mke wangu si muelewi

mke wangu si muelewi

wazawa

Senior Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
184
Reaction score
58
mwaka wa tisa huu nko ktk ndoa ila si muelewi mzazi mwezangu kabisa
tymejaliwa mtoto kabla hapo tulishiriki vema kuihudumia ndoa yetu kwa mapenzi mazito baada ya kujifungua mtoto hiv sasa mapenz yamehama kabisa
kuanzia kujipendezesha na kunihudumia mm..mtoto kawa ndo kila kitu..hadi najuta kwa nn tulizaaa..natamani ni mgeregaze haka katoto ila ndo tunda la mapenzi yangu
namiss na ninakosa upenzi wake nifanyaje
 
Mwaka wa tisa au mwezi wa tisa??
Lakn hiyo hali mara nyingi hutokea..Mvumilie huku.ukijitahid kumwelewesha unavoumia..Na mtoto akikua atabadilika.
 
Yeuwiii ulikuwa hujawa tayari kuzaa.kumbe uulitegemea nini,tubu kwa ulichotamani kumfanya huyo mtoto mana akikua cjui utanunulia wapi mapenzi ya ubaba kwake
 
Pole pole mtafika tu ndio mapenzi hayo na ndoa si lelemama
 
duh! Umesema unatamani kumfanya nini mwanao vile? Dah dunia ni mviringo aisee.

Pole sana kwa mapenzi kupungua au kwisha.
Muite mwenza wako muongee labda anaweza kubadilika. Ila ndio ujue hali hii hutokea mara nyingi na si jambo la ajabu
 
mwaka wa tisa huu nko ktk ndoa ila si muelewi mzazi mwezangu kabisa
tymejaliwa mtoto kabla hapo tulishiriki vema kuihudumia ndoa yetu kwa mapenzi mazito baada ya kujifungua mtoto hiv sasa mapenz yamehama kabisa
kuanzia kujipendezesha na kunihudumia mm..mtoto kawa ndo kila kitu..hadi najuta kwa nn tulizaaa..natamani ni mgeregaze haka katoto ila ndo tunda la mapenzi yangu
namiss na ninakosa upenzi wake nifanyaje

Sasa unataka tukusaidie nini hapa ndani. Hayo ni mambo yako binafisi, sisi tunahusika vipi?. Halafu inabidi uelewe kitu kimoja. Asilimia 40% ya binadam they dont care your problems. The remaining 60% is very happy that you are swiming on problems. So, dont expose your problems. It doenst help.
 
pole sana ila vumilia tu. ndoa hupita katka hatua tatu. moja ni mapenzi motomoto ya pili ni mafarakano na tatu ni mapenzi kurudi kama zamani. sasa hapo mlipo ndio hatua ya pili mabayo kama hakuna uvumilivu basi ndoa huvunjika na mkiweza kuvuka hatua ya pili basi mambo ni murua kabisa huko mbeleni.
 
not always the case.
 
mwaka wa tisa huu nko ktk ndoa ila si muelewi mzazi mwezangu kabisa
tymejaliwa mtoto kabla hapo tulishiriki vema kuihudumia ndoa yetu kwa mapenzi mazito baada ya kujifungua mtoto hiv sasa mapenz yamehama kabisa
kuanzia kujipendezesha na kunihudumia mm..mtoto kawa ndo kila kitu..hadi najuta kwa nn tulizaaa..natamani ni mgeregaze haka katoto ila ndo tunda la mapenzi yangu
namiss na ninakosa upenzi wake nifanyaje

Usituletee utoto hapa umewauliza swali hili wazazi wako?
 
The best thing a father can do to a child is to love his mother..Mpende mkeo tu regardless and eventually it will pay off. Mfikirie mwanao si wewe tu.
 
My gud.
Huu ndio wivu wa baba kwa mwanae.
Baba wengi wakiona mke kazaa na upendo umeamia kwa mtoto uanza fujo ama maneno.
hoo huyu mtoto unamdekeza, hooo huyu mtoto unampenda sana.
Ndio maana wanawake usema wanaume akili zao kama watoto.

Jua mwanamke kumpenda mtoto ni nature, tena anaweza kumpenda hata wa mwenzake.
Kupenda mtoto/watoto ni kama hobby yao.
Mungu kamumba hivo, jaribu kumfanya uyo mtoto kitu kwa wivu wako, atakutangazia ubaya dunia mzima. Atakuita muuaji, mchawi, shetani nk.
Hujui wanawake wewe.

Ushauri.
Ila ukimsaidia kumpa upendo huyo mtoto, hakika utaona mabadiriko, yeye atakupenda wewe kwa vile unampenda mtoto wake.
Kama unataka kujua juu ya wanawake wenye watoto, siku moja ukimuona mama na mtoto wake, mchangamkie mtoto wake, ongea na mtoto wake, msifie mtoto wake, utaona atakavo kushobokea na atakupenda hata kimapenzi.

Kwaiyo kuwa bizi kwa mtoto nawe pia.
Kama vile unaweza kuchange nepi, kumlisha mtoto, kumuogesha, kumpeleka hospitali, kumuimbia mtoto, umpakata, kumpakaza mafuta mwilini, kumvesha nguo, kucheza nae.

Kwa mfano ile unaingia tu home unaenda kumchukua mtoto na kukaa nae, kumprotect, kumfeed, na kumpa upendo.

Na inabidi ujue child baic needs
Physiological needs,
Safety needs
Love and belonging needs

Ukisha jua hayo utakuwa baba kamili na imara.
Haufai kuwa raisi wa jamhuru ya muungano wa tanzania, hutaki watoto wazaliwe waje kutusaidia uzeeni, unataka attention na ngono basi. Unajifikiria mwenyewe.
 
duh,pole sana mkuu.vumilia, yatakwisha,mwenzio nina watoto wawili katika ndoa yangu na sijawahi thubutu kuwaza mabaya juu ya watoto wangu. please tubu kwanza kwa mola wako kwa kumdhania vitu vibaya mwanao ili mkeo akupende and then fanya yafuatayo yakiwa ni baadhi ya kumfanya mkeo akupende kama hapo awali:
1. Kubaliana na ujio wa mtoto wenu katika ndoa yenu kuwa ni baraka toka kwa mungu.
2. Mtoto wako umchukulie kama ni sehemu ya upendo katika ndoa yenu. Mpe nafasi kama ulivyompa nafasi
mkeo.Ukionesha kumchukia mtoto ni rahisi sana kwa mkeo kukupotezea kwa sababu humpendi mtoto aliyembeba yeye
tumboni kwa miezi 9 yenye mateso na karaha nyingi.
3. Jitahidi kumpendezesha mkeo kwa sababu katika kipindi hiki wanawake walio wengi huwa hawajipendi, mawazo yao
kwa sehemu kubwa yapo kwa watoto tu.Fikiria ni namna gani utamfanya mkeo awe up to date kama zamani,pia
waweza kuwa unamletea mtoto wenu zawadi za mara kwa mara kiasi kwamba mama nae ataanza kurudisha mapenzi
taratibu kwako.
4. Mara moja moja toka na mkeo out either mkiwa wawili tu or wote watatu.namaanisha na mtoto wenu.
5. Kamwe usifikirie kutoka nje ya ndoa yako kwa sababu ya hali hii.Ndo utaongeza matatizo mengine ya kumchukia
mkeo pamoja na mtoto wenu.
 
Hili ni jambo la kawaida sana katika ndoa. Wanawake wakishazaa mapenzi yao yote huhamia kwa mtoto. Hadi mtoto akue at least akiwa na mwaka mmoja ndiyo mama ataanza kurudisha mapenzi kwako.
 
Pole sana na kinachoendelea ndani ya familia yako..inaonekana una wivu sana mpaka kufikia hatua ya kumwonea wivu mwanao...ushauri wangu jaribu kuyagawa mapenzi kwa mkeo na mwanao pia tafuta kitu kitakacho kufanya uwe busy mfano movies,soma vitabu na vitu Kama hivyo..mwisho ni swala la muda tu Mvumilie mke wako hayo mambo yataisha tu muda ukifika
 
mwaka wa tisa huu nko ktk ndoa ila si muelewi mzazi mwezangu kabisa
tymejaliwa mtoto kabla hapo tulishiriki vema kuihudumia ndoa yetu kwa mapenzi mazito baada ya kujifungua mtoto hiv sasa mapenz yamehama kabisa
kuanzia kujipendezesha na kunihudumia mm..mtoto kawa ndo kila kitu..hadi najuta kwa nn tulizaaa..natamani ni mgeregaze haka katoto ila ndo tunda la mapenzi yangu
namiss na ninakosa upenzi wake nifanyaje

Mkuu miaka 9 ya ndoa+?ya uchumba=10+ ya mahusiano bila kuwa na mototo, we uoni mke wako yuko excited na ana furaha ya ajabu, masimango na aibu ya mama mkwe na wifi zake nadhani yameisha sasa
huyo mtoto ndio furaha na mkombozi wake katika hii Dunia ya kuchunguzana na kudharirishana, nadhani wewe ndio unayaona sasa , lakini ni kawaida sana
 
Ndo matatizo ya kufunga ndoa bi arusi akiwa mjamzito, wenzio wanaoa 4 love wanakaa miaka2 kuenjoy ndoa yao then wana zaa, wewe mihemko yako kwa mkeo bado iko juu mara mtoto huyo kawasili, unataka asimcare mtoto wenu akupe wewe attention ya ngono too pathetic saidiana na mwenzio mlee mtoto wenu ndo matunda ya ndoa hayo ndoa ni zaidi ya ngono kijana
 
Mkuu@somoe umenena jambo ambalo ni sahihi!
 
Back
Top Bottom