"Mkiniacha mnaniogopa, mkinigusa mmenionea"

Oct 7, 2019
51
156
Well, kwa mara nyingine nimemsoma Mwanasiasa nguli wa Haki za CHADEMA ktk kivuli cha "Monrovian Uamsho" aliyekabidhi kikoba cha "injili" na "Theolojia" kwa Mbowe na kukumbatia "Unyumbu"....Huyu ni Kamanda Mwamakula, yeye anajaribu kulalamikia kufutiwa leseni kwa Gazeti la Tanzania Daima huku jicho lake Mwanasiasa huyu wa kwenye Madhababu likitua rasmi kwenye "Hukumu pekee" na sio "Maonyo" na "kukiri na kurudia Makosa mara kadhaa kwa chombo husika"

Hapa chini kutoka Maktaba,Pichani ni Barua mbili toka kwa Uongozi wa Gazeti la Tanzania Daima lenyewe kwa nyakati tofauti likiomba Radhi kwa kuchapisha Taarifa za Uongo ambazo zingine zililenga kuleta Taharuki ktk jamii....na ikumbukwe kupitia Barua hizi walisamehewa...walisamehewa na chombo kile kile kinachoitwa "Katili" mara baada ya leo hii kuamua kusimamia Sheria na kuchukua Hatua.

#Moja ya Nukuu ktk Barua hizo: "Tunaahidi kuzidisha umakini na kuepuka kurudia Makosa katika Taarifa zetu"
#Note: Ukisoma Barua ya Kufutiwa Leseni Gazeti la Tanzania daima imeelezwa wazi kuwa Gazeti hili limesamehewa na kuonywa kwa zaidi ya Mara 10 achilia mbali kuomba radhi kwa mara mbili pekee.

Barua hizi za kukiri Makosa na kuomba Msamaha ni ushahidi tosha, ni Mwanasiasa yupi wa juu ya Madhabahu, mweye kiremba cha urefu wa size ipi aliyewahi kuwaonya au kuwapa muongozo Free Media kwa namna ilivyo dhambi au kinyume cha sheria kupotosha na kuandika Uongo?..Ndio Kamanda Mwamakula?

Sasa kama Uongozi wa gazeti umewahi kukiri hadharani kuchapa taarifa za uongo kinyume na miiko ya uandishi na kinyume cha miongozo na sheria inayosimamia leseni yao, je wakirudia makosa mara kwa mara waachwe kwa kuwa tu Gazeti hilo linamilikiwa na kiongozi wa chama cha Chadema na itaonekana imeonewa?

kwamba Chombo hiki kesho kikiandika Taarifa kwamba Askofu Mwamakula anatumika na Taasisi fulani ya Marekani kujaribu kueneza Ushoga kanisani badala ya injili halafu Mwamakula mwenyewe akaenda kukishtaki Mahakamani chombo hicho cha habari kwa kuandika uongo na kikashindwa kuthibitisha Uhalali na ukweli wa Taarifa hiyo.Hapa serikali ikichukua hatua dhidi ya chombo husika inakuwa imeonea na kuminya uhuru wa Habari?

Mwamakula anasahau kuwa Wafuasi wenzake wa CHADEMA wamewahi kuchoma Nakala za Gazeti la kamanda mwenzao kubenea "Mwanahalisi" Wakidai kuwa linaandika taarifa za uongo mara baada ya moja ya Chapisho kusomeka "Ben saa nane aonekana kwenye vijiwe vya Kahawa"..imeisha hiyo, Panic at Ur own Risk.
 
Kwa nini usingetumia tu njia ya heshima na ya kistaarabu kuzijibu hizo hoja za huyo Baba Askofu? Kuna sababu gani ya kutumia lugha ya kejeli!! Mbona lugha hiyo hiyo ikitumika kumkejeli malaika wenu mkuu mnatokwa na mapovu? Una ushahidi wowote wa hayo uliyo yaandika!

Yaani mtu akiwakosoa tu basi anaunga mkono ushoga au ametumwa na kutumiwa na Mabeberu!! Awamu ya tano mnaumwa ugonjwa wa aina gani nyinyi? Kwa nini mnataka msifiwe na kupongezwa tu, na siyo kukosolewa?

Mtakwenda motoni kwa kutowaheshimu Watumishi wa Mungu! Kisa tu mmelewa madaraka. Yatokeapo tu majanga mnakuwa mstari wa mbele kuwaomba ili waliombee Taifa! Wakiwakosoa kutokana na udikteta wenu uchwara, mnapaniki!

Hovyo kabisa.
 
Kwa nini usingetumia tu njia ya heshima na ya kistaarabu kuzijibu hizo hoja za huyo Baba Askofu? Kuna sababu gani ya kutumia lugha ya kejeli!! Mbona lugha hiyo hiyo ikitumika kumkejeli malaika wenu mkuu mnatokwa na mapovu? Una ushahidi wowote wa hayo uliyo yaandika!...
maandiko matakatifu yanasema, mjinga hujibiwa kwa kadri ya ujinga wake.
 
Kwa nini usingetumia tu njia ya heshima na ya kistaarabu kuzijibu hizo hoja za huyo Baba Askofu? Kuna sababu gani ya kutumia lugha ya kejeli!! Mbona lugha hiyo hiyo ikitumika kumkejeli malaika wenu mkuu mnatokwa na mapovu? Una ushahidi wowote wa hayo uliyo yaandika!

Yaani mtu akiwakosoa tu basi anaunga mkono ushoga au ametumwa na kutumiwa na Mabeberu!! Awamu ya tano mnaumwa ugonjwa wa aina gani nyinyi? Kwa nini mnataka msifiwe na kupongezwa tu, na siyo kukosolewa?...

Hawa maaskofu wa aina hii hawahitaji heshima, na wakilelewa saana mwisho hugeuka yule askofu kibweterere aliewachoma waumini wake kanisani uganda,

Huwezi kuwa na heshima kama hupati muda wa kutafakari jambo kabla ya kutoa kauli. Na kwa taarifa yako maaskofu wote sio wapakwa mafuta wa mungu, wengi walizoea pesa za rushwa kutoka kwa waumini wao, jambo hilo linawatesa sana wakati huu.
 
maandiko matakatifu yanasema, mjinga hujibiwa kwa kadri ya ujinga wake.

Tatizo mnadhani kila Mtumishi wa Mungu ni mnafiki kama Gwajima na wenzake wengi tu! Kuna wengine wana msimamo kama wa Yohana Mbatizaji aliyekubali kukatwa kichwa na Herode kwa sababu tu ya kusema ukweli!
 
Hawa maaskofu wa aina hii hawahitaji heshima, na wakilelewa saana mwisho hugeuka yule askofu akiuewachoma waumini wake uganda,
Huwezi kuwa na heshima kama hupati muda wa kutafakari jambo kanlabya kutoa kauli.
Na kwa taarifa yako maaskofu wote sio wapakwa mafuta wa mungu, wengi walizoea pesa za rushwa kutoka kwa waumini wao, jambo hilo linawatesa sana wakati huu.

Nawaunga mkono Watumishi wa Mungu wote wa aina ya Bagonza, Mwamakula na wengineo wengi ambao siyo wanafiki! Hakika ukweli utawaweka huru. Kama Nchi inaendeshwa kidikteta, ni haki yao kuwakemea watawala wa aina hiyo walio kengeuka.
 
The only truth ni kwamba Tanzania Daima hawajui kuwasifia, wakiandika ukweli kwenu unageuka tusi hivyo mnawataka wawaombe radhi.

Ndio maana mara nyingine walikuwa hawaombi radhi kwasababu hawakuona makosa yao.
 
Tatizo mnadhani kila Mtumishi wa Mungu ni mnafiki kama Gwajima na wenzake wengi tu! Kuna wengine wana msimamo kama wa Yohana Mbatizaji aliyekubali kukatwa kichwa na Herode kwa sababu tu ya kusema ukweli!
unahitaji maombi
 
Tatizo mnadhani kila Mtumishi wa Mungu ni mnafiki kama Gwajima na wenzake wengi tu! Kuna wengine wana msimamo kama wa Yohana Mbatizaji aliyekubali kukatwa kichwa na Herode kwa sababu tu ya kusema ukweli!

Wameshindwa kuwazuia waumini wao wasifanye makosa na ufisadi, wanachopenda waumini waibe kisha watoe pesa nyingi kwenye makanisa yao kisha wao huwabaliki kwa jina la mungu huku wakijua hizo pesa ni za ufisadi,
Ulishawahi kumuona askofu anakataa pesa ya mtu anatuhumiwa kufanya ugisadi?
 
Back
Top Bottom