa na mkojo wa ngamia hadi afya zao ziliporekebishika.
  Katika hadithi nyingine ya Bukhari Volume 8, Kitabu cha 82, namba 797:
  “Anas Ibn Malik, anaendelea katika volume 8, kitabu cha 82 ukurasa namba 797: Kulikuwa na kundi la watu kutoka ukoo wa kikuraishi (au ‘Uraina’) walikuja Medina na wakaugua, Mtume Muhammad aliamuru watibiwe kwa maziwa na mkojo wa ngamia. Afya zao zilirudi kama zilivyokuwa awali.
  Katika mapokeo mengi kutoka kwa Bukhari na baadaye waandishi wengine tofauti tofauti, iligundulika kwamba mkojo ni tiba iliyokuwa ikitumika katika baadhi ya jamii nyingi zilizopita na katika miaka ya hivi karibuni kuna baadhi ya watu wameanza kutumia tiba hiyo ingawa si kwa kiwango kikubwa.
  Tamaduni nyingine zinavyoitafsiri tiba hiyo
  Nchini China, mkojo wa watoto wadogo unachukuliwa kama tiba mbadala.
  Kusini mwa Uchina, watoto wachanga wanaoshwa uso na mkojo ili kuipa ngozi kinga kutokana na mionzi mbalimbali mara wanapozaliwa.
  Nchini Ufaransa, kuna aina fulani ya soksi inayotumbukizwa kwenye mkojo na kuzungushwa shingoni mwa binadamu kama njia ya kurekebisha mwenendo wa koo.
  Mnamo karne ya 17, kulikuwa na aina ya kabila la wanawake wenye kipato kikubwa wa Kifaransa waliokuwa wakioga kwa kutumia mkojo ili kujiongezea mvuto.
  Katika mji wa Sierra Madre, ulioko Mexico, wakulima huwa wanaandaa mchanganyiko wa mifupa ya wanyama na mikojo ya watoto, na baadaye hujipaka mchanganyiko huo kwenye ngozi kama tiba mbadala ya kurutubisha ngozi na kuikinga na magonjwa.
  Kwa wakazi wa kale katika Jiji la Roma, Italia, mkojo ulikuwa ukitumika kung’arisha meno, hata kama utatumika mkojo ambao si wako.
  Mwandishi John Henry Clarke wa jarida moja nchini Marekani aliandika, “…binadamu ambaye ngozi yake imeathirika, anywe mkojo wake wa kwanza anapoamka asubuhi.
  “Kama dalili zinaonyesha ameathirika sana na amekuwa dhaifu, mkojo utamsaidia kurudi katika hali yake ya awali”.
  Historia inatukumbusha kwamba tiba mbadala ya mkojo imetumika sana nchini China miaka ya nyuma.
  Watabibu wa kale wa Kichina walitibu majeraha kwa kutumia mikojo kwa kumwagia kwenye vidonda vipya na utabibu huo inaelezwa ulienea kwa haraka
  Mashariki ya Mbali.
  Mkojo pia unarahisisha usagaji wa chakula unaponywewa mapema asubuhi.
  Una virutubisho gani?
  Watumiaji wa tiba mbadala ya mkojo wanasema yanapatikana maji na urea ndani yake. Mkojo pia una mamilioni ya chembechembe za homoni, metaboliti na corticosteroidi.
  Mkojo pia una virutubisho vingine vingi kama Vitamini C.
  Katika simulizi tofauti tofauti inaelezwa kuwa mkojo na urea kwa wanaotumia kama tiba mbadala inasaidia kupunguza maambukizi ya saratani mwilini.
  Vimelea vya kansa vinaweza kusafirishwa kwa njia ya mkojo, sasa kwa kutumia mkojo kama kinywaji, vimelea hivi vinaweza kuingia kwenye mfumo wa kinga mwilini na kusaidia urutubishwaji wa kinga mwilini ‘(antibodies)’.
  Ushahidi wa watumiaji
  Mwaka 1978, aliyekuwa Waziri Mkuu wa India, Morarji Desai, mmoja wa watumiaji wa muda mrefu wa tiba mbadala hii, katika mazungumzo yake na mwandishi Dan Rather katika dakika 60 alielezea faida walizozipata mamilioni ya Wahindi waliojitibu kwa tiba mbadala hiyo.
  Mcheza filamu wa Kiingereza, Sarah Miles, alikunywa mkojo wake kwa zaidi ya miaka 30 akiamini kwamba unamsaidia kujenga afya siku hadi siku.
  Mcheza baseball Moisés Alou, alikuwa akiikojolea mikono yake akiamini itamsaidia kutoteleza kwenye mpira mara anapoukamata.
  Mwanamuziki Lady Madonna yeye akihojiwa katika kipindi cha ‘Talk Show’ alielezea jinsi alivyoweza kujitibu majeraha ya miguuni mara anapomaliza kufanya mazoezi ya kukimbia.
  Mpiganaji wa michezo tofauti (Mixed Martial Arts), Lyoto Machida, alikiri katika mahojiano kwamba anakunywa mkojo wake.
  Mwanamasumbwi Juan Manuel Marquez alikuwa akinywa mkojo wake wakati akijiandaa na mpambano baina yake na Floyd Mayweather.
  Mchezaji bingwa wa taekwondo wa Marekani, Adam Paolino, naye ni mtumiaji mzuri wa mkojo wake akiamini unamsaidia kutibu majeraha anayoyapata akiwa mazoezini.
  Ushauri kuhusu tiba hii
  Inashauriwa unapoamka asubuhi kabla ya jua kutoka, unaweza ukanywa japo glasi moja ya mkojo, inasaidia kuimarisha afya.
  Wahindu wa kale walishauri unywaji wa mkojo kabla ya jua kutoka kama njia moja ya kuimarisha afya mwilini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Ushauri kuhusu tiba hii
   Inashauriwa unapoamka asubuhi kabla ya jua kutoka
  unaweza ukanywa japo glasi moja ya mkojoinasaidia kuimarisha afya.
     
  Wahindu wa kale walishauri unywaji wa mkojo kabla ya jua kutoka kama njia moja ya kuimarisha afya mwilini.
  Uchafu uliochujwa na figo urudishwe kwenye figo zile zile madhara yake ta muda mrefu ni kuaathirika kwa figo hizo kwa kuzidiwa na uchafu.......................................tupime faida na hasara kwa sababu virutubisho tajwa vyaweza kupatikana kwa njia nyingine katika vyakula......then the big question becomes why risk your renal failure?
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Fyi mkojo sio uchafu ni pure
   
 4. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Please! Wataalam naomba tufafanulieni ili vizuri ili wengine tuanze kujinywea tupate hizo faida.
  Ni kweli mkojo ni tiba au kinga dhidi ya magonjwa?? Na je ni magonjwa yepi??
  Tafadhari wataalam wa afya zetu msikae kimya katika hili, please please!!.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Tatizo lao ni kwamba they will never tell you the truth because taht is their business. Wakikuambia mkojao unaweza kukutibu ugonjwa fulani si hutanunua tena dawa? Ili upate dawa si lazima wakupime n.k Madaktari na mafamasia hawatakaa wakuambie cho chote kuhusu tiba mbadala. Hata ukiwaambia maji ni dawa watakuambia shit .

  Wewe jisomee hapahttp:

  http://www.lifepositive.com/body/traditional-therapies/urine-therapy.asp
  Urine Therapy

  http://www.lifepositive.com/body/traditional-therapies/urine-therapy.asp
   
Loading...