Sioni sababu gani unapata ugumu kumshirikisha mwenzio maombi ya kugawia watu (hata kama ni ndugu zako) rasilimali za familia. Fedha hata kama ni zako, hizo ni za kwenu ndani ya familia hivyo mke ana uhalali wa kuhoji zinatumika vipi. Hapa naona shida unayo wewe na bado hujatambua kuwa unachokifanya ni tatizo. Bahati mbaya maelezo yako yanaonesha wote na mkeo mmekuwa ni watu wa kufichana mambo. Yeye ana siri zake nawe una zake. Kwa style hii ndoa haiwezi kuwa na afya. Inakuwepo tu ndoa jina.