Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,430
- 108,591
Serikali inamuenzi Baba wa Taifa wa vitendo, hakutaka mkoa wako uwe wa kisasa, alipenda ubaki na asili yake ndio maana Nyerere hakupeleka rami Butihama.Ni kweli kwamba baba wa Taifa Hayati Mwl Julius K. Nyerere alikuwa ni mzaliwa wa mkoa huu na ambaye ndiye alikuwa mwasisi mkuu wa TANU na hatimaye CCM. Licha ya hiyo naweza sema kwamba mkoa huu umesaulika sana na katika shughuli za maendeleo ya jamii. Mkoa unakabiliwa na miundombinu mibovu, huduma mbovu za maji, elimu na afya.
Swali langu ni Je mkoa huu umewakosea nini watawala wote waliopita na wa sasa ndani ya serikali ya CCM??
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Nimrod Mkono Buswege amejenga nyumba ya kisasa baada ya Nyerere kufa, hata matajili wa mkoa wa mara wengi hawana spirit ya kuwekeza kwao, sababu kuu ni huyuhuyu mzee mwenye JK Nyerere.
Tatizo la mkoa wa Mara ni ujamaa wa Nyerere msitafute mchawi. Nyerere alihakikisha rami ipo kutoka Mwanza hadi border ya Sirari hilo ndio lilikuwa la msingi kwake lakini mambo mengine alitaka wote muwe wajamaa.
