Mkidengua tunaenda Kenya,Wakenya wakidengua tunarudi Tanzania,tunachezeshwa shele,Ushauri wangu ni huu.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Haya Mabeberu yameamua kutuchezesha shele Watanzania,lakini ukweli ni kwamba mkataba wa bandari hauna tija kwa Tanzania na hauna tija kwa Wakenya,wanatuchezesha shele ili kile wanachokitaka toka kwetu wakipate kwa bei ya chini zaidi kama sio bure,wao wanatuchezesha kujihakikishia ushindi kwa vyo vyote vile itakavyokuwa.

Ushauri wangu ni huu;-

1.Ibara ya 27 katika mkataba huo inatufunga nchi ya Tanzania,Ili isitufunge nashauri kiwepo kipengele ambacho Tanzania inawazuia DPW wasiwekeze kwenye nchi Jirani au yoyote shindani na Tanzania maana kama ni Tanzania kunufaika basi Watanzania tulipaswa tuwe na kipengere hicho kwenye mkataba huo,endapo tutakimbilia kuwapa bandari na bado Wakenya nao wakawaita Dpw kwao na kuwekeza,tutakuwa tumetwanga maji kwenye kinu,kwa maana hatutaweza kuzuia lengo na kumkomoa Kenya na nchi nyingine zenye bandari kwa faida ya Tanzania,rejea kilichotokea Djibouti, mkataba ulikuwa hauifungi DP World isiwekeze Congo na Rwanda,waliizunguka Djibouti mizigo ya Ethiopia na Somalia ikawa kesi,

2.Suala la muda katika mkataba liwekwe wazi,ibara ya 23(1) ya mkataba huo irekebishwe ni hatari kusema ukomo wa muda wa DPw kufanya kazi Tanzania mpaka pale shughuli za mradi zitakapokwisha.

3.Kampuni ya kigeni isimilikishwe ardhi kama kuna mwenyeji ana hisa 35% basi ardhi iwe ya huyo Mwenyeji mwenye hizo hisa 35% na atakapovunja masharti ya mkataba tunachukua ardhi yetu.

3.Mkataba uwe na kipengere cha kuvunjwa pindi vipengele vya mkataba vikivunjwa,ibara ya 23(4) ya mkataba huo wa bandari ibadilishwe ilikuwa inakataa mkataba kuvunjwa.

4.Mkataba usiwe juu ya Katiba na sheria za nchi ya Tanzania.

5.Kwenye mkataba huo Serikali iwe na uwezo wa kukagua muda wowote juu ya kile kinachofanyika bandarini.

6.Katika mkataba huo iwekwe wazi DP World wapewe baadhi ya bandari na ifanye ubia na Serikali sio kupewa bandari zote kama mali yao.

7.Katika mkataba huo Serikali iruhusiwe kutazama fursa nyingine sio kuuliza Dubai,Serikali ya Tanzania inatakiwa iwe na nguvu,na Dubai ndio waulize Tanzania pindi wakiona fursa yoyote,ibara ya 27 katika mkataba huu wa bandari ibadilishwe.

8.Katika mkataba kuwe na tangible results (matokeo au manufaa halisi) toka kwa DP World,matokeo,mafanikio au manufaa halisi itakayopata Tanzania yasisemwe kwa nadharia tu hewani hewani yawepo ndani ya mkataba na Watanzania wayapime kama ni mafanikio kweli au mtoto kimdanganya na peremende,manufaa yasemwe ni yapi na kwa kiasi gani kwa Watanzania.

9.Uwekezaji unaokwenda kufanywa uwekwe wazi,sio kueleza kwa ujumla kuendeleza,kusimamia na kuendesha hali inayoweza kupelekea ubinafsishaji kinyume na sheria ya bandari na 17 ya mwaka 2004.

10.Utaratibu wa kupewa kazi DPW ulipaswa kufuata utaratibu wa kawaida kupitia TPA na kwa sheria za public private partnership (PPP) act na public procurement act no 7 ya mwaka 2011 na kwa ushahidi zionyeshwe kwa Watanzania sio kuelezea tu ooh zilichujwa kampuni 7 kuipata Dpw.

Mwisho suala la mkataba wa bandari ni jambo kubwa haliwezi kuingiwa kwa dharula na kusababisha kukosa uhalali wa kisheria,kwa mapungufu sehemu ya sahihi za wenye dhamana na pia kwa kukataliwa na wananchi mmoja mmoja.

Hizi ndizo shida na malalamiko ya Watanzania huku mtaani kwenye kahawa,kwa mangi, kwenye vijiwe vya ulanzi na komoni,kwenye korido za wasomi Chuo kikuu,na kwa wabobezi madaktari wa falsafa, Wanasheria na maprofesa,naamini mtazingatia waliojitokeza kuelezea matakwa yao kwenye mkataba huo wa bandari,ni jambo jipya kwa kariba ya manguli wa sheria na wabobezi mbalimbali kuungana kupinga mkataba huu wa bandari,tulizoea walalahoi kupiga kelele na tuliwadharau ila leo hii ni kariba nyingine ya walalamikaji,tuwasikilize na tufanyie kazi maoni yao.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Sawa Leslie Mbena.
Ngoja nikope Songesha nikutumie hata vocha ya buku tano! Namba yako nimeiona...
 
Ule mkataba ni wa kishenzi uvunjwe, bila kujali kama mwarabu atawekeza Kenya au hatawekeza.
 
Watu wa rangi nyeusi tunakuwaga na shida sana tunapotaka kuingia kwenye kila jambo. Iwe kwenye mahusiano, ndoa au ajira. Tunakuwaga na moto na shauku kiasi cha kutotaka hata kuelewa masharti, kufahamu undani wa hicho kitu wala kuangalia madhara.

Lakini huwa tunakuja kushtuka madhara yakianza kutokea. Tunaanza kutafutana uchawi.

Nchi hii mambo mengi yamefanyika kwa mihemko. Na huwa inakuwa mbaya zaidi pale kiongozi mkuu anapoonyesha interest zaidi na hilo jambo. Yaani hata washauri wake unakuta wanataka wafanye tu kile kinachomfurahisha bosi wao.

Ndio maana Magu alikuwa anapenda kujiridhisha vitu vingi mwenyewe sababu alijua hata hao washauri watafanya kile kinachomfurahisha yeye hata kama wameona kuna elements za kupigwa na yeye hakuona hilo.

Mwisho wa siku hao washauri wanaungana na wewe tena kushangaa. Pembeni wanasema tulijua tu.
 
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu rais kuongoza mihula miwili (2) mfululizo ya urais kwa maana ya miaka 10.. ila ikiwapendeza wabunge wetu wanaweza wakafanya namna kurekebisha hicho kifungu ili kukidhi mahitaji yetu kwa sasa.. Mama Samia aongoze hadi 2040.
 
Back
Top Bottom