Mkemia mkuu tunaomba utuhurumie, unatuumiza sana

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Habari wadau.

Leo napenda kuweka wazi hili linalonikwaza kwa huyu mkemia mkuu wa serikali.

Ijulikane kwamba kila mwisho wa mwaka mkemia mkuu wa serikali amekuwa akitoa matokeo ya vipimo vya DNA alivyovifanya kwa mwaka mzima.

Lakini kila akitoa ripoti huonyesha kuwa wababa wengi walioenda kupima DNA inaonyesha watoto si wa kwao!

Yani bila kujali madhara yatakayotokea kwenye jamii ,yeye hutangaza tu kwamba matokeo yanaonyesha watoto si wa kwenu.

Jiulize wewe baba umelea mimba kwa kutoa matumizi, mtoto akazaliwa ukanunua nguo na mtoto akakua na ukampeleka shule.

Baadae kirahisi rahisi tu mkemia mkuu anakuja kutangaza mtoto si wako!!

Ungekuwa wewe ungejisikiaje??

Kwa taarifa yako hiyo ripoti inasababisha ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa watoto wa mitaani!!

Mkemia mkuu jiulize upya namna ya kuwasilisha ripoti yako kwa jamii.
 
Elitwege We ulitakaje labda??
Yaani aongee tu uongo ili kulinda Ndoa za wengine??
Kama mama kambambikia Mumewe watoto basi hata hiyo inayoitwa Ndoa ki msingi ni kama haipo, bora ivunjike tu
 
Elitwege Kwa kuwa ufahamu wenu ulishabemendwa na CCM na serikali yake kwa kufanywa misukule ya kulishwa uongo,unataka kila taasisi itoe taarifa ya uongo!

Ulitaka mkemia mkuu atoe taarifa na takwimu za uongo kama watoavyo TRA,TBA na wengine wengi ili iweje?Uongo hauwezi kulisaidia Taifa, mwache mkemia mkuu asimamie Ukweli wa taasisi yake ili jamii itambue kiasi cha usariti unaofanywa katika ndoa.
 
Jiulize wewe baba umelea mimba kwa kutoa matumizi, mtoto akazaliwa ukanunua nguo na mtoto akakua na ukampeleka shule.

Baadae kirahisi rahisi tu mkemia mkuu anakuja kutangaza mtoto si wako!!

Ungekuwa wewe ungejisikiaje??

Kwa taarifa yako hiyo ripoti inasababisha ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa watoto wa mitaani!!

Mkemia mkuu jiulize upya namna ya kuwasilisha ripoti yako kwa jamii.
Anatoa taarifa kirahisi? Ki vipi?
Ulitaka atoe taarifa akiwa katika mazingira magumu? Akiwa amekalia kisu? au akiwa anatafuna moto? au akiwa ananawa uso kwa maji yenye pili pili? Au akiwa na kitanzi shingoni?
 
Kuukimbia au kuukana ukweli hakujawahi kuwa suluhisho la ukweli wa jambo flani.

Watu wanachepuka utadhani hawana akili nzuri. Na bahati yetu wanaume hatubebi ujauzito, wanawake wangekuwa wanalea watoto wasio wao zaidi ya sisi leo tunavyolea watoto wasio wetu!
 
Elitwege Hio report ya mkemia mkuu si tu inasababisha ndoa kuvunjika na ongezeko la watoto wa mtaani Bali pia inapunguza nguvu za kiume maradufu kwa kuleta stress za kiwango cha makinikia
 
Habari wadau.

Leo napenda kuweka wazi hili linalonikwaza kwa huyu mkemia mkuu wa serikali.

Ijulikane kwamba kila mwisho wa mwaka mkemia mkuu wa serikali amekuwa akitoa matokeo ya vipimo vya DNA alivyovifanya kwa mwaka mzima.

Lakini kila akitoa ripoti huonyesha kuwa wababa wengi walioenda kupima DNA inaonyesha watoto si wa kwao!

Yani bila kujali madhara yatakayotokea kwenye jamii ,yeye hutangaza tu kwamba matokeo yanaonyesha watoto si wa kwenu.

Jiulize wewe baba umelea mimba kwa kutoa matumizi, mtoto akazaliwa ukanunua nguo na mtoto akakua na ukampeleka shule.

Baadae kirahisi rahisi tu mkemia mkuu anakuja kutangaza mtoto si wako!!

Ungekuwa wewe ungejisikiaje??

Kwa taarifa yako hiyo ripoti inasababisha ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa watoto wa mitaani!!

Mkemia mkuu jiulize upya namna ya kuwasilisha ripoti yako kwa jamii.
Elitwege, UNASEMAJEEEEEEEEEEEEEEEE?!
 
Hii mijamaa ya CCM bana inataka usemwe uongo hata kwenye mambo ya kisayansi nyie mmezoea kuiba kura sasa mnataka hata majibu ya mkemia muibe.
 
Haya ndio Trump alikua akisema!

Mtu kusema ukweli tunaanza kumzonga zonga! Hivi tuna akili mbovu kiasi gani?
 
Ni kweli kabisa.Taarifa ya mkemia mkuu inakosa ladha na ninaomba ichukuliwe kama ni kuongea bila staha.Madhara ni mengi kuliko faida ya kutoa ripoti kama ilivyo.Kama alivyosema ndugu yangu hapo juu kuwa mtoto umemfanyia kila jambo saa nyingine mpaka anahitimu chuo kikuu lakini leo unaambiwa mengine.

Jueni kuwa haya mambo yalikuwepo toka zama na mpaka majirani wanajua mtoto yule wa fulani lakini siri zilitunzwa.Leo hii tunashuhudia wasomi hawa wakitoa taarifa ambazo zinaikwaza jamii.Wote tumesikia majuzi mtu kawalima majembe mke, mtoto na shemeji kwa mambo hayahaya.TUBADILIKE.
 
Sioni kwa nini unaona yeye anachangia hayo kwenye ndoa.. labda mtu uwe una mashaka au tayari unahusika na hayo.

Na kama unamashaka si mkapime tu.. yeye ndio kazi yake.. ni nyie wanaume kuwapa raha wake zenu wasitoke nje.
 
Ni kweli kabisa.Taarifa ya mkemia mkuu inakosa ladha na ninaomba ichukuliwe kama ni kuongea bila staha.Madhara ni mengi kuliko faida ya kutoa ripoti kama ilivyo.Kama alivyosema ndugu yangu hapo juu kuwa mtoto umemfanyia kila jambo saa nyingine mpaka anahitimu chuo kikuu lakini leo unaambiwa mengine.Jueni kuwa haya mambo yalikuwepo toka zama na mpaka majirani wanajua mtoto yule wa fulani lakini siri zilitunzwa.Leo hii tunashuhudia wasomi hawa wakitoa taarifa ambazo zinaikwaza jamii.Wote tumesikia majuzi mtu kawalima majembe mke, mtoto na shemeji kwa mambo hayahaya.TUBADILIKE.
Kwaiyo adanganye
 
Ukienda kupima hiyo DNA mwambie unata majibu yaseme huyo ni mtoto wako utakuwa umemaliza tatizo.
 
Back
Top Bottom