Mkenya Asiyetosheka na Wanawake Afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkenya Asiyetosheka na Wanawake Afariki

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ancentus Akuku maarufu kwa jina la "Danger" akiwa na baadhi ya wake zake enzi za uhai wake
  Mwanaume wa nchini Kenya ambaye alioa wanawake 130 na kuzaa watoto 210, amefariki dunia nchini Kenya. Mwanaume wa nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Ancentus Akuku maarufu kwa jina la "Danger" ambaye huenda akawa mwanaume aliyeoa wanawake wengi kuliko wanaume wote duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

  Katika maisha yake, Akuku alioa jumla ya wanawake 130 kati ya wake zake hao 30 aliwapa talaka.

  Kama jina lake linavyobashiri "Danger", (hatari), Akuku alikuwa na watoto 210, wakiume 106 na wakike 104. Kati yao watoto wake wa kike 35 na wa kiume 20 wamefariki dunia.

  Kwa mujibu wa mtoto wake mkubwa, Akuku alizimia akiwa kwenye mazingira ya nyumba yake mjini Kisumu, alipowahishwa hospitali alifariki dunia.

  Akuku alimuoa mke wake wa kwanza Dinah Akuku, mwaka 1939, wakati mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 79, Akuku alifunga ndoa na msichana kigori mwenye umri wa miaka 18. Huyo ndiyo alikuwa mwanamke wa mwisho kufunga ndoa na Akuku.

  Mazishi ya Akuku aliyefariki jumamosi yamekumbwa na mzozo kutokana na idadi kubwa ya watoto. Hadi sasa muafaka haujafikiwa kuhusiana na tarehe ya kuzikwa kwake.

  Ukoo wa Akuku una shule mbili zilizojengwa na Akuku ili kuwapa elimu watoto na wajukuu zake na pia wanamiliki kanisa lao moja kwaajili ya ibada.

  Dr Tom Akuku ambaye ni mtoto mkubwa kuliko wote wa kiume wa Akuku, alisema kuwa ingawa hati walizo nazo zinaonyesha Akuku ana watoto 210, huenda baba yao akawa na watoto zaidi ya 210.

  "Mzee alikuwa na watoto wa kike 104 na wa kiume 106 hivyo kufanya jumla ya watoto 210, lakini naamini kutakuwa na watoto wengi hawamo kwenye listi".

  "Idadi ya wajukuu ni zaidi ya 1,800", alimalizia kusema Dr. Akuku.

  Ukoo wa Akuku unategemea kukutana tena alhamisi kujadili tarehe ya mazishi.
  Chanzo : NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Na Picha zake limepiga kijanja Jana na pensi....wajuu na watoto wanaweza kumzika bila mtu mwingine kuhudhulia...na kila mtu akiwa analia kwa uchungu.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Du huyo kweli alikuwa na nguvu za ajabu! Lakini watoto wote hao ana uhakika ni wake?
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,761
  Trophy Points: 280
  We uSIetosheka na alietosheka wote mko njia moja kazi ipo!!
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Kitanda hakizai haramu, hiyo kweli damu yangu..."
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mh! Haya...
   
 7. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duh!mwisho wajukuu wataoana bila kujuana
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,254
  Trophy Points: 280
  HUYU BABU HAKIKA NI JINI MAHABA.
  NDO MAANA KIFO CHAKE KIMEAMBATANA NA UVUMI WA KIFO CHA SHEIKH YAHYA MTAALAM WA KITIMOTO:decision:
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Huyu katimiza agizo la Muumba,nendeni duniani mkaijaze nchi.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Lakini sio kwa namna hii ya huyu mzee, wake 130 hii ni balaa!
   
 11. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  130 wote aliwaoa, na dini gani au kimila?
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Nani alimdanganya kule kuna migodi ya dhahabu mpaka awe ana wake wengi kiasi hicho!
   
Loading...