Mke wangu wa ki-malawi (nimebaki njia panda)

Mke wangu wa ki-malawi (nimebaki njia panda)

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,778
Reaction score
1,223
Habari zenu wana MMU, Miaka takriban miwili na nusu iliyopita nilibahaatika kuwa na mahusiano na binti mmoja mwenyeji wa malawi ambaye baada ya kama miezi 6 ya uchumba tulifunga ndoa.
Kutokana na wazazi wa yule binti kuishi nje ya nchi (malawi) niliwaomba wazazi walezi tumalize kwanza michakato ya then ndo tupange utaratibu wa kwenda kuwaona wazazi husika kwa maana ya kujitambulisha nashukuru walikubali bila kinyongo.

Baada ya kuishi zaidi ya mwaka mmoja na nusu bila mke wangu kutokuwa na dalili zote za ujauzito ilibidi nishtuke na hatua ya kwanza niliyochukua ni kwenda kwa wataalam kwa ajili ya kunifanyia uchunguzi na matokeo yake waliambia sina tatizo lolote kwa upande wa mwenza wangu
niliporudi nyumbani nilimweleza oyte mke wangu na kumuuliza kulikoni miaka inaenda bila dalili zozote za ujauzito alichoniambia hata yeye yuko safi ila inawezekana ni wakati kwahiyo nivute subira kwani mambo mazuri hayataki harakakutokana na jibu hilo nikahisi kuna kitu si hivi hivi nikaomba ruhusa ya siku kumi na nne kazini kwa ajiri ya safari kwenda huko kwao malawi (mzuzu) kwa ajili ya mibaraka na kuonana nao ana kwa ana

Baada ya safari iliyochukua takriban masaa 18 hatimaye tulifika salama na kupokelewa kwa shangwe na vigelege vya kutosha
siku mbili baadae mama-mkwe alinichukua na kwenda kunitembeza nikaone mji na kweli kale kamji ni kadogo lakini kamepangiliawa vizuri sana na kwa sababu tulikuwa na usafiri wetu binafsi tuli-enjioy sana
tukiwa katika maongezi ya hapa na pale nilimtania mama-mkwe japo wajukuu wanasumbua katika maombi yake asilisahau na hilo kwani linampa tabu sana
Lah haula hamadi ndipo yule mama alipoanza kufunguka juu ya yule binti yake kwamba kama hakuwa na taarifa basi
hiyo ndio rasmi ni hivi binti yake kipindi anasoma alipewa mimba na mwanafunzi mwenzake na ile mimba ilimsumbua sana mpaka kupelekea kufanyiwa operesheni na bahati mbaya mtoto alikufa hivyo aliwekewa vijiti na madaktari walimshauri akae zaidi ya miaka mitatu ndo anaweza kubeba mimba
kutokana na taarifa ile ilibidi kesho yake nianze safari ya kurudi bongo huku nikimuahidi aendelee kukaa kwa mwezi mmoja zaidi ili nijipe muda wa nini cha kufanya

Wana JF tumezoea kuzibwa kwa mirija ya uzazi ili mwanamke asizae hivi inawezekana kweli mwanamke akawekewa vijiti sehemu za ukeni na asizae na wala mwanaume usijue?
na kama kweli ni kisayansi au kimitishamba mbali na hilo niegundua kuwa waifu wangu ni material wife hilo pekee yake linaweza sababisha nimuache?
kwanini amenisubilisha badala ya kuniambia ukweli?
hivo vijiti havina side effect kwenye mwili?
wakwe zangu wamekuwa wawazi na kuonyesha ushiriano mkubwa sana kwangu nafikili mila na desturi zinachangia ingekuwa hapa naona wangechuna tu hii inakuwaje?
natanguliza shukrani mawazo yanayojenga ahsanteni na tufunge mwaka kwa salama ni mi wenu KIFIMBOPLAYER
 
ilo mbona Kawaida? na sio lazima kuwekwa kwenye papuchi, wanaweka ata kwenye mkono.....
 
mkuu mayombo kwenye mkono kuna mahusiano gani na viungo vya uzazi
 
Kama mna nia moja nendeni hospital mkatoe hivyo vijiti mzae!
 
Mke kutozaa sio dhambi,ila kilichoharibu hapo why hakukwambia yaliyojili tangu awali? Piga chini usiendelee kupoteza milkshake yako hapo.
 
kama uwezekano huo nitafanya hivo mkuu swat
 
la kutokuniambia mapema naona ndo tatizo lakini kwa mambo mengine ni binti mmoja mzuri sana anajituma katika kazihapendi mambo ya umbeya umbeya akimaliza shughuri zake ye ni ndani hana tyme na mtu
 
kuweka vijiti ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango. inabidi akatolewe hivyo vijiti ili aweze kushika ujauzito

naloliona gumu kidogo hapo ni daktari kumwambia asishike ujauzito mpaka baada ya miaka mitatu. je hiyo miaka mitatu ilishafika. maana inawezekana alipata complications (kama uterus kuchanika) kwenye ujauzito wake wa kwanza ndio maana akaambiwa asubiri kwanza mpaka baada ya muda flani ndio abebe mimba

baya zaidi ni kukuficha ukweli kuhusu hali yake. kwanini alificha?
 
Soma hapa kama lugha ya watu inapanda.

nashukuru sana chief kwa hiyo elimu mpaka njiti za kiberiti zinatumika nimeshangaa sana
na imeainisha hasara na faida, gharama jinsi ya kutumia nk naamini kabisa hii ni teknolojia mpya inahitaji uzoef ukidogo naweza ona wakunga kwa hizi hospital za wilaya au mpaka mikoani
 
Ndoa ndoano,vumilia three years sio inshu kwenye uzima.
 
kuweka vijiti ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango. inabidi akatolewe hivyo vijiti ili aweze kushika ujauzito

naloliona gumu kidogo hapo ni daktari kumwambia asishike ujauzito mpaka baada ya miaka mitatu. je hiyo miaka mitatu ilishafika. maana inawezekana alipata complications (kama uterus kuchanika) kwenye ujauzito wake wa kwanza ndio maana akaambiwa asubiri kwanza mpaka baada ya muda flani ndio abebe mimba

baya zaidi ni kukuficha ukweli kuhusu hali yake. kwanini alificha?

nashukuru dada venin nilivyofatilia niliambiwa ni kweli alipatwa na matatizo kwenye mirija (uterus)
kwa hiyo iliitaji muda kidogo kujitazamia nadhani ndo maana walimpa miaka hiyo mitatu
 
la kutokuniambia mapema naona ndo tatizo lakini kwa mambo mengine ni binti mmoja mzuri sana anajituma katika kazihapendi mambo ya umbeya umbeya akimaliza shughuri zake ye ni ndani hana tyme na mtu

Ubea si mpaka ajue lugha vizuri? And I'm pretty sure that hajui kiswahili vizuri.so usitumie hicho kama kigezo
 
Ndoa ndoano,vumilia three years sio inshu kwenye uzima.
ni kweli GIDE japo inauma sana unajitahidi kujipinda lakini wapi unachanganya karanga na mihogo wapi kumbe umewekewa njiti za kiberiti inauma sana
 
Ubea si mpaka ajue lugha vizuri? And I'm pretty sure that hajui kiswahili vizuri.so usitumie hicho kama kigezo

ahhhh mkuu chaja usiniombee mabaya maduu wa kibongo ndo kupiga domo lakini huyu sidhani japo kiswahili chake cha kuunga unga
 
Ndugu yangu kila binadam anamapungufu isipo kua yanatofautiana. Nikweli alifanya makosa kuto kukuambia mapema lkn labda aliogopa kukupoteza akidhan kua utamwacha, lkn pia kama mambo mengine yupo safi usifuache utaja juta ww kwahil la kuto kukuambia msamehe but kama kuna mengine zaid ya hilo fanya maamuzi magum.
 
Vijiti vinatumika sana tu kuzuia ujauzito,cha msingi hakikisha hiyo miaka mi3 inatimia kama alivyoshauriwa ndio vikatolewe.
Kama inawezekana nendeni pamoja mkapewe elimu ya uzazi wa mpango na hasa hiyo njia ya vijiti ambayo mkeo ameitumia,maswali yako yote yatajibiwa vizuri huko.
Kukuficha pia usimlaumu sana,inawezekana alihofu kuwa usingejisikia vizuri kujua ali conceive akiwa shule na katika umri mdogo.
Msamehe na muendelee na maisha
 
Hapa kuna mengi unataka tukushauri. Nakuambia hivi, Mke si shamba useme maadamu nimepanda mbegu pale lazima nitavuna tu. Maajabu ya Mungu ni kuwa, wale wanao mtafuta mtoto kwa bidii na nguvu zote, hawapati ila wale wasomtaka kabisa ndio wanampata hata kwa zile dakika 10 tu za kiwimawima. Hayo tumwachie Mungu.
Sasa, sijui kama ulimwambia mkeo kuwa unataka mtoto kwa udi na uvumba. Naamini angekuambia tulia tu muda ukifika mtoto atakupa. Hilo ndio jibu sawia. Hakujua kuwa ukienda kwao unaenda kujadili na mamkwe wako ati mimi namwekea mbegu mwanao lakini hazipandi. Angelilijua hilo asinge kupeleka kwao ukayasikie hayo.
Jambo jingine nataka ujue, sio kwamba mama mkwe wako hakutaka ujue siri hiyo ya kutokumpata mtoto. Aliipanga rasmi kabisa ili upaparike, ukasirike umwachie mwanaye. Akafanikiwa. Mission accomplished.
Si ajabu, Malawi saa hii wanakula fungate
 
Back
Top Bottom