Mkemia mkuu tunaomba utuhurumie, unatuumiza sana

Nyie wengine munafurahia taarifa ya mkemia mkuu? Mungu anawaona sawa bhana.

Lakini kwani lengo la taarifa yake hiyo ni nini hasa? Familia ziachane nyingi au ?
 
Ila huwa haendelei kuweka wazi kua wote walioenda kupima tayari walikua na wasiwasi au Mashaka juu ya uhusika wa uhalali wa kua biological father inaelekea lengo lake ni negative
 
So unataka aongope tuendelee kule matoto ya wenzetu?

Sema tu ukweli baba kama mbai iwe mbwai barida
 
Kwani amewataja kwa majina wote? na ukenda kupima DNA watoto kwani hupewi majibu? Unataka nini hasa?
 
Kwanza kabisa mpaka mkapime DNA inamaana kuna matatizo makubwa juu yenu,kwahiyo majib yakitoka kwamba mtoto sio wa baba ni kawaida ,mkemia yupo sahihi kutoa takwim hizo tatizo ni jamii,pia takwimu za HIV kwenye kijiji
 
mchapiwe wake zenu mpaka wanazalishwa halafu lawama mnapeleka kwa Mkemia Mkuu
 
Sasa mnataka mpewe nini!! Hiyo ndio hali halisi. Jiulize anafahidika na kipi akidanganya!?
 
Mpaka watu wapeleke issue yao kwa huyo mkemikali mkuu tayari kuna wasi wasi fulani. Therefore kwa ujumla asilimia kubwa ya matokeo lazima yatakuwa hivyo. It is expected. Mfano inategemewa kwa asilimia kubwa ya watu wote wanaohudhuria hospital watakuwa wagonjwa. So sishangai kabisa. Halafu ukweli ni ukweli kwa nini unataka mkemikali mkuu adanganye? Let the truth be spoken!
 
Unataka kumponza "mtaalamu" yamkute yaliyomkuta Mama Anna Kilango Malecela "MKOA WA SHINYANGA HAKUNA MTUMISHI HEWA"
 
Ifahamike tu kwamba wengi wetu humu hatujawahi kwenda kupima hizo DNA kwakuwa hatuna quarrel wala doubt kwenye upatikanaji wa mtoto aliyezaliwa.wengi wanaornda kule ni wale waliokuwa na wasiwasi jinsi mimba ilivyopatikana.na MTU sio mjinga atoe gharama zake kubwa akapime DNA wakati hakuna tatizo lolote.umesafiri umekaa miezi minne unarudi unamkuta mkeo ana mimba ya miezi miwili lazima uwe na wasiwasi na wasiwasi wako ni reasonable ndio maana wengi wao wanaokwenda kupima majibu yanakuja negative hivyo lazima majibu ya mkemia mkuu yawe hivyo kwakuwa wanaopelekana huko wengi wao tayari walishaona dalili
 
Fahamu kuwa, mpaka kupima DNA hadi kesi iende mahakamani. Mara nyingi baba huwa anasema mtoto sio wake hasa hasa kwa wanafunzi wanaopewa mimba.
 
Habari wadau.

Leo napenda kuweka wazi hili linalonikwaza kwa huyu mkemia mkuu wa serikali.

Ijulikane kwamba kila mwisho wa mwaka mkemia mkuu wa serikali amekuwa akitoa matokeo ya vipimo vya DNA alivyovifanya kwa mwaka mzima.

Lakini kila akitoa ripoti huonyesha kuwa wababa wengi walioenda kupima DNA inaonyesha watoto si wa kwao!

Yani bila kujali madhara yatakayotokea kwenye jamii ,yeye hutangaza tu kwamba matokeo yanaonyesha watoto si wa kwenu.

Jiulize wewe baba umelea mimba kwa kutoa matumizi, mtoto akazaliwa ukanunua nguo na mtoto akakua na ukampeleka shule.

Baadae kirahisi rahisi tu mkemia mkuu anakuja kutangaza mtoto si wako!!

Ungekuwa wewe ungejisikiaje??

Kwa taarifa yako hiyo ripoti inasababisha ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa watoto wa mitaani!!

Mkemia mkuu jiulize upya namna ya kuwasilisha ripoti yako kwa jamii.
Ndugu yangu kwa hiyo wewe unataka mkemia awe mnafiki?? Hao ndo wake zetu inabidi tukubaliane na matokeo kama ni matumizi ya mtoto piga moyo konde kwani pesa zinatafutwa hasara roho
 
Acheni uzinzi, kwa nini Unataka aseme uongo? Uongo ni dhambi
 
Back
Top Bottom