Mkeo sio adui

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,415
7,968
Wanaume wengi sana, tuna dhana kwamba mke ni adui, na mara nyingi tunatumia vitabu vya dini eti vinasema tukae na wanawake kwa akili, kweli? Huyu Mungu ambaye ndiye aliowaumba anaweza kuwatengeneza wanawake wawe maadui kwa wanaume? No, sio kweli, hivyo vitabu vya dini hizo aya za hivyo zimeandikwa na wanaume kwa maslahi ya wanaume. Ewe mwanaume mwenzangu, mkeo ndiye rafiki yako mkubwa, ndiye mwandani wako, mpende, mpe raha, mpe kila aina ya usaidizi.
 
Kwani kuishi na kiumbe kwa akili kunamaanisha kwamba hicho kiumbe ni adui yako? Plus, kama angetaka pawepo uadui, asingeshauri TUISHI nao, bali TUWAKIMBIE kama tunavyoshauriwa kuikimbia dhambi. Alipokuwa anamlaani nyoka alisema nitaweka uadui, na sijawahi ona anywhere tunashauriwa kuishi na nyoka kwa akili. Kumbuka, maagizo ya namna ya kuiendesha bustani alipewa Adam (mwanaume). Shetani kwa werevu wake akaingilia kwa mwanamke, then mwanamke akamshawishi Adam nae alile tunda lililokatazwa(kwa tafsiri yoyote ya tunda unayoifahamu). Mwenyezi Mungu anajua jinsi mwanaume alivyo boflo mbele ya vishawishi vya mdada, ndo akashauri tuishi nao kwa akili.
 
Hizo ni alinacha tu,tena ni vitabu vimeandikwa na wanaume.Kwanini mwanaume ndio awe anaambiwa aishi na mwanamke kwa akili?
 
1704538833833.jpg

Wanawake waache dharau
 
Wanaume wengi sana,tuna dhana kwamba mke ni adui na mara nyingi tunatumua vitabu vya dini eti vinasema tukae na wanawwke kwa akili,kweli? Huyu Mungu ambae ndio aliowaumba anaweza kuwatengeneza wanawake wawe maadui kwa wanaume? No sio kweli,hivyo vitabu vya dini hizo aya za hivyo zimeandikwa na wanaume kwa maslahi ya wanaume.Ewe mwanaume mwenzangu,mkeo ndio rafiki yako mkubwa,ndio mwandani wako,mpende,mpe raha,mpe kila aina ya usaidizi
Limbwata at work
 
Umesema ukweli ,moja ya ujinga tunamezeshwa ni hili la kuwachukia wanawake eti tuishi nao kwa akili mara sio ndugu zetu....Unaweza kufirikia kama mambo yote hayo ni kweli kuna haja gani ya kuoa au kuishi mke na mume.

Baadhi ya ndugu pia ni wajinga wanajifanya wao wana mamlaka kwa kaka yao kuliko mkewe wa ndoa ,yote hayo ni ujinga kuamini mwanaume adui wake ni mkewe ...Kama ndugu wa maana sana basi kila mtu aoe dada ake waliozaliwa tumbo moja.

Mtu anaongea ujinga wakati yeye kafika hpo kwa malezi ya mama na baba..

USHAURI; WAKE ZENU NDIO WATU WENU WA KARIBu ,CHOOSE WISELY ...Ndi ikiwa safi utaishi vizuri.
 
Mke siyo adui?? Kwahiyo unataka kusema mke ni ndugu yako?

Mbona anakuita honey lkn kiksanuka anakuita mbwa?

Mbona anakupeti peti leo ukiwa na afya nzuri, kipato kizuri na cheo kizuri lkn ukiugua, ukafilisika ama kushushwa cheo anakukimbia? Mke siyo ndugu yako.
 
Betri low
 
Wanaume wengi sana,tuna dhana kwamba mke ni adui na mara nyingi tunatumua vitabu vya dini eti vinasema tukae na wanawwke kwa akili,kweli? Huyu Mungu ambae ndio aliowaumba anaweza kuwatengeneza wanawake wawe maadui kwa wanaume? No sio kweli,hivyo vitabu vya dini hizo aya za hivyo zimeandikwa na wanaume kwa maslahi ya wanaume.Ewe mwanaume mwenzangu,mkeo ndio rafiki yako mkubwa,ndio mwandani wako,mpende,mpe raha,mpe kila aina ya usaidizi
Wew bado mtoto mdogo, hujayajua mengi.
 
Back
Top Bottom