Mkoani Katavi, askari wa TAWA wamedaiwa kumpiga mtu mmoja na kumsababishia umauti

Gilbert Julius

Senior Member
Jan 28, 2014
102
72
Huko wilaya ya Mlele Mkoani Katavi askari wa TAWA wamedaiwa kumpiga mtu mmoja na kumsababishia umauti baada ya kumkuta porini.

Baada ya kumpiga vibaya wakampeleka kituo cha polisi cha Inyonga wilayani Mlele.

Walivyoona atawafia kituoni wakampeleka hospital kupoteza ushahidi. Yaani mtu amefia njiani kutoka polisi kwenda hospital.

Walipofika hospital wakasema wamemuokota porini.

Jinsi maiti inavyozidi kukaa inavimba upande mmoja wa tumbo. (Mateke).
 
Inasikitisha yaani wamemkuta porini wamempiga binaadamu tukipewa na mamlaka utu unatoweka
 
Shida asee majangili nao ni ishu mno. Huwa battle za majangili nazo si mchezo kwa askari wa Tawa. Wanaviziana mnooo!

Siungi mkono lakini kuuwana
 
Huko wilaya ya Mlele Mkoani Katavi askari wa TAWA wamedaiwa kumpiga mtu mmoja na kumsababishia umauti baada ya kumkuta porini.

Baada ya kumpiga vibaya wakampeleka kituo cha polisi cha Inyonga wilayani Mlele.

Walivyoona atawafia kituoni wakampeleka hospital kupoteza ushahidi. Yaani mtu amefia njiani kutoka polisi kwenda hospital.

Walipofika hospital wakasema wamemuokota porini.

Jinsi maiti inavyozidi kukaa inavimba upande mmoja wa tumbo. (Mateke).
tawa ni kawaida yao. shida huwa wanataka kuonyesha kwamba na wao walienda depo,kumbe ni raia wakakamavu tu. unampigaje mtu ambaye tayari umemuarest?
 
Kwanini ni wakatili hivyo ? Au ndio sifa za jeshi usu ?
Mambo ya maliasili na nyara za serikali huenda wanachoshwa na matukio ya kujirudia rudia, na hivi wamejengwa kuwa aggressive haijalishi umepotea njia wakikukuta kwenye mamlaka zao wanakuachaje salama. Labda ukutwe na burungutu la dollar mfukoni wakunyang'anye wakutie makofi uende zako.
 
Back
Top Bottom