Mke wangu ndio kasababisha nimsaliti

Lion01

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
474
903
Kwanza kabisa naomba nishauri, ukibahatika kukutana na mtu unayempenda hata siku moja usije ukauliza au ukapata udadisi wa kuuliza mambo yake ya zamani, wewe Anza kumpenda pale mlipo anzia.

Okey turudi kwenye mada, nimekuwa nikiishi na mke wangu tangu tuanze kukaa pamoja huu ni mwaka almost WA nane, sijafunga nae ndoa lakini few months to come Mungu akijalia nitafunga nae pingu za maisha.

Katika kukaa kwetu Mungu katujalia watoto kadhaa na tunafuraha.

Mimi kama mwanaume tangu nizaliwe sijawah kukutana na mwanamke mwingine kimwili na Wala sijawahi kufikilia kumsaliti Kwa sababu nampenda sana tena sana.

Lakini mambo yalikuja kubadilika siku tulioamua kusimuliana mambo ya nyuma hasa mahusiano, Nilimwambia yangu ambayo yalikuwa dhaifu sana, Alinisimulia Mengi ya kwake alikuja kupigilia msumali pale aliponiambia Aliwahi KUNISALITI daaah.

Hapo hadi vipepeo vilicheza tumboni, nilishituka sana tena sana WHY? Kwa sababu nilimpenda na kumuamini sana kiasi kwamba sijawahi kufikilia kama anaweza nisaliti na Wala sijawahi kumuuliza kama amewahi kunisaliti na alinisaliti.

Mimi nikiwa nakomaa na PCB mitaa Fulani ya mkoa WA Kilimanjaro.

Amekaa na hiyo Siri takribani miaka nane yote niliokaa naye,

Nilijitahidi kumsamehe Kwa moyo wangu wote, lakini imagine unaishi na mwanamke aliekusaliti ingawa anasema mara moja lakini huwezi jua kama ni kweli au laah mana takribani miaka 3 tangu tuanze mahusiano tulitengana mi shule Alevel na yeye shule O level, sasa imagine wewe mwanaume hujawahi kumsaliti daah!!!

Ni kama udhaifu Fulani ivi!,
Laiti angeniambia mapema basi mahusiano yangeisha pale pale lakini tayari tuna watoto,.

Kimoyo safi mwanaume nikatoa msamaha lakini ule ukuta imara alionijengea wa kuto msaliti ukawa umeishia hapo, mana Kuna muda nilikuwa na uwezo hata WA kufanya mapenzi na mtu mwingine but najizuia Kwa sababu yake nikujua hajawahi nisaliti but not for today.

Kuna msichana nimemfukizia Kwa muda Wa wiki tatu, na Leo rasmi nimemsaliti mke wangu kipenzi kama alivofanya yeye miaka kadhaa nyuma. Na nimemsaliti sio Kwa sababu simpendi, hapana ila nataka nibalance mzani nisiwe namuona yeye anahatia ila nami nijiunge nae.

So kutokea Leo sintakuja tena kumsaliti mke wangu na Wala sitawahi kuja kumwambia nimemsaliti.

NB: Kuyaandika haya ni kwamba nimetoa la moyoni Ili hata siku nijichanganye vip yeye hata kuja kujua Wala sitakuja kumuambia
#ACHA YALIOPITA YAPITE
Mahusiano ya mtu wako kabla ya wewe usitake kuyajua kabisa.
NAWASILISHA NAOMBA KUSAMEHEWA
 
Kwanza kabisa naomba nishauri, ukibahatika kukutana na mtu unayempenda hata siku moja usije ukauliza au ukapata udadisi wa kuuliza mambo yake ya zamani, wewe Anza kumpenda pale mlipo anzia.
Hivi nyie wakristo mbona mnapenda sana kuzini utakaje na mwana mke miaka mine una zini nae tu. Ndoa huna na unaona ni kawaida na fahari sana mpaka unasimlia watu, mnasingizia kupata pesa na pesa zenyewe mpaka leo mnakosa.......
 
Hivi nyie wakristo mbona mnapenda sana kuzini utakaje na mwana mke miaka mine una zini nae tu. Ndoa huna na unaona ni kawaida na fahari sana mpaka unasimlia watu, mnasingizia kupata pesa na pesa zenyewe mpaka leo mnakosa.......
Kwani waislamu ambao hawajafunga ndoa ila wanaishi kama mke na mume???
 
Mkuu similizi zake ndo zinaonyesha kwamba ni mkristo huwezi kukaa na mtoto wa mtu miaka minne af akawa nanguvu kusimlia hivo, wao wanaona ni sehemu ya maisha.

Kwa hiyo kwenye simulizi umeiona dini kuliko makosa yake, ungeamua kumsema yeye binafsi bila kuingiza dini comment yako isingekamilika
 
Back
Top Bottom