Mkinga: Mkapa alimtisha Magufuli IKULU

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,344
2,535
Naangalia kipindi cha mada moto channel ten hapa, wageni ni Renatus Mkinga na Rais wa chama cha Mawakala wa Forodha nchini Steven Ngatunga.

Mkinga ametonya kwamba, siku ambayo Mkapa alikwenda Ikulu kumtembelea Magufuli amepata taarifa kwamba Mkapa alimtisha Magufuli kwamba asiirudishe NASACO kuchukua nafasi ya Mawakala wa forodha eti Makampuni ya meli yataacha kufanya biashara na Tanzania.

Hili ni DOA kubwa sana kama ni kweli.
 
Magu ni mtiifu kupita kiasi kwa Mkapa!! Ameliona hilo tu? Mbona mengine hasemi? Sie tunacheki movie tu wacha mashabiki waendelee kutunga pambio za sifa!!
 
Kila mtu nchi hii ni jipu sema wanaonewa wachache
Dawa ya ufisadi bandarini:
(1) Kuanzisha REGULATORY AUTHORY ya bandari zote nchini. Bahati mbaya chombo hiki kinaogopwa sana na mafisadi, ndo maana wanapinga kisiwepo. Bila kuwa na agency ya dola ya kuregulate bandani nchini, juhudi zote zinazofanywa na akina Magufuli na Majaliwa zitakuwa mere cosmetic, short term solutions. Lazima kutengeneza controlling mechanism(mfumo) ya kudumu na ambayo ipo kisheria. Private Agents wanafanya biashara tu, hawawezi kulinda masilahi ya nchi zaidi ya kutafuta faida yao.
(2)Mapato/tozo yote ya serikali yakusanywe na taasisi moja ya serikali. TRA ndo wahusike kukusanya malipo/kodi/tozo yote ya serikali. Malipo yote yawe kwenye risiti moja(integrated receipt) ya TRA.
Note:TPA wasihusike kupokea malipo ya aina yoyote ile.
 
Naangalia kipindi cha mada moto channel ten hapa, wageni ni Renatus Mkinga na Rais wa chama cha Mawakala wa Forodha nchini Steven Ngatunga.

Mkinga ametonya kwamba, siku ambayo Mkapa alikwenda Ikulu kumtembelea Magufuli amepata taarifa kwamba Mkapa alimtisha Magufuli kwamba asiirudishe NASACO kuchukua nafasi ya Mawakala wa forodha eti Makampuni ya meli yataacha kufanya biashara na Tanzania.

Hili ni DOA kubwa sana kama ni kweli.
Mambo mengine ni vigumu sana kuyaamini hasa pale mtu anapotoa taarifa ya jambo ambalo hakuwa sehemu ya jambo hilo wakati linatendeka. Ndiyo maana mahakamani ushahidi wa "niliambiwa" huwa haukubaliki.
 
Naangalia kipindi cha mada moto channel ten hapa, wageni ni Renatus Mkinga na Rais wa chama cha Mawakala wa Forodha nchini Steven Ngatunga.

Mkinga ametonya kwamba, siku ambayo Mkapa alikwenda Ikulu kumtembelea Magufuli amepata taarifa kwamba Mkapa alimtisha Magufuli kwamba asiirudishe NASACO kuchukua nafasi ya Mawakala wa forodha eti Makampuni ya meli yataacha kufanya biashara na Tanzania.

Hili ni DOA kubwa sana kama ni kweli.

Wengine mnafikiria Tanzania kuna marais wanne!
 
Nina wiki nzima nimefunga huku nikiomba mhe Rais asije akasahau akiishamaliza kuyatumbua majipu ayakabidhi kwa wataalam wa kuminya wayaminye na wayakamue kisawasawa pabaki mashimo kama ya machimboni.
 
Hii vita kati ya serikali na wafanyabiashara bado naiangaliaa, sijui mshindi atakuwa nani, na Serikali ikishinda basi itaandikwa historia katika dunia hii ya kibepari
 
Back
Top Bottom