mke wangu muhuni simtaki, nataka mtoto wangu.....

mke wangu muhuni simtaki, nataka mtoto wangu.....

kipusy

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
639
Reaction score
323
Nimegundua mke wangu anatoka nje miez sita sasa kwa ushahidi wa kuwarecord kwa kutegesha recording kwenye simu yake baada ya kuchoka vitimbwi na kutopewa haki ya ndoa mara kwa mara na kuchelewa kurudi home pia safari nyingi kila weekend. Nikaamua kumtenga chumba baada ya kugombana na pia kutopata msaada kutoka kwa ndugu na wazazi wake kwani cku zote wamekua wako upande wake hata afanye baya gani.

Baada ya kumtenga chumba akaanza kushughulikia uhamisho kwan yeye ni mwalimu wa primary. Nilimihamishia mkoa ninao fanya kazi mimi cha ajabu halmashauri ya jiji imempa uhamisho, na mtoto wangu kamtorosha(ana miaka 6) na kwenda kumuanzisha darasa la kwanza mkoa mwingine wakati tayari nilishamtafutia shule nzuri english medium. Naombeni msaada wa mawazo na SHERIA.
 
Sioni kama ni sahihi kumuhusisha mtoto mdogo kwenye ugomvi wenu kwasababu hujui anaathirika kiasi gani kisaikolojia...Nyinyi ni watu wazima,hata kama mmechokana na mmeshindwana mnatakiwa muwe na makubaliano huyo mtoto mtamleaje na katika misingi gani!Nakushauri ukae kitako na huyo mwenzi wako na muongelee suala hili kwa undani kwa maslahi ya mtoto wenu.Na ikiwezekana pia muweke tofauti zenu pembeni na mumlee pamoja kwasababu mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote wawili!Jaribu kuhusisha ndugu au marafiki wa karibu wa pande zote mbili vilevile.
Na kama yote hayo yakishindikana sheria ichukue mkondo wake.Mtoto wote mna haki nae sawa 50/50,Unapewa 50% custody ya mwanao!
 
ss unasubiri nn na mtu kashasepa?
huna mke hapo anza mbele.
pole sana
 
Namsupport mimi49,fanyeni makubaliano mtoto asiwe affected na vurugu zenu,inawezekana
 
Last edited by a moderator:
Nimegundua mke wangu anatoka nje miez sita sasa kwa ushahidi wa kuwarecord kwa kutegesha recording kwenye simu yake baada ya kuchoka vitimbwi na kutopewa haki ya ndoa mara kwa mara na kuchelewa kurudi home pia safari nyingi kila weekend. Nikaamua kumtenga chumba baada ya kugombana na pia kutopata msaada kutoka kwa ndugu na wazazi wake kwani cku zote wamekua wako upande wake hata afanye baya gani.

Baada ya kumtenga chumba akaanza kushughulikia uhamisho kwan yeye ni mwalimu wa primary. Nilimihamishia mkoa ninao fanya kazi mimi cha ajabu halmashauri ya jiji imempa uhamisho, na mtoto wangu kamtorosha(ana miaka 6) na kwenda kumuanzisha darasa la kwanza mkoa mwingine wakati tayari nilishamtafutia shule nzuri english medium. Naombeni msaada wa mawazo na SHERIA.

mwache aende, chukua mwanao umtunze
 
Kwan huna uwezo wa kuzalisha mtoto mwngne weweee?acha kuogopa mkuuuu tafta mke mwngne zalisha tunza kidi
 
Sioni kama ni sahihi kumuhusisha mtoto mdogo kwenye ugomvi wenu kwasababu hujui anaathirika kiasi gani kisaikolojia...Nyinyi ni watu wazima,hata kama mmechokana na mmeshindwana mnatakiwa muwe na makubaliano huyo mtoto mtamleaje na katika misingi gani!Nakushauri ukae kitako na huyo mwenzi wako na muongelee suala hili kwa undani kwa maslahi ya mtoto wenu.Na ikiwezekana pia muweke tofauti zenu pembeni na mumlee pamoja kwasababu mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote wawili!Jaribu kuhusisha ndugu au marafiki wa karibu wa pande zote mbili vilevile.
Na kama yote hayo yakishindikana sheria ichukue mkondo wake.Mtoto wote mna haki nae sawa 50/50,Unapewa 50% custody ya mwanao!

Kifupi sio rahic kukaa tena kwani yeye kama yeye hana uamuzi wa mambo yake. Mama mkwe ndio anampelekapeleka sana. Na huyo mama alinitamkia kama nimemchoka nimpe talaka yake kwani ndoa za kiislamu hazina kugandana. Pamoja na mambo mabaya aliyonifanyia mtoto wake anashinikiza tuachane
 
Duh, ndoa za siku hizi bwana. Yaani hamna siri kabisa. Jamani haya mambo ya kuibiwa mke yalikuwepo toka enzi hizo ndio maana kukawa na msemo wa 'kitanda hakizai haramu'. Kipindi tunakuwa tulikuwa tunasimuliwa kuwa fulani sio mtoto wa mzee mwenye mke lakini anatumia jina la ukoo huo. Na nakumbuka nilishaoneshwa baba zangu wadogo kama 4 hivi ambao babu alizaa na wake za watu na hawatumii jina la uko wetu kwani wanaeleweka ni watoto wa mwenye mke. Sio kwamba zamani wake za watu na waume za watu walikuwa hawatoki nje, ni usiri tu na uvumilivu ulikuwa ukiendelea wakati huo.
 
Hapo anaepata madhara ni mtoto atakua katika inferior life malezi bora kwa mtoto yanaanzia kwa upendo wa wazazi. Mi binafsi nimelelewa na mzazi mmoja kiukweli uwa sina raha na maisha haya ingawa ni mtu mzima kwa sasa. Ongea na mzazi mwenzio labda mnaweza mkatatua ilo tatizo kwa faida ya mtoto lakini
 
kifupi sio rahic kukaa tena kwani yeye kama yeye hana uamuzi wa mambo yake. Mama mkwe ndio anampelekapeleka sana. Na huyo mama alinitamkia kama nimemchoka nimpe talaka yake kwani ndoa za kiislamu hazina kugandana. Pamoja na mambo mabaya aliyonifanyia mtoto wake anashinikiza tuachane
unampenda mkeo?unamuhitaji?Mapenzi yenu nyinyi kwanini mnahusisha watu wengine?
 
Dokta ushanga,
anaongeza nguvu za kiume, kurudisha mpenz aliyepotea!
 
Daah...pole sana,kiukweli mapenz yanauma,me nakushauri fanya mambo yako ila pata muda wa kutosha kuwa karibu na mtoto kumtembelea,kuwa na mawacliano ya karibu hata akiwa naye huko poa, na uzuri dini yako inaruhusu kuwa na mke mwingine OA..kila la kheri.
 
Back
Top Bottom