Mkeo ndio rafiki wako wa kweli

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,585
44,831
Juzi nimemsikia mchungaji mmoja akisema kwa wale mnaoishi maisha ya unyumba ukitaka kujua mkeo ndio rafiki wako mkubwa basi ugua ugonjwa wa kulazwa wa kukaribia kufa au ugonjwa uzidiwe mpaka ujinyee mkeo atakusafisha matako bila kuona kinyaa maadam mlipendana kwa dhati.

Ndugu na marafiki watakuja week ya Kwanza na matunda ya kuzuga baada ya hapo hutawaona Tena. Mkeo atakaa mpaka dakika ya mwisho na yeye akianza kuchoka jua ameshaona hutoboi so ni Bora ukamwachia roho yako bwana kiroho Safi na ndo maana hata mirathi next of keen awe mkeo hawezi kuacha watoto wenu ila ndugu wengine hawana uchungu wanakula Mali yote..
 
Hawa
Wanawake wa kizazi Cha Beijing,

Akiona unaumwa unakaribia kufa,

anakutengenezea usia feki

Na kukuletea kukusainisha ukiwa hoi kitandani.

Kisha anakudunga sindano ya sumu ufe kabisa abaki na mali na hataki ndugu au Yoyote yule ahoji usia feki wa marehemu

YAPO SANA KWNY JAMII YETU NA YAMETOKEA KWA MACHACHE TUMESHUHUDIA
 
Juzi nimemsikia mchungaji mmoja akisema kwa wale mnaoishi maisha ya unyumba ukitaka kujua mkeo ndio rafiki wako mkubwa basi ugua ugonjwa wa kulazwa wa kukaribia kufa au ugonjwa uzidiwe mpaka ujinyee mkeo atakusafisha matako bila kuona kinyaa maadam mlipendana kwa dhati.

Ndugu na marafiki watakuja week ya Kwanza na matunda ya kuzuga baada ya hapo hutawaona Tena. Mkeo atakaa mpaka dakika ya mwisho na yeye akianza kuchoka jua ameshaona hutoboi so ni Bora ukamwachia roho yako bwana kiroho Safi na ndo maana hata mirathi next of keen awe mkeo hawezi kuacha watoto wenu ila ndugu wengine hawana uchungu wanakula Mali yote..
Halina kanuni maalumu. Binadamu hatabiriki
 
Mama mzazi kama bado yupo hai huyo ndio rafiki wa kweli. Hataangalia hali yako ya kifedha au cheo wala unaumwa kwa kiasi gani, atakuosha pasipo kukumbuka wala kutegemea malipo. Baba anaweza kuona uvivu lakini sio mama. Mke aisee, aah hamna kitu.
 
Back
Top Bottom