Mkoa wa Arusha hali ni mbaya

Mkoa wa Arusha hali ni mbaya

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,966
Reaction score
5,559
Hapo vipi,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo chini, mkoa wa Arusha umeendea kusahaulika na kutelekwezwa, awamu hii japo ndio mkoa unaochangia mapato makubwa katika Nchi hii.

Miundo mbinu ndani ya mjini, imegeuka kama mito, chini ya uongozi wa Mrisho Gambo huu mkoa umekuwa na hali mbaya kimaendeleo.

Kuna hii barabara ya kutoka white rose na pale mianzini zimekuwa kama mito ndani ya mjini..

Cha kujiuliza mkoa nyeti Kama mkoa wa Arusha, yenye fursa za kitalii ,makao mkuu ya Afrika Mashariki.. Inatelekezwa hivi kisa hila za kisiasa ,inakuwa haina maana Kwa sababu hauwakomoi watu wa Arusha peke yao ila ni Taifa nzima, kwasababu watalii wanapenda mkoa wenye miundo mbinu nzuri.

Sasa Kama utamzungusha Mzungu kwenye mashimo namna hii, unategemea akirudi kwao atarudi tena au ataenda kumuhamasisha wezio waje watembelee mkoa wa Arusha.

Ni aibu kwa uongozi huu, Embu muache tabia za kimaskini, tufike mahali tuangalie maslahi mapana ya Taifa hili.

Mkoa wa Arusha unatakiwa utuzwe sio kwa maslahi ya watu Wa Arusha ila ni Kwa maslahi ya Taifa.

Leo kinachoendelea hapa Arusha ni siasa za kimaskini za kupokonya mkoa huu fursa na kupeleka mikoa mingine kwa hila.

Leo mikutano ya kimataifa ilifanyika hapa miaka mitano iliyopita , hata Bunge la East Africa sidhani kama bdo waendelea kufanyika hapa.

Juzi wanunuzi na wauza mawe wanaambiwa wasionekane tena mjini, eti waande Namanga, kufanyia biashara ni aibu.

Hivi mtu ametoka na Billioni zake Thailand, unamuambia aende Namanga akalale kwa guest kwa usalama upi.

Kinachoamua centre ya biashara sio maamuzi ya kisiasa ni miundo mbinu za kibiasha ni kimaanisha usalama wa wao na huduma muhimu kwao. Sasa Kama tunafikia pahala pa kuwaamurisha watu kama Ngo'mbe pasipo kukaa na wadau wenyewe ukapokea maoni yao,tafsiri yake hiyo mipango yenu ya kisiasa lazima itakwama au mtaharibu biashara ya madini moja kwa moja.
IMG_20190523_165030.jpg

IMG_20190523_164850.jpg IMG_20190523_164937.jpg IMG_20190523_165030.jpg IMG_20190523_164940.jpg IMG_20190523_164937.jpg
IMG_20190523_164937.jpg
IMG_20190523_164850.jpg
IMG_20190523_164940.jpg
 
Hii inaitwa majungu on making........

Kwa taarifa yako mikoa yote inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na maendeleo hayawezi kugawanywa kwa kuzingatia waliochangia pato hilo kwa wingi kwa mwaka fulani.

Na kwa kipindi hiki cha mvua ni maeneo mengi ya nchi yameathirika na mvua miundombinu imeharibika na hakuna ahaja ya kumlaumu mtendaji mmoja mmoja kwa jambo hili.

Tafakari kwanza kabla ya kundika usiwe na mihemko mkuu

Nikutakie asubuhi njema na sikunnjema katika kutekeleza majukumu yako
 
Hoja unayo ila umeiwasilisha kikudakuda sana,kwani sisi wa Tunduru hatuhitaji barabara nzuri,mbona Iringa wanatulisha,acha kujifanya wathamani kuliko sisi.
Tatizo uelewa wako ni wachini Sana hata nikiongee na ww mpaka kesho, hatutaelewana.
 
Hoja unayo ila umeiwasilisha kikudakuda sana,kwani sisi wa Tunduru hatuhitaji barabara nzuri,mbona Iringa wanatulisha,acha kujifanya wathamani kuliko sisi.
Sijui umetumia kiungo gani cha ajabu kuwaza ila una uhuru wa kutoa hata upumbavu wako kwa watu
 
Declaration of interest.
Mimi nimesoma Arusha, na pia nimeoa Arusha hivyo Arusha nakuja sana, ni kama kwangu, nakiri kwa kweli kabisa, hii hali ni mbaya sana, sikuwahi kushuhudia barabara kama hii maeneo ya mjini kati, labda Ngarenaro, Kijenge ya Juu na Olamatejoo ya enzi hizo.

Ukiambiwa hapa kuna mbunge unaweza usiamini, its so sad and pathetic. Hivi mbunge wa hapa ni nani?. Kuna Barabara za Tarura na za Tanroad, sijawahi kuisikia barabara hii ikizungumzwa popote. Jee mbunge yupo?. Fedha za mfuko wa jimbo anafanyia nini?, maana zinatosha hata kumwaga tuu kifusi.

Hata si mliishaambiwa ili eneo fulani lipate maendeleo mnatakiwa kufanya nini?. Inawezekana Wana Arusha mlifanya makosa sana, ndio maana hali ni hii, sasa ili mpate maendeleo, msirudie tena makosa kama yale ili Arusha irudie ile hadhi yake ya zamani, pia naomba kuwahakikishia, kama mlifanya makosa, mmeisha samehewa, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa.

P
 
Hoja unayo ila umeiwasilisha kikudakuda sana,kwani sisi wa Tunduru hatuhitaji barabara nzuri,mbona Iringa wanatulisha,acha kujifanya wathamani kuliko sisi.
Amesema mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii, uategemewa na taifa Zima. Na wewe wa Tunduru sema huo mkoa taifa linautegemeaje maana naamini mikoa yote ni ya watanzania hakuna mkoa special Ila kila mtu lazima apigie debe anapoishi.
 
Wewe ni mjinga japo kiasi una hoja kwa mbali. Hivi ninyi wakaskazini mna shida gani? Ni fursa gani ilopokonywa Arusha na kupelekwa mkoa mwingine? Mbona mna mambo ya kijinga jinga saana, ukanda unawasaidia nini? Hoja ungeiweka ktk ubovu wa miundombinu tuu ingeeleweka. Kwanza ni mkoa gani umekamilika ktk suala la miundombinu hapa Tz. Jifunze kujenga hoja bila kuweka mambo ya ukanda.
 
KITU cha white Rose ni shida kuja mpaka huku Juu ilkiurei ni TABU bin problem...nilivyoona Title nikasema usipo mention barabara ya kupanda ilkiurei lazima nitaiongelea.

Hii road imekua MTO na mbaya zaidi serikali inajua vyema kabisa..ukipandisha na hii barabara hadi huku juu Ngateu utaelewa kua huu ni Mto na si Barabara..

So sad tumezitumia hizi barabara zikiwa mbaya tangu utotoni na hadi leo tuna mifamilia barabara hizi ziko vile vile..Huruma kwakweli na saingine ni kuoneana Tu sjui sababu nini?😡
 
Hii inaitwa majungu on making........

Kwa taarifa yako mikoa yote inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na maendeleo hayawezi kugawanywa kwa kuzingatia waliochangia pato hilo kwa wingi kwa mwaka fulani.

Na kwa kipindi hiki cha mvua ni maeneo mengi ya nchi yameathirika na mvua miundombinu imeharibika na hakuna ahaja ya kumlaumu mtendaji mmoja mmoja kwa jambo hili.

Tafakari kwanza kabla ya kundika usiwe na mihemko mkuu

Nikutakie asubuhi njema na sikunnjema katika kutekeleza majukumu yako
Hapo unaona umenijibu vizuri.. 🙊🙊
 
Kwa kweli hii hali ni mbaya kweli!, ukiambiwa hapa kuna mbunge unaweza usiamini, its so sad and pathetic. Hivi mbunge wa hapa ni nani tena vile?. Fedha za mfuko wa jimbo anafanyia nini?, maana zinatosha hata kumwaga tuu kifusi. Wana Arusha mlifanya makosa sana, sasa msirudie makosa ili Arusha irudie ile hadhi yake.

P
vifusi vimemwagwa sana mkuuu..hii barabara inahitaji Lami na si VIFUSI maana ni njia ya MAJI ukiweka vifusi maji yakichuruzika siku mbili tu Barabara inaharibika zaidi ya ilivyokua kabla ya kuwekwa vifusi...
 
Kwa kweli hii hali ni mbaya kweli!, ukiambiwa hapa kuna mbunge unaweza usiamini, its so sad and pathetic. Hivi mbunge wa hapa ni nani tena vile?. Fedha za mfuko wa jimbo anafanyia nini?, maana zinatosha hata kumwaga tuu kifusi. Wana Arusha mlifanya makosa sana, sasa msirudie makosa ili Arusha irudie ile hadhi yake.

P
Daaah Brother hata wewe tena?
I thought I could see a comment like this from praise team and 7000/= aspirants.. but not from you. To me ua among the members who gives us thoughtful and constructive ideas.. but this one mmmmmmmmm
 
Naamini tunapaswa kujenga nchi kwa ajili yetu na si kwa ajili ya wageni.sote tunastahili kilicho bora,acha mawazo ya kitumwa.
Tatizo uelewa wako Upo chini, ninacho maanisha hapo ukiitengeneza mkoa wa Arusha vizuri, watalii wataongezeka kwa kupata huduma nzuri, then pato la Taifa litaongezeka ndio na ww utaweza kutengeneza nchi kwa ajili yako.. Kwa kifupi katika nchi yeyote kuna mikoa imekaa kibiashara kitaifa.
 
Back
Top Bottom