Mkishangaa ya Chato msisahau ya Msoga

Mkishangaa ya Chato msisahau ya Msoga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,879
Reaction score
828,412
Natambua wingi wa matukio na harakati za maisha vinatufanya kuangalia mapya bila kutafakari yaliyopita.

Wiki hii kulikuwa na mjadala mwingine baada ya kuzinduliwa Mahakama ya wilaya CHATO ikitajwa kama mahaka kubwa na nzuri kulinganisha na Mahakama nyingine za mwanzo TANZANIA

Tangu awamu hii ishike hatamu mambo mengi ya kimaendelea yamefanyika CHATO... Kwa kutaja chache tu

Traffic lights
Jengo kubwa la Bank ya CRDB
Jengo la mamlaka ya mapato TRA
Mbuga ya wanyama
Uwanja wa ndege
Uwanja wa mpira
Msikiti mkubwa nknk
Malalamiko yamekuwa mengi kuwa kuna upendeleo unafanywa kuipa CHATO maendeleo isiyostahili
Ni lazima tukumbuke kanuni hii muhimu ya BINADAMU kwamba MWAMBA NGOMA NGOZI HUVUTIA KWAKE... Ni baba wa Taifa pekee hayati Mwalimu J. K. Nyerere ambaye alienda tofauti na kauli hii na kidogo akafuatiwa na Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa

Alipoingia madarakani brother Jakaya mambo yakawa tofauti... Akaamua kutumia nafasi yake kuwasaidia watu wa kwake.. Aamejitahidi kadiri alivyoweza kuiamsha Pwani.. Miradi mingi ikipelekwa huko ama Pwani ikipewa kipaumbele... Ombwe halikuonekana sana kwakuwa pia Pwani ni eneo MKAKATI kwa ajili ya kuingia na kutoka Dar.

Hata hivi viwanda vya leo Pwani zilikuwa ni juhudi zake.. Lakini kuna mengine yakawa ni kama hayakuwa na ullazima wa kuyafanya... Leo hii kuna njia mbili za lami mpaka mlangoni kwake pale Msoga... Lakini kuna Msikiti mkubwa mzuri ulijenga pale Msoga barabarani siku hizi umezungukwa na nyasi. Hauhudumiwi tena

Natambua dhima ya kila kiongozi kutaka kusaidia eneo lake ili walau lifanane na kwingine... Natambua fika mawazoni mwao wanataka kuona maeneo yao yakifanana na kaskazini hasa ukanda wote wa Tanga, Moshi mpaka Arusha... Lakini huu ni mchakato mrefu wenye kuhitaji maandalizi na mpango MKAKATI a kina... Kielimu na kubadili mtazamo wa wenyeji wake

Watu wa kaskazini wako vizuri juu na chini pia na wnapenda sana kutumia vizuri fursa zilizopo, ni wabunifu na ni wachapakazi.. Hawana majungu na wanathamini kila kitu kizuri.. Wanapenda UMOJA na kushirikishana... Wanajua vizuri thamani ya elimu ardhi na rasilimali watu....

Maendeleo yaliyojaribu kupelekwa CHATO na PWANI yangepelekwa kaskazini... kisinheharibika hata kitu kimoja na kingetumiwa kwa weledi mkubwa na kuleta matokeo chanya zaidi... Lakini la zaidi huko kote wanaosimania na kujaribu kuleta matokeo hayo chanya bado ni wale wale wa kaskazini!

Kwa mfano Pwani ya JK wenyeji wamebaki kuwa viibarua wapagazi na kazi zisizo na taaluma huku wakiendelea kuuza ardhi zao kwa bei sawa na bure.. Wao wakipata pesa kidogo ni starehe na KUONGEZA wake.

Siwezi kuizungumzia CHATO kwasasa lakini haina tofauti sana na Pwani... Na kuna uwezekano mkubwa sana awamu hii ikiheshimu Katiba na kuondoka madarakani kila kitu kitakufa kule.... Labda wa kaskazini wafanye jitihada kuokoa jahazi kwakuwa maono yao ni makubwa na uelewa wao uko deep zaidi...

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtoto aliyekulia nyumba ya nyasi na aliyekulia nyumba ya bati na sakafu...

Nimemaliza...!!!!

Jr
 
Dah, haya mkuu yetu macho uliyosema yana ukweli wake. Jengo la mahakama wilaya ya Chato ni hatari kuliko mikoa mingi niyotembelea na hakika muendelezo wa hayo yote itakuwa ni changamoto kwani rasilimali watu haijaendelezwa kabisa
 
Msukuma ana hela sana, lakini ni mtu wa kuridhika mapema!. Booster la Chato litafanya kazi hata Meko akiondoka lakini litaishia kuiinua Chato pekee!.
Ukiiangalia Mwanza imeendelea lakini hao hao wasukuma ndio wapo Shinyanga, angalia Kahama inaendelea lakini kwanini sio Shinyanga nzima?).
Tunapiga kazi lakini tunaridhika mapema!.
tunaamini ushindani ni kuvunja undugu
 
Ukizungumzia maendeleo ya kanda ya Kaskazini usisahau kuna kanda ya ziwa pia.

Siku zote ni huwa Mwanza vs Arusha na Moshi vs Kagera na si Chato vs Kaskazini.

Lakini kwanini haya yote ni chato kama si ubinafsi wakati Kagera hawana hata stendi ya mabasi ya kueleweka.
 
Mind setting... Una mifugo mingi lakini kila ukiuza pesa unafutika mchagoni
Una mifugo mingi lakini haina afya nzuri
Una mifugo mingi lakini familia inaishi mazingira magumu kuanzia lishe mpaka elimu na mahitaji mengine muhimu... Hili tatizo lipo hata umasaini... Mifugo inapewa thamani kubwa kuliko BINADAMU lakini wamasai sasa wameanza kubadilika
Una maanisha watu wa chato wauze n'gombe wakarundike mihela Bank au

Jr
 
Back
Top Bottom