Mkija kwenye miji yetu msitutafute lawama tafadhali

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Kasumba ya kwamba wewe ukija niliko basi muda wote nitakuwa na wewe ondoa kabisa akilini. Huo ni upuuzi. Mtu analalamika kuwa kaja town kakaa 2 weeks eti tumeonana mara 3 tu.

Sasa uliambiwa kuwa mimi ni tour guide? Mtu akitoka bush akaja town anataka akatembelee maeneo yote aliyowahi yasikia na kuyaona insta. Kumbuka yeye kaja kwa ratiba zake. Kama kaja mapumziko maana yake ana muda.

Sasa anataka nami nivunje ratiba zote nimwangalie yeye. Weekend tukeshe sehemu za starehe. Ni ubwege huo. Mimi nikienda Mkoani au nchi ya mtu namwambia tu kuwa nipo nampa hi. Then hanisikii tena. Akijisikia kunitafuta atanitafuta asipojisikia to hell nlienda na ratiba zangu. Mwezi uliopita nilikaa Sweden 3 weeks na yupo pale mwana. Nlimjulisha tu nipo Jijini. Akasema atanitafuta. Hakunitafuta.

Nliporudi Dar ananilaumu kwa nini sikumwambia aje nilipo tuonane. Nikamwambia tu nlimjulisha nipo jijini kwake so alitakiwa aangalie ratiba zake kama ana nafasi au hana but siyo mimi kumghasi.

Na ninyi mkija kwetu acheni ujinga wa kusema nitafutie demu mkali, mipeleke sijui wapi. Kila mtu ana ratiba zake. Nawapa huu ujumbe na wengine pia. Hatutaki urafiki lawama.
 
Back
Top Bottom