Mkoa wa Mtwara unafaa kuishi na biashara?

Mkoa wa Mtwara unafaa kuishi na biashara?

hahaaaaa nimecheka peke yangu, Mtwara nilikuwa naenda late 2000s kwa sibling na baadae kahama kauza na nyumba but iringa nimeenda siku nyingi hayo ndio nayasikia kwako. Labda nikuulize bado unaamini ushirikina kama kikwazo direct kwa biashara au ni indirectly kwa kuifisha maana mie nadhani wakazi washirikina hawana maendeleo na wana effect kubwa kwako hata familia kuliko wanaoutumia kwa biashara ie utapanga/kuishi nao jirani, utanunua vyakula na mahitaji kwao lakini hao wapinzani ni kila mahali sema njia tofauti na ushirikina naona ni issue ndo kama unaamini.
Hapo Mama Joe umechemka ndugu yangu, ni Heri aende Mtwara kuliko huko unakomwambia aende, huko wenyeji ni wajanja kuliko na hawataki mgeni aingize ushindani kwenye biashara zao, hawachelei kumpiga kipapai, labda apeleke biashara mpya kabisa ambayo wao hawaijui, lakini sjui aende kuuza hardware, sijui ajenge hotel wale ndugu zangu wana ukabila wa kuzidi mpaka wanabore! Mtwara ya sku hizi inafunguka sana, na ni sehemu yenye fursa mpya kwa mtu anayeanza ni nzuri zaidi ushindani mdogo na hivyo ni rahisi kukita mizizi kuliko hiyo mikoa mikubwa, labda aingie na mtaji mkubwa sana, hasa kwenye kilimo na ufugaji.
 
Mama Joe ushirikina upo wa aina nyingi, hata chuki binafsi, ukabila vyote hivyo ni ushirikina. Hebu rudi tena Iringa, uende mpaka Njombe ukafanye research ya kizushi uangalie wamiliki wengi wa biashara za hardware na general store ni watu wa wapi!! Njombe nzima ukihesabu wafanyabiashara wa kichaga waliofanikiwa sidhani kama wanazidi wawili!!!....Sehemu akishindwa mchagga na mhindi iangalie mara mbili!
 
Last edited by a moderator:
sehemu ambapo mpemba na mchaga hawapo hapafai kuishi

Are u sure hakuna wapemba na wachaga? Kwa taarifa yako matajiri wa mtwara ukimtoa Murji tajiri kwa vile mbunge wengine wote na maarufu ni wachaga na ndo wamiliki wa bar na hoteli nyingi.
 
Sasa hapo kwa Wachagga umekosea labda wapemba sawa na labda Njombe but nimekulia Iringa nikihesabu schoolmate na majirani zangu wachagga ni nusu/50% na walikuwa wafanyabiashara nakumbuka hata kuku wa kisasa tulijifunzia kwao. Ila kiukweli pia waking wameshika biashara nyingi zaidi hadi tunaondoka unaweza kuwa sawa. Kilichonivunja moyo Mtwara kwa biashara ndogondogo yaani mzunguko wa hela hamna kila kitu wanakopa kipindi hicho hata wahindi wanakopesha viatu, nguo kwa kubandika! just imagine....
Mama Joe ushirikina upo wa aina nyingi, hata chuki binafsi, ukabila vyote hivyo ni ushirikina. Hebu rudi tena Iringa, uende mpaka Njombe ukafanye research ya kizushi uangalie wamiliki wengi wa biashara za hardware na general store ni watu wa wapi!! Njombe nzima ukihesabu wafanyabiashara wa kichaga waliofanikiwa sidhani kama wanazidi wawili!!!....Sehemu akishindwa mchagga na mhindi iangalie mara mbili!
 
Anachosema Mama Joe ni sahii kabisa

Mimi ninaishi Mtwara huu ni Mwaka wa 6, mtwara ukianzia Mitaani mpaka katika biashara za maduka ni Ushirikina Mtupu. Jamii ya Mtwara imeweka mbele ushikina kuliko kazi.

kama Jamaa ana nia ya kufanya biashara hii ya kawaida Mabanda (frame) ya biashara kodi kwa Mwezi ni kati ya TSh 100,000 hadi 200,000.

Kama mtu ana mtaji na anauwezo wa kupambana na vigagura wa Mtwara biashara ya Hotel au Nyumba za kulala wageni ni nzuri kwani wageni ni wengi wanakuja na nyumba za wageni ni chache. (vigagura siyo ktk biashara tu hata uko mtaani utakako ishi.




Acha kumtisha mwenzako bila sababu, nahisi wewe unaongea kwa imaginations lakini haujafika Mtwara bado.Huo ushirikina unaousemea sijui umeushuhudia wapi. Nimeishi Mtwara Miaka 3 na bado huwa nakwenda huko mara kwa mara lakini huwezi kuniambia ushirikina wa Mtwara unaufikia ule wa kupiga nondo wa Mbeya na Iringa au wa kuua Albino wa Shinyanga.
Kwa miaka ya hivi karibu ni mkoa huu wazi kabisa naona maendeleo yake yanavyokwenda kwa kasi ya ajabu na watu wanamiminika kuinvest huko, kwa miaka michahce sana ijayo mikoa ya Lindi na Mtwara itakuwa populated sana kutokana na ugunduzi wa gesi pamoja na ujenzi wa viwanda kama cha theruji cha Dangote na cha mbolea ambavyo very soon vikishakamilika vinaanza uzalishaji. Hivyo ndugu mleta hoja usitishwe na huyu mdau nakushauri nenda physically ukafanye upembuzi yakinifu wewe mwenyewe uone. Tena nakushauri fanya haraka maana soon viwanja mjini bei yake itakuwa haishikiki sasa hivi tu kukipata lazima ujipange.

Wazo la investment kwenye kilimo cha mboga mboga na mahotel na guest house nakushauri ufanyie kazi kama wadau walivyosema hapo juu hii biashara itakulipa sana. Kuhusu ukarimu wa wamakonde wala usitie shaka ni wakarimu sana sema kupiga mizinga kwao ni kama sehemu ya maisha yao.
 
Anachosema Mama Joe ni sahii kabisa

Mimi ninaishi Mtwara huu ni Mwaka wa 6, mtwara ukianzia Mitaani mpaka katika biashara za maduka ni Ushirikina Mtupu. Jamii ya Mtwara imeweka mbele ushikina kuliko kazi.

kama Jamaa ana nia ya kufanya biashara hii ya kawaida Mabanda (frame) ya biashara kodi kwa Mwezi ni kati ya TSh 100,000 hadi 200,000.

Kama mtu ana mtaji na anauwezo wa kupambana na vigagura wa Mtwara biashara ya Hotel au Nyumba za kulala wageni ni nzuri kwani wageni ni wengi wanakuja na nyumba za wageni ni chache. (vigagura siyo ktk biashara tu hata uko mtaani utakako ishi.



Mkuu Mtwara umeishi maeneo gani? Mimi matukio ya ushirikina sijawahi yasikia hata nashangaa nyie mnayasikia wapi?
 
Kaka Nimeishi Kiangu, Ligula na sasa naishi Shangani

nilishawai fanya mazungumzo na jamaa zangu ambao ni wafanya biashara mitaa ya Bima, uwanja wa Umoja na wale sokoni.

Mkuu Mtwara umeishi maeneo gani? Mimi matukio ya ushirikina sijawahi yasikia hata nashangaa nyie mnayasikia wapi?
 
Mm nipo chuo cha stella maris (SAUT) mpk sasa nina mda wa miaka mitatu bado nipo,katika swala la biashara mtwara bado iko chini maana hawana uzalishaji wwte zaidi ya kutegemea kilimo cha korosho, na ukiangalia mwaka huu bei ya korosho ilikuwa ya shida ,so kila kitu wanategemea mikoa mingine mfano nyanya ,viazi,matunda,mahindi,pilipili,vitunguu,n.k .kiukweli biashara kwa sasa ni ngumu kidogo tofauti na mwaka Jana bei ya korosho ilikuwa nzuri kila kitu kilikuwa kinaenda sawa,na kuhusu ushirikina ,ilo sijalishuhudia ila ni ww mwenye unatakiwa uishi kwa nidhamu maana ushirikina kila sehemu upo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asikudanganye mtu mtwara ni mji mzuri sana kuishi hasa kwa mtu anaefanya biashara aina yoyote .ila sio kwa mkulima! Binafsi niliishi mtwara kwa miaka sita ni wafanyabiashara tu wenye maisha ya uhakika na si wakulima.

Mtwara ni mji wenye maisha ghali sana kuliko arusha isipokuwa tu chumvi na mpenzi manake kwa shiling 500 unapata mpenzi hata kwa mkopo pia hadi utakapo pata . Ukitaka kuoa unatoa elfu 10 hadi 30.

Vitu madukani bei ya juu mno na vinatoka dar na msumbiji.

Viazi vya kutengeneza chips vinatoka dar . Nyama ya ngombe wanakula matajiri .

Kipato cha wananchi wa kawaida ni cha chini mno isipokuwa wachache wenye mashamba ya korosho wanapata nafuu kipindi cha msimu wa korosho.

Wakazi wa mtwara hasa vijana ni wavivu mno hawapendi kilimo isipokuwa wazee wanaolima jembe la mkono mazao kama mihogo mtama mpunga na vijana wachache kwenye uvuvi

Kuhusu Wakazi wa mtwara si wabaguzi ila ni tegemezi mno maana ukifika tu mtwara ukiwa mgeni wazee watakuomba wawe wazazi wako makaka na wadada uwe ndugu yao ili mradi tu unawajali kuwapa 500 ya unga sukari ya msokoto au dagaa
Fursa ya biashara ya mahindi iko vipi mtwara?soko lipo
 
Mtwara imebadilika sana, sana.
Fursa za biashara zipo nyingi tu, kwani wageni ni wengi sana. Sasa hivi Mtwara hakuna hoteli nzuri inayotoa huduma ya chakula, chakula kinapatikana kwa mama ntilie na kwenye mabaa mishikaki na chipsi. Kuna ongezeko la nyumba za kulala wageni lakini bado nyingi hadhi yake ni ya chini. Bado wananchi hawajaona fursa ya kulima mbogamboga na kufuga kuku na mbuzi, bado nyanya zinalimwa nje ya mkoa na kuletwa kwa malori ambazo hazitoshelezi soko. Matunda ni machache sana sokoni hata yaliyopo ni ya kiwango cha chini sana.
[/QUOTE
UMESEMA UKWELI.MIAKA 2008 IKIPITA SAA 12 JIONI CHAKULA VIHOTELINI HAKUNA LABDA UWE NA ODA MAALUMU. Mengine kama matunda ni shida hasa yenye hadhi. Sasa sielewi ukipeleka mazuri bei wataiweza? PILI guest nzuri sasa zipo kiasi ila zile za bei kuanzia elfu 50 zinakosa wateja mara nyingi. Hali ya MTWARA kama isipofanyiwa zoezi maalumu itakuwa jangwa. Ukishamaliza msitu ulioko mkoa wa pwani naa somanga pale lindi kwingine kwenda mpaka mtwara mjini ni vichaka sio misitu. jaribu na wewe hasa kwa vile kuna hiyo gesi.
 
Umesema kweli kabisa na mzunguko wa hela mdoogo sana. Pia bado wanapenda ushirikina. Kwa mgeni tena unayeanza maisha sikushauri uende huko maana unahitaji utaowaajiri wawe wanajituma na kiasi fulani kukutia moyo pia majirani na jamii nzima. Kwa mtu uliyeishi nchi za mchakamchaka utakata tamaa. Kama unapenda kusini nenda iringa, njombe au mbeya kilimo kitakutoa hata biashara kidogo zinafaa na maisha sio expensive.
Huijui Mtwara wewe,unaongea kwa kuimagine
 
Karibu mkuu :
Kuna kwa lipaja
Brother Y
Sisi kwa sisi
Migo migo
Kopa kabana
And other many places which are attractive and enjoyable.
WELCOME:
 
Ndugu zangu
kuna mada inaendelea hapa jamvini kuhusu ushauri wa kurejea Tanzania,wote mliotoa ushauri nawashukuru sana na kwa taarifa tu ni kwamba nimeamua kurejea nyumbani!
sifahamu kuhusu mikoa mingi lakini kwa kuwa nina uwezo wa kuishi maisha yoyote yale ninatamani sana kwenda kuishi mtwara
najua mtwara ni mkoa uliosahauliwa sana na serikali yetu,lakini kwa kuwa kuna watu wanaishi ningependa kujua maisha ya palea yakoje??je wenyeji wa pale wanapenda wageni???je wana nia ya dhati ya kujiletea maendeleo?fursa za biashara zikoje pale??natamani kuijua mtwara!
mtwara bishara yoyote ile inaweza kufanya watu wa kusini in wakarimu sana sijapata kuona
 
Back
Top Bottom